Watu sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba zausajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.
ACP Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka (32) ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizigo mingi.
Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha Mwakiti.
ACP Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijijicha Ilongero.
Ameongeza kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.
Ameeleza kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.
“Hawa wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida,Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.