Wananchi wa Mkoa wa Singida wameshauriwa kufanya mazoezi na kuendeleza kula mlo kamili ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuimarisha afya ya akili na mwili.
Akizungumza baada ya kukutana na mwandishi wetu katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida Afisa Lishe Mkoa Bi. Teda Sinde amesema ni muhimu makundi matano ya chakula yazingatiwe wakati wa ulaji na kufanya mazoezi ili kujenga afya Bora.
"Kwa Mkoa wa Singida makundi haya ni uwele, mahindi, mchele, mtama, ulezi na kundi la pili ni la mikunde na vyakula vyenye asili ya wanyama kama maziwa, nyama, mayai, samaki, na dagaa kundi la tatu matunda na mboga na kundi la tano mafuta, sukari na asali" Alisema Teda.
Aidha amebainisha kwamba kundi la tano ambalo ni la sukari, mafuta na asali linatakiwa kutumika kwa kiasi kidogo ili kupunguza uzito mkubwa na mafuta mengi mwilini.
Bi Teda alimalizia kwa kutoa wito kwa vijana na wazee kuhakikisha wanafuata utaratibu wa ulaji ili kuepusha magonjwa katika miili yao.
Afisa Lishe Mkoa Bi. Teda Sinde wakati wa mazungumzo na Mwandishi wa Habari (hayupo pichani) katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida
Moja kati ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Hussen Mwatawala akiwa katika mazoezi
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.