Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewashauri wabunge wote wa Mkoa wa Singida kushirikiana kutafuta fedha Serikalini ili kusaidia utekelezaji wa miradi kumi (10) ya Barabara ya Mkoa huo iliyopangwa kutekelezwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
Ushauri huo ameutoa wakati wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoani hapo Machi 12, 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano baada ya Wakala wa Barabara ya nchini TANROADS kutoa taarifa kwamba katika mwaka wa fedha wa 23/24 wana jumla ya miradi 10 yenye jumla ya Km 1718.31
Serukamba amebainisha kwamba, endapo miradi hiyo kumi ikitekelezwa kwa ufanisi mkoa utakuwa umepiga hatua kwenye upande wa miundombinu ya usafirishaji hivyo ni jukumu la kila Kiongozi kutafakari namna ya upatikanaji wa fedha hizo.
"Nashauri zoezi la utafutaji wa fedha za utekelezaji wa mradi wa barabara ufanywe na kila mmoja wetu, wabunge mkatusaidie Bungeni TANROAD muongeze uhusiano na makao makuu ili tuhakikishe fedha zinapatikana" Alisema Serukamba.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji TARURA Mhandisi David Tembo amesema katika bajeti ya mwaka 2023/24 jumla ya Bilioni 21.43 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo zikiwa Bilioni 5.73 zinatokana na mfuko wa barabara, Bilioni 4 zinatokana na mfuko wa jimbo wakati Bilioni 10.65 ikiwa ni ongezeko la bajeti ya tozo ya mafuta.
Hata hivyo wajumbe walipongeza taasisi hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakifungua na kukarabati barabara huku baadhi ya wakuu wa Wilaya waliomba kuongeza idadi ya taa za Barabarani ili kupendezesha miji pamoja kuongeza usalama wa watu na mali zao.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.