• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Watakao chelewesha miradi ya maendeleo Singida kukiona - Serukamba

Posted on: June 1st, 2023

Siku tatu baada ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga kutoa maagizo kwa Mkandarasi anayejenga wodi mbili na nyumba ya kuhifadhia Maiti Wilayani Manyoni ya kuwalipa staahiki zao mafundi na vibarua leo Mkuu wa Mkoa huo, Peter Serukamba naye ametembelea eneo hilo na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni kulipa fedha za Mkandarasi huyo na kuwalipa mafundi pamoja na vibarua ili kazi iweze kukamilika kwa wakati.

RC Serukamba ametoa maagizo hayo baada ya kupewa taarifa na Mhandisi wa Wilaya hiyo, Gabriel Mayaya kwamba, kazi ya ujenzi inachelewa kwa sababu Mkandarasi haonekani eneo la kazi na vibarua  hawajalipwa fedha zao jambo ambalo huchangia kusuasua kwa kazi hiyo ndipo alipotoa maelekezo fedha hizo kukatwa na kuwalipa vibarua na mafundi huku akimtaka Mhandisi huyo kuongeza usimamizi ili kazi ikamilike kwa wakati.

"Huwezi kuacha kuwalipa vibarua halafu utegemee kazi itamalizika, Mhandisi kaa na Mkurungezi chukueni fedha za Mkandarasi lipeni vibarua wake kwa kuwa inafahamika kiasi wanacholipwa kwa kazi walizofanya" Serukamba

Aidha amemuagiza Mhandisi Mayaya kuongeza mafundi wengine kwa kuwa sehemu ya ujenzi iliyobaki ni kubwa na mafundi ni wachache huku muda ukiwa ni mdogo uliobaki.

"Hatuwezi kumsubiri mtu ambaye hata ‘site’ haonekani, fedha zake walipeni hao vibarua na tafuteni mafundi wengine ili kazi ikamilike kwa wakati".

Hata hivyo RC Serukamba amebainisha kwamba mtumishi yeyote atakayeshindwa kusimamia miradi ya maendeleo Mkoani Singida na akasababisha fedha kurudi hazina watakuwa wamehatarisha vibarua vyao.

Hata hivyo akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni, Elias Moleli (Afisa Maendeleo ya Jamii) Wilayani hapo amemuahidi Mkuu wa Mkoa kwamba wataongeza mafundi na watahakikisha kazi inafanyika usiku na mchana na kwa viwango vinavyotakiwa.

Aidha Moleli amesema tayari wamenunua vifaa vyote muhimu vikiwemo mabati nondo na madirisha na mbao kwa ajili kukamilisha kazi hiyo.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI WA ZIARA

 

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.