Wakazi wa Kijiji cha Ughandi B Wilayani Singida Mkoani hapo wamekabidhiwa rasmi Mradi wa maji wenye ujazo wa Lita Elfu 90 na wametakiwa kutunza Mazingira na vyanzo vya maji ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa leo na Msaidizi wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2022 Emmanuel Ndege Chacha wakati wa uzinduzi wa Mradi wa maji unaomilikiwa na Wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) ambapo aliwataka wananchi kutunza mradi huo pamoja na kuyalinda Mazingira kuzungukia vyanzo vya maji ili yaendelee kupatika kwa muda mrefu.
Kabla ya kuzindua Mradi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alibainisha baadhi ya kasoro katika chanzo cha maji na taratibu za malipo hapo aliwataka kufanya marekebisho hayo madogo huku wananchi wakiendelea kupata manufaa ya mradi huo.
Chacha amezitaka kamati za maji za eneo hilo kuhakikisha wanatunza na kukarabati miundombinu ya maji badala ya kusubiri RUWASA.
Hata hivyo Kiongozi huyo amewataka Wahandisi kufuata maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya maji katika kutekeleza miradi hiyo.
Hata hivyo amewataka RUWASA kuwa na kawaida ya kutoa taarifa kwa wananchi pindi wanapofanya usafi au matengenezo ya miundombinu ya maji hayo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.
Awali Meneja wa RUWASA Mhandisi Athumani Mkalimoto amesema Mradi huo umekamilika na umeanza kuhudumia wananchi wa eneo hilo.
Hata hivyo Mhandisi amebainisha kwamba Mradi umeokoa kiasi cha Milioni 155.1 baada ya kutumia gharama kiasi cha Tsh.Milion 410.4 ambapo ulitengewa bajeti ya Tsh.Milioni 565.5 mpaka kukamilika alieleza.
Aidha Mhandisi Athumani ameeleza kwamba wananchi wapatao 5500 wa Kijiji cha Ughandi B wamekuwa wakifaidika na uwepo wa Mradi huo.
Mwenge wa Uhuru huo umekamilisha mbio zake katika Wilaya ya Singida baada ya kukagua na kuzindua miradi mitano na programu tano ambazo Mwenge wa Uhuru zote zilipitishwa.
Mwisho
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.