Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amesisitiza umuhimu wa kutunza amani na utulivu katika Taifa letu,akisisitiza waumini kuendelea kutunza umoja na ushirikiano walio nao kama nyanja muhimu ya kuwaweka pamoja na kufanya shughuli za maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Juni 7,2025 katika kanisa la Unyankindi Mkoani Singida wakati alipoalikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee ya ujenzi wa kanisa hilo ambapo pia amewahimiza wananchi kutumia jukwaa la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu vema kwa ajili ya kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo na kuitunza amani iliyopo hapa nchini.
“Tunaenda kwenye uchaguzi mwaka huu. Tuendelee kuomba amani. Suala hilo litufikie na liishe salama. Tuwe wamoja – iwe Waislamu, Wakristo, KKKT au dhehebu lolote – tuwe wamoja katika kulinda amani,” amesema Mhe. Dendego
Aidha, Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa kusaidia kwenye ujenzi wa nyumba za ibada ni sehemu ya maandalizi ya safari ya kiroho ya kila mwanadamu hivyo ni vema kila mmoja kushiriki ili kuwezesha kazi ya Mungu kusonga mbele kadhalika na kumpa kila mmoja baraka.
“Msafiri bora ni yule aliyefunga mizigo yake sawasawa.. na mizigo hiyo ni kama hii ya ujenzi wa kanisa, kusaidia maskini, kuwajali yatima. Haya yote yanatuandalia safari njema ya kesho,”
Naye Mchungaji Livingstone kutoka nchini Kenya,akizungumza qakati wa harambee hiyo,amewaasa Watanzania kuilinda na kuitunza vizuri amani waliyonayo kwqni ni hazina kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na utulivu uliopo nchini Tanzania ambao unawapa wananchi nafasi ya kushiriki vema katika shughuli za uzalishaji ambazo zimekua kichocheo kikubwa cha maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
“Nimesafiri nchi nyingi sana, lakini amani ya Tanzania ni ya kipekee. Tanzania mna amani sana chini ya uongozi huu. Ithaminini hiyo amani yenu,” amesema.
Kwa upande wake, Mchungaji Dr. David, Askofu Mkuu wa Kanda ya Kati wa Kanisa la Waadventista Wasabato, amemshukuru Mgeni rasmi wa Shughuli hiyo- Mkuu wa Mkoa na waumini wote wa ujumla kwa kukubali kushiriki katika harambee hiyo iliyogusa mioyo yao na kufanikiwa kufikia lengo lililotarajiwa.
Katika harambee hiyo iliyokua na lengo la kukusanya jumla ya Shilingi Milioni mia moja,imefanikisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia moja na kuvuka lengo lililopangwa hapo awali huku Mkuu wa Mkoa akichangia kiasi cha Milioni 15.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.