Mkuu wa Mkoa wa Singida amewataka Wadau wa kudhibiti ukimwi nchini kutumia vyema taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na binafsi ili kubaini rasirimali zilizopo na kuongeza bajeti kwenye sekta hizo ili kupunguza utegemezi wa fedha kutoka nje kwa ajili ya mapambano ya VVU na UKIMWI.
Akifungua mkutano wa usambazaji wa taarifa ya mapato ya matumizi ya fedha za ukimwi kwenye sekta za umma na binafsi ya mwaka 2022 ambao unafanyika mkoani hapa, Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba amesema hatua hiyo itasadia kuwa na mipango endelevu katika kudhibiti VVU na UKIMWI nchini kufikia mwaka 2030 kama ilivyo malengo ya dunia katika kumaliza ugonjwa huo.
Amesema taarifa hiyo inasaidia Serikali kujua kiwango cha matumizi ya fedha katika utekelezaji wa afua za VVU na ukimwi kubaini changamoto za fedha na kuweka mikakati madhubuti ili kutatua changamoto hiyo.
Akizungumza kando ya mkutano huo Mkurugenzi wa fedha na utawala wa TACAIDS, Yassin Abbas amesema mkutano huo umewakusanya waratibu wa ukimwi kutoka kwenye Wizara, mikoa Halmashauri na sekta binafsi lengo likiwa ni kusambaza taarifa ya matumizi ya fedha za ukimwi katika sekta ya umma na binafsi.Amesema mkutano utajikita kujua namna nchini inavyowekeza fedha katika mapambano ya ukimwi na kutambua maeneo ambayo fedha zinapelekwa ili kusudi iwaisaidie kupanga mipango ya kukabiliana na ugonjwa huo.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.