Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikagua kitanda cha chumba cha upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akina mama wa Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi huku wakiandamana na kutoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akipanda mti katika eneo la kituo na kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki (kulia) na mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Singida Aisharose Matembe (kushoto) mara baada ya kukagua jengo la utambuzi wa magonjwa la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua kituo na kiwanda cha kuongeza thamani ya mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UN Women Tanzania Maria Karadenizli.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.