Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amewaagiza Maafisa Afya katika mkoa huo kuwachukulia hatua kali wananchi ambao watabainika kukaidi kufanya usafi katika maeneo yao kama hatua ya kuondoa tatizo la magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Mkuu wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mjini Manyoni.
RC. Dendego amesema mwananchi wa mkoa wa Singida wanao wajibu wa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na wanaopuuza sheria za usafi wawajibishwe kwa sababu wanaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo magonjwa ya mlipuko.
“Wananchi tekelezeni sheria za usafi za Halmashauri na za nchi katika kutunza mazingira yenu ili kuepuka maradhi yanayozuilika, Amesisitiza Dendego.
Naye, Afisa Afya wa Wilaya ya Manyoni Seif Swed amesema Halmashauri hiyo imejipanga vizuri katika zoezi la usafi wa mazingira ambapo wameweka siku ya Jumatano kuwa ni siku ya usafi kwa wananchi wote na mwisho wa mwezi.
Swed amesema kwa sasa Halmashauri hiyo ni Moja ya Halmashauri zinazofanya vizuri kwenye suala la usafi mkoani Singida hivyo amewahimiza wananchi waendelee na moyo huo katika kufanya usafi ili Halmashauri hiyo iweze kushika namba Moja Kitaifa kwa usafi wa mazingira.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Manyoni walioshiriki zoezi la usafi wamesisitiza kuwekwa mkazo katika matumizi ya sheria hasa kwa wananchi ambao wanakaidi kufanya usafi kwenye maeneo yao.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.