Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ametembea mradi wa maji unaotekelezwa katika mji wa Manyoni mkoani Singida unaotarajiwa kugharimu Sh. 29 Bilioni ukitarajiwa kuwahudumia zaidi ya wananchi elfu 64 katika kata ya Mkwese, Muhalala, na Manyoni mjini na kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa maji safi na salama kufikia Januari 2025.
Silaa amewataka watendaji wanaotekeleza mradi meradi huo kuhakikisha unakamilika kwa Wakati Kulingana na thamani ya fedha iliokusudiwa huku akiwasisitiza Kutunza Mazingira na kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na manufaa wa kazi wenzi wa mji wa Manyoni
Hayo yamejiri Oktoba 22,2024 katika Halmashauri ya Manyoni mkoani Singida wakati akiwa katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kukagua, kuzindua na kutembelea miradi Mbalimbali ya mawasiliano na miradi mingine ya kimaendeleo
“kazi hii ndio matokeo ya fedha ambazo tumekuwa tukizisema Wakati wote ambao Mheshimiwa Rais amekuwa akizileta kwaajili ya miradi ya Maendeleo, kwahiyo niwatie shime watendaji katika mradi huu wahakikishe unakamlika kwa Wakati kutokana na fedha na wananchi tuendelee kuitunza miradi hii kwa manufaa yao” alisema
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe, Halima Dendego ameishukuru serikali kwa uwezeshaji wa mradi huo na kwamba utakapokamilika utasaidi sana katika kutatua changamoto ya maji na kumaliza Maswali ya wananchi ya kuwa mradi unakamilika lini
“Tumeshatembelea sana hapa lakini tunashukuru kwa msaada wa serikali hii mana tunaenda kupata maji ndani ya muda mfupi”
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Manyoni Vincent Bashinji katika taarifa yake, mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 30 za utekelezaji wake huku vijana zaidi 85 wakipata ajira kutokana na mradi huo na kuchochea ukuaji wa uchumi katika eneo hilo
Aidha waziri silaa ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mlowa iliopo halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni wenye thamani ya zaidi ya sh. 493 milioni
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.