• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

SINGIDA YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA USAFI WA MAZINGIRA

Posted on: August 15th, 2025

 Viongozi na wataalamu wa afya wametakiwa  kusimamia kwa umakini utekelezaji wa Mradi Endelevu wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSSP) ili kufanikisha lengo la kuwa na mkoa wenye viwango vya juu vya usafi ifikapo mwaka 2025.

Akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi huo leo (15 Agosti 2025),   Katibu Tawala Msaidizi wa Sehemu ya Mipango na Uratibu Mkoa wa Singida Ndg.Nesphory Bwana, akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, amesema mpango huo, unaotekelezwa kwa mfumo wa Malipo kwa Ufanisi (Result Based Financing), umewezesha mkoa kupokea zaidi ya shilingi bilioni 6.42 katika kipindi cha miaka mitano, na kuboresha miundombinu ya maji na usafi katika vituo 154 vya kutolea huduma za afya.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Victorina Ludovick amesema miradi ya usafi wa mazingira na uboreshaji wa miundombinu ya maji imekuwa chanzo muhimu cha mapato kwa mkoa, na kufafanua kuwa mwaka 2021 ulipokelewa mtaji wa kuanzia wa shilingi milioni 262.87, lakini hadi kufikia mwaka wa fedha 2024/2025 zaidi ya shilingi bilioni 6 zimepokelewa. Fedha hizo zimetumika kujenga vyoo, vichomea taka, kuboresha maeneo ya huduma za mama na mtoto na miundombinu ya maji safi na salama.

Aidha, amesema kikao hicho pia kinajadili ushirikiano na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa ukaguzi na usajili wa maeneo ya biashara, ambapo asilimia 40 ya mapato yatabaki halmashauri na asilimia 10 kuingia mkoani, hatua ambayo itaimarisha mapato.

Naye Afisa Afya Mkoa wa Singida, Bw. Mgeta Sebastian, ameeleza kuwa huduma za WASH zimeboreshwa na kuwafikia makundi maalumu, hususan wenye ulemavu na afya ya mama na mtoto huku Idadi ya kaya zenye vyoo bora ikiongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2020 hadi 75.9 mwaka 2025, kadhalika vifaa vya kunawia mikono vikiongezeka kutoka asilimia 16 hadi 46 katika kipindi hicho. Amesema pia uelewa wa wananchi kuhusu usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo jumuishi umeimarika.

Bw. Mgeta ameongeza kuwa mkoa umefanikisha ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa miradi, kuhamasisha jamii kutumia vyoo bora, na kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kijamii na kidini katika kutekeleza sheria za mazingira.

Kikao hicho kimeazimia kuendelea kusimamia kwa ufanisi miradi ya maji na usafi wa mazingira, ili Singida ibaki kinara wa afya bora na mazingira safi nchini.



Kwa undani zaidi wa yaliyojiri katika kikao hicho tafadhali fatilia kiungo kifuatacho kuona Video ya kikao hicho

https://youtu.be/AuKmMZfwCgU

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • SINGIDA YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA USAFI WA MAZINGIRA

    August 15, 2025
  • WAZAZI WASIOPELEKA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM SHULENI KUCHUKULIWA HATUA

    August 14, 2025
  • SINGIDA YAADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI – VIJANA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA

    August 12, 2025
  • "ARDHI NI MAISHA – TUIKUMBATIE KAMA URITHI WA VIZAZI VYETU" : RC HALIMA DENDEGO

    July 21, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.