Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala Wilayani Mkalama ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega imetembelea na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali wilayani Mkalama.
Ziara hiyo inayotarajiwa kuwa ya siku mbili kuanzia tarehe 1-2/11/2024 imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Nyumba ya walimu katika shule ya Sekondari Mkalama One, kutembelea Jumuiya ya watumia maji kijiji cha Nkungi, Ujenzi wa barabara ya Nkungi- Mng'anda, ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu shule ya msingi Kinyangiri, ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani -Kinyangiri pamoja na ujenzi wa madarasa 3 pamoja na matundu 6 ya vyoo shule ya msingi Mwandu
Ziara hiyo inatarajia kuendelea Novemba 2,2024 kwa kupita na kukagua miradi katika vijiji vya Kisuluiga, Miganga, Muntamba, Dominiki na Kidarafa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.