Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imetoa mafunzo kwa Maafisa Watendaji wa Kata zote 20 za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Mafunzo hayo yamefanyika Januari 23, 2025 katika Ukumbi mkubwa wa mikutano wa Halmashauri.
Mafunzo hayo yametolewa na Wawezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), makao makuu Dodoma, wakiongozwa na Makamu mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Mohamed Khamis Hamad.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe. Mohamed Khamis Hamad amesema moja ya majukumu ya tume ni Pamoja na kutoa elimu kwa umma katika makundi mbali kama vile viongozi, wananchi wa kawaida, wanafunzi na watendaji wa kata nchini ambao hupata taarifa kwa urahisi zaidi kutoka kwa wananchi.
"Ninyi ndio mnakaa na wananchi, mnapata taarifa nyingi. Tukiwa karibu na nanyi na ushirikiano mzuri tutapata taarifa nyingi kwa kwaajili ya kuleta ustawi wa wananchi wetu.” Amesema Mhe. Mohamed Khamis Hamad
Mafunzo yamelenga kuwakumbusha Watendaji namna ya kukabiliana na changamoto za uvunjifu wa haki za binadamu ikiwemo masuala ya ukatili wa kijinsia, utatuzi wa migogoro mbalimbali katika maeneo yao, pamoja na utekelezaji wa majukumu kwa nafasi zao kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.