Mjumbe wa Tume huru ya uchaguzi,Mhe,Dkt.Zakia M.Abubakar ametoa wito kwa wananchi Mkoani Singida kutoa ushirikiano kwa asasi mbali mbali zinazotoa elimu ya mpiga kura katika kipindi hiki cha uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Hayo yamesemwa (Septemba 14,2024) katika mafunzo kwa watendaji ngazi ya Mkoa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura aliyofanyika katika Chuo cha uhasibu Mkoani Singida yaliyohusisha mratibu wa uandikishaji wa Mkoa,maafisa uandikishaji,maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo,maafisa uchaguzi,maafisa ugavi na maafisa TEHAMA Wa halmashauri.
Amesema kuwa matokeo bora ya zoezi hili yatategemea ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji,serikali,vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kwa kuwa na ushirikiano mzuri na wa karibu na tume wakati wote wa utekelezaji.
Dkt.Zakia Amesema kuwa Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi hiki ambapo jumla ya asasi 290 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo huku akisisitiza utekelezaji wa majukumu katika kila eneo.
Baadhi ya wajumbe wakishiriki katika Mkutano wa Mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi na uandikishaji wa daftari la wapiga kura.
Pia,amesisitiza utunzwaji wa vifaa vya uandikishaji kwani vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini na gharama za ununuzi wake ni kubwa sana na endapo utunzwaji wake hautazingatiwa kutapelekea athari kubwa katika ukamilishwaji wa zoezi hilo.
Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la wapiga kura Mkoani Singida linatarajiwa kuanza Septemba 25,2024 na kukamilika Octoba mosi.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.