Kuelekea katika sherehe ya krisimasi Desemba 25,na mwaka mpya 2025, Uongozi wa Sekretarieti ya mkoa wa Singida umeandaa na kukabidhi zawadi mbali mbali kwa Watumishi kama kielelezo cha upendo na kujali kuelekea katika sikukuu /sherehe za krisimasi na mwaka mpya.
Akizungumza wakati wa gafla hiyo,Kaimu Katibu Tawala Ndg.Starnslaus choaji, amesema tukio hilo limefanyika kwa lengo la kuthamini mchango watumishi wote kwa ushirikiano waliokuwa nao pamoja kwa muda wa mwaka mzima uliofanikisha mipango na malengo mbali mbali yaliyokuwa yamepangwa kufanyika.
"Zawadi hizi ni sehemu ndogo ya kuonyesha kuthamini uwepo wa watumishi wote kwa kuonyesha ushirikiano ambao umezaa matunda ya mafanikio katika kuhakikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida inafanya kazi kwa weledi katika kuwahudumia na kuwafikia wananchi wake kwa wakati."alisema Choaji
Ameongeza kwa kusema kuwa motisha hizo hazitafikia tamati kwani licha ya kufanyika kila mwaka,mwakani zitaboreshwa zaidi na kupendeza kuliko ilivyo sasa.
Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Bi.Josephine Mbozu akizungumza kwa niaba ya watumishi wengine baada ya kupokea zawadi hizo ameushukuru uongozi wa Sekretarieti kwa kuwajali na kuutambua mchango wao katika taasisi hiyo.
" Tunashukuru sana kwa zawadi ya Christmas,Zawadi tulizopata zimetufaa sisi pamoja na familia zetu, tunasema Asante kwa upendo wenu kwa sisi watumishi .Mwenyezi Mungu awabariki sana kwa kutujali"alisema Bi.Josephine.
Akionyesha kufurahia baada ya tukio hilo,Katibu wa Madereva Bw,Shamakala amesema ni jambo la faraja kwa viongozi kutuamini mchango wao katika kazi hivyo wamewapa chachu ya kuzidi kuipenda kazi yao kwani mahusiano kati yao na viongozi ni mazuri na mazingira ya kazi ni ya furaha na amani.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.