• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Agriculture

TAARIFA YA SEHEMU YA UCHUMI NA UZALISHAJI


  • UTANGULIZI

Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji inaratibu majukumu ya Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Maliasili, Biashara, Viwanda, Madini na Ushirika. Utekelezaji wa majukumu katika sekta hizi ambazo kwa kiasi kikubwa ndiyo zinazoajiri wananchi wengi wa Mkoa wa Singida ni wa kuridhisha.

Uzalishaji katika sekta ya Kilimo ni wa unatosheleza mahitaji ya chakula kwa mwaka na kubakiwa na ziada ambayo wananchi wanauza na kujipatia kipato kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo zikiwemo ujenzi wa makazi ya kisasa, kugharamia matibabu na mavazi. Uzalishaji wa mazao ya biashara na hasa zao kuu la alizeti bado ni mdogo kutokana na changamoto zilizopo na hasa upatikanaji wa pembejeo za kisasa hususan mbegu bora. Changamoto hizo zinapelekea uzalishaji mdogo ambao haukidhi mahitaji ya malighafi ya mbegu za alizeti kiasi cha tani …. Kinachohitajika katika viwanda ….. vilivyopo ndani ya Mkoa. Utekelezaji katika kila Sekta umeoneshwa hapa chini.

  • SEKTA YA KILIMO

Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi ya wakazi wa Mkoa wa Singida ambapo takribani 90% ya wananchi wote wanategea kilimo kuwa ni shughuli kuu ya kiuchumi. Mkoa una jumla ya Hekta 1,099,235 zinazofaa kwa kilimo ambapo mazao ya chakula yanayolimwa ni mahindi, mtama, uwele, ulezi, mpunga, viazi vitamu, mihogo na mikunde. Mazao ya biashara yanayolimwa ni alizeti, vitunguu, pamba, korosho, ufuta, choroko, dengu na asali.

  • Uzalishaji wa mazao kwa mwaka 2020/2021 na matarajio ya uzalishaji kwa mwaka 2021/2022
  •  
  • Mazao ya Chakula

Mavuno ya msimu wa 2020/2021yalikuwa ni Tani 821,881.7 za mazao ya chakula. Mahitaji ya chakula kwa mwaka kwa wakazi wote wa Mkoa wa Singida ni Tani 444,688.93 za chakula. Hivyo kulikuwa na ziada ya chakula kiasi cha Tani 377,192.8 kama inavyoonekana katika jedwali la hapa chini:

Jedwali Na. 1: Mahitaji ya chakula 
Halmashauri 
Idadi ya watu
Mahitaji (T)
Uzalishaji (T)
Ziada/Pungufu (T)
Mkalama

    234,237.0

    70,271.1

   186,738.3

          116,467.2

Manispaa

92,017

26,655.93

     9,470.6

          -17,185.3

Itigi

    138,129.0

    37,295.0

     61,395.0

             24,100.0

Iramba

    282,727.0

    77,396.5

   180,943.0

          103,546.5

Singida

    280,874.0

    84,262.2

   159,492.4

             75,230.2

Ikungi

    310,072.0

  84,882.2

  156,594.4

             71,712.2

Manyoni

    236,763.0

  63,926.0

     67,248.0

               3,322.0

JUMLA

        1,574,819.0

444,688.93

821,881.7

377,192.8

Wakazi wa Manispaa wanategemea kununua chakula chao sokoni na hivyo hakuna upungufu wa chakula unaojitokeza. Alama inayoashiria upungufu inatokana na uhaba wa eneo la kilimo kwa sababu eneo kubwa la Manispaa ni kwa ajili ya shughuli zingine za maendeleo ambazo siyo kilimo.

Katika msimu wa 2021/2022 matarajio ni kuvuna tani 812,309.7 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini:

 Jedwali Na. 2: Utekelezaji malengo ya kilimo na matarajio ya mavuno kwa mwaka 2021/2022.

Aina ya zao
       Eneo lililopandwa (Ha)
   Matarajio ya mavuno(tani)
Mahindi

216,268.6

407,011.1

Mpunga

34,017.6

46,406.4

Mtama

74,908.4

111,694.6

Uwele

28,242.3

52,245.9

Ulezi

8,023.9

13,378.0

Ngano

28.0

22.4

Mihogo

15,300.7

59,657.1

Viazi vitamu

48,880.8

121,840.2

Viazi mviringo

30.0

54.0

JUMLA

425,700.3

812,309.7

Jumla ya tani 384,677.4 za mazao ya biashara zinatarajiwa kuvunwa kwa mwaka 2021/2022. Kwa zao la alizeti pekee, jumla ya tani 260,492.5 zinatarajiwa kuvunwa kati ya matarajio ya awali ya kuvuna tani 581,986.3 kutokana na utekelezaji wa mkakati wa Mkoa wa Singida wa kuongeza uzalishaji. Mkakati huo ulilenga kulima Hekta 238,763.6 (sawa na ekari 596,909) ambapo utekelezaji ni Hekta 261,508    zimelimwa (sawa na ekari 653,770). Utekelezaji huu ni zaidi ya lengo kwa 9.5 %. Hata hivyo matarajio ya awali ya kuzalisha tani 581,986.3 yameshuka hadi kufikia matarajio ya kuzalisha tani 260,492.5 kutokana na mashamba mengi kukauka kulikosababishwa na upungufu wa mvua na ubora wa mbegu nyingi zilizotumika kuwa mdogo.

Jedwali Na. 3: Utekelezaji wa malengo ya kilimo na matarajio ya mavuno ya mazao ya biashara mwaka 2021;2022

ZAO
ENEO LILILOLIMWA (Hekta )
Matarajio ya Mavuno (Tani)
Pamba

21,637.4

25,778.1

Korosho

11,983.4

2,873.4

Vitunguu

12,112.6

47,401.4

Alizeti

261,508

260,492.5

Ufuta

6,630.9

6,609.9

Karanga

22,529.8

26,326.0

kartamu

78.0

132.6

Choroko

6,433.0

6,795.0

Dengu

6,973.0

8,268.5

JUMLA

349,808.2

384,677.4

  • Kilimo cha mazao ya Kimkakati
  •  
  • Korosho

Mkoa wa Singida unatekeleza kilimo cha zao la korosho kwa mfumo wa mashamba ya pamoja (block farming). Mashamba ya pamoja yanalimwa katika Halmashauri za Manyoni, Itigi na Ikungi. Utekelezaji wa mfumo huu umesaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Ugani kwa kuwatumia Maafisa Ugani wachache waliopo lakini pia kudhibiti wadudu na magonjwa kiurahisi zaidi. Jedwali hapa chini linaonesha utekelezaji wa kilimo cha mashamba ya pamoja ya korosho.

Jedwali Na.4: Utekelezaji wa mashamba ya pamoja ya zao la korosho

S/N
Jina la eneo la mashamba
Idadi ya Wakulima
Ekari zilizolimwa

HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI

1
MKWESE

345

6,090

2
MASIGATI

683

16,310

JUMLA NDOGO

22,400

HALMASHAURI YA WILAYA YA ITIGI
1
KAMENYANGA

79

1,882.4

2
NJIRII

169

4,676

JUMLA NDOGO

6,558.8

HALMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI
1
MKIWA

1,000

JUMLA KUU

58,917.2

Katika msimu huu wa 2022/2023, serikali imepanga kuupatia Mkoa wa Singida kiasi cha lita 2,255 za kudhibiti na kutibu magonjwa na wadudu wa mikorosho. Aidha, katika msimu wa 2021/2022, serikali iliupatia Mkoa wa Singida mbegu bora zenye ruzuku ya 100% kiasi cha tani 6.238 za korosho ambazo zilisambazwa kwa wakulima.

  • Alizeti

Alizeti ni zao kuu la biashara kwa wakazi wa Mkoa wa Singida. Ili kuongeza uzalishaji, Mkoa uliandaa mkakati ambao ulilenga kulima jumla ya ekari 596,909 ili kuzalisha jumla ya tani 581,986.3 za alizeti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo. Katika utekelezaji wa mkakati huo, Mkoa ulipokea mbegu za alizeti zenye ruzuku ya 50% kutoka serikali kuu kiasi cha tani 465.2 ambapo kati ya kiasi hicho, tani 453.6 kilisambazwa na kutumika na wakulima. Wadau wengine ambao ni makampuni yanayojishughulisha na kilimo cha alizeti na wakulima wakubwa walifanikisha upatikanaji na matumizi ya tani 35.3 za mbegu chotara za alizeti. Wakulima pia walitumia mbegu walizopata kwa kujinunulia na zile walizotunza kutokana na mavuno ya msimu uliopita. Jitihada hizi zote zimewezesha kulima jumla ya ekari 653,770. Kutokana na upungufu mkubw wa mvua na kiasi kikubwa cha mbegu zilizotumika kuwa na ubora wa wastani, hali ya matarajio ya mavuno ni tani 260,492.5 ikilinganishwa na tani 581,986.3 za matarajio ya awali wakati tunaandaa mkakati wa Mkoa.

  • Upatikanaji wa Huduma za Ugani

Mkoa una jumla ya Maafisa Ugani 161 katika ngazi zote (Sekretarieti ya Mkoa, Ofisi za Wakurugenzi na ngazi za Kata na Vijiji). Ili kuboresha utoaji huduma za Ugani, Serikali Kuu imewapatia Maafisa Ugani wote pikipiki ili waweze kuwafikia wakulima popote walipo kwa urahisi. Hatua hii inatarajiwa kuongeza tija katika shughuli za kilimo na ufugaji kwa kuwa wakulima na wafugaji watapata na kutumia maelekezo ya mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji.

  • SEKTA YA MALIASILI

TAAFIRA FUPI YA SEKTA YA MALIASILI MKOA WA SINGIDA.

Sekta ya Maliasili inashughulikia sekta ndogo za Misitu, Wanyamapori, Ufugaji wa Nyuki, Utalii, Mambo ya Kale na Mazingira.

MISITU.

Sera na Sheria ya Misitu zinahimiza ushiriki wa jamii katika hifadhi ya misitu ya asili ya ardhi ya vijiji ambapo utekelezaji wake umekuwa wa mafanikio ambayo tayari hekta 433,247.48 za misitu zimehifadhiwa katika mkoa. Misitu hiyo ni Mgori wenye hekta 39, 000, Minyughe hekta 230,000, Mlilii Hekta 5,700, Sekenke/Tulya hekta 30,360 na misitu ya wananchi mmoja mmoja na vikundi jumla ya hekta 128,187.48.

Kupitia sekta ya misitu Mkoa una lengo la kupanda miti 10,500,000 kila mwaka sawa na miche ya miti 1,500,000 kwa kila halmashauri ,hata hivyo kutokana na uwepo mkubwa wa mabadiliko ya tabianchi na bajeti za kila mwaka  Mkoa umeweza kufikia lengo la upandaji miti kwa asilimia 70 ya lengo ambapo kati ya miti hiyo inayopandwa asilimia 42 ya miti ndiyo inayokua.

Sekta ndogo ya misitu inakabiliwa na changamoto zifuatazo;

Uvamizi wa misitu unaofanywa na wahamiaji kwa shughuli za Kilimo, Makazi na ufugaji.

Uvunaji holela wa mazao ya misitu hususani  mkaa

Ubanguaji wa miti kwa nia ya kutengeneza mizinga ya asili ya magome.

 

Sekta ndogo  ya  Utalii

Mkoa una lengo la kuendeleza shughuli za utalii katika nyanda kame kwa  kutambua na kutangaza vivutio vya utalii ili kuogeza mapato na ajira kwa wananchi. Tayari Vivutio vipya takribani 31 Vimetambuliwa kwenye Mkoa kama ifuatavyo:

Halmashauri ya Wilaya ya Singida;

Msitu wa Sombi uliopo kijiji cha Msikii, Eneo la juu la kutazama bonde la ufa katika Vijiji vya Msikii na Kinyamwenda (Rift Valley view point),  Michoro ya mapangoni ya Ngimu ,Msitu wa Mgori na Msitu wa Nalogwa Ikingu uliopo Kijiji cha Mkenge.

Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi

Vyanzo vya maji ya moto Misughaa na  Sambaru , Magofu ya Wamisionari wa kwanza Kimbwi na Jiwe lenye bao la kienyeji Ng’ongosoro.

 

Halmashauri ya Manispaa ya Singida

Maziwa pacha ya Singidani na Kindai , Michoro ya mapangoni ya Unyambwa na Boma la Mjerumani na mti uliotumika kusaga nafaka ya chakula cha wafungwa wa enzi za ukoloni.

Halmashauri ya Wilaya ya Itigi,

 Mapori ya akiba ya Rungwa, Muhesi na  Kizigo na Njia ya watumwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama,

Ngoma za asili Uwanza , Boma la Mjerumani na Maeneo ya Wahadzabe katika Kijiji cha  Munguli Kitongoji cha Kipamba.

Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

Michoro ya mapangoni Kisana, Ziwa Kitangiri , Mbuga na tope la Wembere, na Mti wa mikutano ya awali ya  Uhuru.

 Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni

Eneo la katikati ya Tanzania lililopo katika Kijiji cha Chisingisa Kata ya Sasilo ,Bonde la chumvi la Bahi, njia ya Watumwa, Magofu ya Wajerumani katika Kijiji cha Kilimatinde, Eneo la juu la kutazama bonde la ufa (Rift Valley View point)  na Vichaka vya Itigi.

 

Sekta ndogo ya Ufugaji nyuki

Sekta  hii imejikita katika Kukuza uchumi kwa kuimarisha na kuongeza upatikanaji wa mazao ya nyuki yakiwemo asali na nta, ambapo Mkoa huvuna wastani wa tani za asali 296.4 na tani 38.95 za nta. Hata hivyo, Mkoa unakadiriwa kuwa na mizinga ya kienyeji 151,022 na mizinga ya kisasa 12,076.

 

 

Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi

 

Mkoa wa Singida kama ilivyo mikoa miingine haujaachwa katika kupata madhara ya mabadiliko ya tabianchi, ambapo Mkoa umekumbwa na ongezeko la joto na mtawanyiko mbaya wa mvua, hali inayopelekea kupata upungufu wa chakula na magonjwa yatokanayo na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi yakiwemo magonjwa ya mtoto wa jicho na mengine mengi.

Aidha Mkoa umejaliwa kuwa na madini ya aina mbali mbali yakiwemo, Dhahabu, Chumvi, Shaba, Jasi, madini ya ujenzi na Vito vikiwemo quarts na Amethysts.

Sekta ndogo ya Wanyamapori.

Mkoa una mapori ambayo ni makazi mazuri ya Wanyamapori, mapori haya yamegawanyika katika sehemu mkuu mbili za uhifadhi kam ifuatavyo;

Mapori ya akiba yanayomilikiwa na Serikali kuu.

Mapori haya ni Rungwa, Muhesi na Kizigo yaliyopo katika Wilaya ya Manyoni. Mapori haya yenye idadi kubwa ya tembo ukilinganisha na mapori mengine ndani ya nchi yanatumika kwa uwindaji wa kitalii, yakiwa vitalu vya uwindaji ndani yake.

Mapori ya hifadhi ya ardhi za Vijiji

Mapori/ Misitu ya hifadhi ya ardhi ya vijiji iliyopo ni Mgori, Sekenke/ Tulya, Minyughe, Mlilii na misitu ya miingine midogo ya watu binafsi imekuwa makazi mazuri ya Wanyamapori. Misitu hii ina wanyamapori wadogo hadi wakubwa wakiwemo tembo. Misitu hii pia inatumika kama ushoroba/ mapito ya tembo, hasa kwenye mfumo ikolojia wa Rungwa - Serengeti na Rungwa - Tarangire.

 

 

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.