• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

"SINGIDA BILA VVU NA TATIZO LA AFYA YA AKILI INAWEZEKANA":DAKTARI MGANGA.*

Posted on: November 28th, 2024

Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa WA Singida  leo tarehe 28,aNovemba 2024 wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu udhibiti wa VVU, UKIMWI na ugonjwa wa Afya ya akili kwa Watumishi wa Umma mahali pa kazi yaluyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuanzia saa tatu kamili asubuhi.

Akiwasilisha mada kuhusu VVU na UKIMWI,Dr. Said Mgeleka ambae ni Meneja wa Mradi kutoka USAID AFYA YANGU mkoa wa Singida, ametoa mada kuhusu hali ya Maambukizi wa VVU na UKIMWI  kwa,uwiano wa wagonjwa kijiografia,umri, Jinsia na Hali ya Ndoa, katika Mkoa wa Singida.

Kuhusu Maambukizi ya VVU kwa Jinsia Amesema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa jinsia ya kiume imekuwa nyuma katika kupima VVU NA UKIMWI kwani kati ya jumla ya wateja 27,678 waliopo kwenye Huduma za Matibabu; wanaume ni  ni 8,581 asilimia 31%  pekee huku wanawake wakiwa 19,097

"Kundi linaloongoza Kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI ni watu waliopo katika ndoa sababu kuu ikiwa ni kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja huku kata ya Mandewa na Misuna ikitajwa kuongoza Kwa idadi ya maambukizi" amesema Dr.Mgeleka.

Naye Dkt.Lewis Rwegayula,ambaye ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singidaa amewasilisha mada kuhusu tatizo la Ugonjwa wa Afya ya Akili akianisha sababu,dalili na matibabu ya afya ya akili huku akiwaasa watumishi kutumia muda vizuri kwa kuhakikisha wanamaliza majukumu yao Kwa wakati husika ili kuweza kuyamudu vema mazingira ya kazini na baada ya kazi,Pia kuyatambua mahitaji ya viongozi wao na kuyatekeleza vema ili kuepusha migogoro kazini itakayoweza kuwasababishia tatizo la afya ya akili kwa lengo la kuwa na matokeo mazuri katika kazi.

"Ni vema pia Kwa viongozi kuzitambua vema tabia za wasaidizi wao Ili kufahamu vyema namna gani watawaongoza na kuwasimamia katika utendaji wao wa kazi,pia Kila mmoja ayatambue mapungufu yake na kuyafanyia kazi ili kutokuwa sababu Kwa wengine kupata tatizo la afya ya akili".alisema Dkt Lewis

Pia amewasihi watumishi kuepuka kutumia dawa ambazo hawajaelekezwa na Daktari kwani nazo huchangia tatizo la Afya ya Akili.

Akizungumza Kwa niaba ya Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe,Dkt.Shilla Mwashiuya amewaasa watumishi kuwashauri wenzao Wenye tatizo au dalili za afya ya akili ndani na nje ya ofisi Kwa kuwatia moyo wahusika na kuwasaidia pale inapowezekana na sio kuwavunja moyo na kuzidi kuwakatisha tamaa inayozidisha uwezekano wa  kupata tatizo la Afya ya Akili.


Katibu  Tawala WA Mkoa wa Singida,Daktari Fatuma Mganga akizungumza baada ya kuwasilishwa Kwa mada hizo amesema ni wakati sasa wa kuamua kunadilika kitqbia Kwa Kila mmoja kuhakikisha anajiepusha na mazingira yote yenye kuweza kusababisha maambukizi ya VVU huku akisisitiza watumishi kuwa na uthubutu wa kupima afya zao katika magonjwa ya kuambukiza na Yale yasiyoambukiza ili kuzifahamu Hali zao vema.

Kuhusu tatizo la Afya ya Akili amesema ni vema watumishi kutumia muda wao mwingi katika shuhuli za kujiingizia kipato baada ya kazi za ofisini ili kupunguza wimbi la watu Wenye tatizo la Afya ya Akili mara baada ya kustaafu akisisitiza matumizi Sahihi ya fedha na kutunza akiba Kwa manufaa Sahihi ya baadae.

"Tukapime afya zetu Kwa kupima magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza,Pia ni vema kufanya mazoezi ya viungo mara Kwa mara ili kuuweka mwili mbali na magonjwa"alisema Daktari Mganga.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.