• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

UVAMIZI WA TEMBO IKUNGI WAPATIWA MWAROBAINI WAKE.

Posted on: October 28th, 2024

Kufuatia uvamizi wa tembo katika kijiji cha Mkiwa wilayani Ikungi,Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ameelekeza timu ya Askari Uhifadhi 18 kuweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kwa lengo la kukabiliana na tembo wanaovambia makazi ya watu.

Hatua hiyo inafuatiwa na tukio la hivi karibuni la tembo kuwepo katika eneo hilo na kusababisha taharuki kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara  Oktoba 28,2024 kwenye Kijiji cha Mkiwa Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida Mhe. Chana amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo inapungua au kumalizika kabisa.

"Tunakwenda kuongeza askari watakaotusaidia kuhakikisha tembo wanarudi katika maeneo yao ya hifadhi sambamba na kuongeza mabomu baridi kufukuza tembo" Mhe. Chana amesisitiza.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji,Wilaya  na Mkoa itafanya zoezi la kutambua na kuweka alama katika maeneo ya Korido za wanyamapori (shoroba) na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutoweka shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

"Baada ya kuzitambua shoroba tunataka kuwepo na shughuli za uhifadhi mfano kuanzisha Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) ili kuendeleza uhifadhi" Mhe. Chana amesisitiza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Chana amesema Serikali inaenda kuweka mpango wa matumizi bora ya Ardhi ili maeneo ya mifugo, makazi na kilimo yajulikane.

Mhe. Chana ametaja mikakati mingine ya kudhibiti tembo kuwa ni kuwafunga kola maalum kujua uelekeo wa kundi la tembo,kutoa elimu kwa Askari wa Vijiji (VGS) na kufanya sensa ya wanyamapori.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amewataka wananchi wa Ikungi kutoa ushirikiano kwa Askari Uhifadhi hao ili kukabiliana na tembo ipasavyo ikiwemo kwa wahitimu wa jeshi la akiba kupata mafunzo maalum juuvya kukabiliana na tembo ili kuwa msaada pale ambapo tembo watajitokeza eneo hilo.

Kadhalika Mhe.Dendego baada ya kuhitimisha mkutano kuhusu madhara ya Tembo alibaki katika kusikiliza na kutatua kero mbali mbali za wananchi wa Ikungi.

Salome  Njiku,mkazi wa Ikungi,amefurahishwa na ujio wa Waziri na viongozi wa Mkoa na wilaya akisema kuwa ni wazi kuwa serikali inawajali kwa kuwapa kipaumbele katika kuhakikisha usalama wao dhidi ya uvamizi wa tembo na sasa wanaamini kupitia mikakati mbali mbali iliyowekwa watakwenda kuwa salama na kuendelea na shuhuli zao za maendeleo ikiwemo kilimo cha mazao mbali mbali.

Mkutano huo umehudhuriwa na wananchi pamoja na Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka Mkoa wa Singida na Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake ikiwa ni siku mbili baada ya wanachi wa Mkiwa wilayani Ikungi kufunga bara bara kushinikiza serikali kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu baada ya tembo kuharibu nyumba na mazao yao.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.