• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

WAZIRI JAFO APONGEZA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA AFYA IKUNGI

Posted on: March 6th, 2018

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi nzuri  ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.Mhe.Jafo alitoa pongezi hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua  miradi ya maendeleo na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ihanje.Aliongeza kuwa Kituo cha Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200  vitakavyopekea/vilivyopokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.Nimekagua majengo yote sita yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi  kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za ujenzi hupungua ukilinganisha na  wakandarasi; Hii  inanipa faraja kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu, Alisema Mhe.Jafo.Awali akitoa taarifa hiyo  Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  Sembua Mrisho amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa bohari ya dawa kwa ajili ya  vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.“Mara baada ya kupokea Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii imefanyika kwa kutumia “Local fund” na  inasimamia na Wakandarasi wa Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.Aliongeza kuwa  Kituo cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi  mahitaji kutokana na kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.Akizungumza kwa furaha Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a mtoto.Ukarabati sambamba na uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha Vituo vya Afya 161.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.