• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WATUMISHI NA VIONGOZI MKOANI SINGIDA WAPEWA MAFUNZO KUINUA UTENDAJI KAZI

Posted on: December 18th, 2024

Katika kuhakikisha viongozi wanafanya kazi zao Kwa uadilifu na utawala Bora,Madiwani,wakuu wa divisheni na vitengo,wenyeviti wa vijiji,Mitaa na vitongoji  katika Wilaya ya Ikungi na Halmashauri ya Singida wamepatiwa Mafunzo Kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi ili kuwa daraja zuri katika kuwaunganisha wananchi na Serikali.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg.Justice L.Kijazi amefungua mafunzo ya kuboresha utendaji kazi kwa madiwani na wakuu wa divisheni na vitengo katika Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.

Mafunzo hayo yameanza tarehe 16 Disemba, 2024 huku yakitarajiwa kuendelea mpaka tarehe 20 Disemba, 2024 ambapo Halmashauri imeandaa mafunzo ya ujazaji tamko la maadili kwa viongozi kufuatia matakwa mapya ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma ya ujazaji wa tamko la rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kwa njia ya mfumo kwa mujibu wa sheria.

"Tumealika viongozi kutoka taasisi mbalimbali ili kutoa mada kuhusu uboreshaji utendaji kazi wetu hivyo tutakuwa na mada kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na tamko la rasilimali na madeni na masuala ya serikali za mitaa" amezungumza Kijazi 

Mkurugenzi Mtendaji ameongeza na kusema kuwa mwisho wa kujaza Tamko la maadili ni tarehe 31 Disemba, 2024.

Kwa upande wao baadhi ya wajumbe katika mafunzo hayo wameishukuru Halmashauri kwa kutenga bajeti kwa ajili ya mafunzo hayo kwani yanaenda kuwa chachu katika utendaji kazi katika maeneo yao.

Lengo la mafunzo hayo ya siku 5 nii kuwawezesha viongozi hao kujifunza maswala ya utawala bora kwa maslahi mapana ya wananchi wa wilaya ya Ikungi na mkoa wa Singida kwa ujumla.

Kwa upande mwingine Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji  kutoka katika halmashauri ya Singida wamepatiwa mafunzo ya Uongozi kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi katika maswala ya uongozi ili kuleta Maendeleo kwa wananchi na kuisaidia Serikali yanayofanyika Kwa siku mbili Disemba 18 na 19,2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ilongero.


Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( OR-TAMISEMI),yameandaliwa na uongozi wa Halmashauri na kutolewa na wawezeshaji kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Bw.Shabani Mongomongo amewapongeza wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji kwa kuaminiwa na   kuchaguliwa kuwaongoza wananchi akiwasihi  kusimamia misingi ya uongozi pasipo kuingiliana katika utendaji kazi.Sambamba na hilo,ametoa Pongezi kwa Chuo Cha Hombolo kwa kukubali kutoa mafunzo hayo.

       Jumla ya wenyeviti wa vijiji 84 na wenyeviti wa vitongoji 435 wanatarajiwa kupata mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa siku mbili.


Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.