WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imewagiza Watendaji wa vijiji, kata na mitaa katika halmashuri ya Manispaa ya Singida kuliweka katika agenda ya kudumu kwenye vikao vya Kamati za Maendeleo za Kata (WDC) suala la anwani ya makazi ili kuweka uendelevu wa usimamizi na uhakiki wa taarifa za anwani za makazi na kuwasihi wakazi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikia ili kufanikisha uhakiki huo sanjari na taarifa zao kuingizwa katika mfumo wa anwani za makazi.
Mtaalamu wa Mfumo wa anwani za makazi kutoka Wizara hiyo, Innocent Jacob, amesema hayo (Machi 15, 2024) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Uhakiki Anwani za Makazi katika Mfumo wa Kidigitali (NaPA) yanatolewa kwa watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya uhakiki wa anwani za makazi.
Jacob amesema anwani za makazi ni muhimu sana kwasababu zinasaidia ulinzi na usalama,kutoa huduma kwa wakazi na pia inasaidia biashara mtandao kupitia fumo wa Kidigitali (NaPA). Kwaupande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Adrianus Kalekezi, amewaagiza Watendaji wa Kata vijiji na wenyeviti wa mtaa kutekeleza kikamilifu zoezi hilo na kutoa taarifa kwa wakati katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ili kujua kila hatua ya utekelezaji.
Naye Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mtaa katika Manispaa ya Singida Abilai Hussein,ambaye ni Mwenyekiti wa Mji wa zamani amewasihi wenyeviti wenzake kuunga mkoano juhudu za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kwa kushiriki kikamilifu utoaji taarifa sahihi ili kuhakikiwa na kuwekwa katika mfumo wa anwani za makazi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.