Katibu Tawala Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga,Ameshiriki katika ufunguzi wa programu ya siku tatu mafunzo ya awamu ya kwanza ya kuwaongezea uwezo na maarifa wataalam 30 wa RUWASA kupatiwa mafunzo ya usanifu,usimamizi,na uendeshaji wa miradi inayotumia nishati ya umeme jua,utafiti na uendelezaji wa rasilimali za maji chini ya ardhi iliyoandaliwa na RUWASA na Shirika la Global Water Centre.
Wataalamu hao wanapata mafunzo hayo kwa lengo la kwenda kuwa wakufunzi kwa wataalamu wengine zaidi ya 300 ili kuwa wabobevu katika suala la usanifu ,usimamizi,na uendelezaji wa miradi inayotumia umeme jua, utafiti na uendelezaji wa rasilimali za maji chini ya ardhi.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo,Katibu Tawala Mkoa wa Singida,amesema kuwa mradi huo unatarajiwa kwenda kupunguza gharama za upatikaji wa maji kwa wananchi hasa wale wa vijijini wenye uwezo mdogo na hali duni kwa kupata maji ya uhakika,kwa gharama nafuu na kwa ufanisi zaidi.
Amewaasa washiriki hao kutumia mafunzo hayo vizuri kwa lengo la kwenda kuleta mabadiliko katika jamii zetu katika maswala ya usanifu na miradi hiyo akisema kuwa nia mafunzo hayo endapo yakifanyiwa kazi vizuri yatakwenda kuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wote wakiwemo wale ambao wanapata changamoto ya maji.
"Ni vema tukawa wasikivu na kuelewa vizuri kwasababu tutakachokipokea sisi ndicho kitakacho kwenda kuleta tija katika eneo kubwa zaidi ,hivyo tuhakikishe tunafahamu zaidi namna ya kutunza miradi hiyo kwani itakuwa jambo la fedheha kushindwa kuendeleza mradi huu na kupata matokeo hasi ambayo haikutarajiwa kwa kurejea katika matumizi makubwa ya gharama ikiwemo matumizi ya mafuta ya dizeli ambayo gharama yake ni kubwa ukilinganisha na gharama za umeme wa jua"amesema Daktari Mganga.
Pia katika mafunzo hayo,wataalamu wanatarajia kufanya ziara ya katika miradi wa Kinyamwenda uliopo takribani kilometa 40 kutoka Singida Mjini kwa lengo la kujifunza zaidi namna ya kuwa na maarifa sahihi ya usimamizi wa miradi ya maji inayotumia nishati ya jua
Umuhimu wa programu hiyo ni kuongeza ufahamu wa kutosha juu ya mfumo wa matumizi ya nishati ya umeme jua katika miradi ya maji na kutambua mafanikio na changamoto juu ya miradi inayotumia nishati hiyo kwa kuainisha changamoto na utatuzi wake hususani katika miradi iliyokwama na kufahamu mitaala inayoweza kuboresha na kuendeleza ujuzi ili kuwa na utekelezaji wenye mafanikio katika miradi inayotumia mfumo wa nishati ya umeme jua na kujifunza namna ya kuongoza programu na viashiria vya mafanikio katika miradi inayotumia nishati ya umeme wa jua kuhakikisha wananchi wanapata rasilimali maji ya kutosha na yenye viwango vya hali ya juu.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.