OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA SINGIDA
TATHMINI YA HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA, USTAWI WA JAMII NA LISHE MKOA WA SINGIDA
JUNI 2022
VIFUPISHO
AIDS
ANC |
Acquired Immunodeficiency Syndrome
Antenatal Care |
AFSRH
|
Adolescent Friendly Sexual and Reproductive Health
|
APHTA
|
Association of Private Health Facilities in Tanzania
|
ART
|
Antiretroviral Therapy
|
BOQ
BCG |
Bills of Quantities
Bacillus Calmette Guerin |
CBHS
|
Community-Based HIV and AIDS Services
|
CBO
CECAP |
Community-Based Organization
Cervical Cancer Prevention |
CHMT
CT- SCAN |
Council Health Management Team
Computerized Tomography SCAN |
UVIKO -19
|
Ugonjwa wa Virusi vya Korona 2019
|
CTC
|
Care and Treatment Clinics
|
DM
|
Diabetes Mellitus
|
DMO
|
District Medical Officer
|
DOD
|
Department of Defense (America)
|
DOTS
|
Direct Observed Therapy short course
|
DTHO
|
District Tuberculosis and HIV/AIDS officer
|
DTLC
ECHO LLIN |
District Tuberculosis and Leprosy Coordinator
Electrocardiogram Long Lasting Insecticidal Nets |
FBO
FP |
Faith-Based Organizations
Family Planning |
HBC
|
Home-Based Care
|
HIV
KIHODOWE KKKT iCHF ICU IDSR IPTp2 |
Human Immunodeficiency Virus
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Improved Community Health Funds Intensive Care Unit Integrated Disease Surveillance and Response Intermittent Preventive Treatment of Malaria |
IPD
|
Inpatient Department
|
TPT
MD Mrdt MUAC MRI |
Tuberculosis Preventive Therapy
Medical Doctor Malaria Rapid Diagnostic Tests Mid- Upper Arm Circumference Magnetic Resonance Imaging |
MSD
MYA OJT OR- TAMISEMI |
Medical Stores Department
Magonjwa Yasio ya Kuambukiza On Job Training Ofisi Ya Raisi- Tawala za Mikoani na Serikali za Mitaa |
PMTCT
|
Prevention from Mother-to-Child Transmission
|
RCH
SACCOs SP TASAF TEHAMA TNNS |
Reproductive and Child Health
Savings and Credit Cooperative Organization or Society Sulfadoxine/Pyrimethamine Tanzania Social Action Fund Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Tanzania National Nutrition Survey |
UN
|
United Nations
|
UNFPA
WCD WAVIU |
United Nations Population Fund
Women Children Development Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI |
W4SS
|
WHO – Recommended Four - Symptom’s screening
|
WHO
|
World Health Organization
|
TATHMINI YA HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA, USTAWI WA JAMII NA LISHE MKOA WA SINGIDA
Mkoa wa Singida una wilaya tano (5) ambazo ni: Ikungi, Iramba, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri saba (7) ambazo ni: Halmashauri za Wilaya Ikungi, Iramba, Itigi, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri ya Manispaa ya Singida. Aidha, Mkoa una jumla ya Tarafa 21, Kata 136, Vijiji 441, Mitaa 53 na Vitongoji 2,298. Kwa mujibu wa taarifa ya makadirio ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2021, inakadiriwa Mkoa wa Singida kuwa na idadi ya wakazi wapatao 1,754,370 wanaojumuisha Wanaume 868,646 na Wanawake 885,724.
Huduma za Afya zimeendelea kutolewa kwa kuzingatia Sera, Miongozo na kanuni mbalimbali za Afya katika afua zote za Tiba na Kinga. Mkoa una jumla ya vituo 256 vya kutolea huduma za Afya ikiwa ni Hospitali 11 Vituo vya Afya 20, Zahanati 221 na kliniki 4. Rejea Kiambatisho Na 1(a) na 1(b)VIAMBATISHO
Kiambatiusho Na 1(a) : Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoa wa Singida
|
Serikali |
Mashirika |
FBO/NGO |
Binafsi |
Jumla |
Hospitali
|
5 |
0 |
6 |
0 |
11 |
Vituo vya Afya
|
18 |
0 |
1 |
1 |
20 |
Zahanati
|
189 |
0 |
25 |
7 |
221 |
Kliniki
|
0 |
0 |
1 |
3 |
4 |
Jumla
|
212 |
0 |
33 |
11 |
256 |
Kiambatisho Na 1 (b): Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za afya Mkoa wa Singida kwa umiliki
Halmashauri
|
Hospitali
|
Vituo vya Afya |
Zahanati |
Kliniki |
Jumla |
||||||||
Serikali
|
Mashirika ya Dini (FBOs)
|
Binafsi
|
Serikali
|
Mashirika ya Dini (FBOs)
|
Binafsi
|
Serikali
|
Mashirika ya Dini (FBOs)
|
Binafsi
|
Serikali
|
Mashirika ya Dini (FBOs)
|
Binafsi
|
||
Iramba
|
1
|
0
|
0
|
4
|
0
|
0
|
33
|
6
|
1
|
0
|
0
|
0
|
45
|
Ikungi
|
0
|
2
|
0
|
3
|
0
|
0
|
37
|
3
|
0
|
0
|
0
|
1
|
46
|
Itigi
|
0
|
1
|
0
|
2
|
0
|
0
|
15
|
1
|
2
|
0
|
0
|
0
|
21
|
Manyoni
|
1
|
1
|
0
|
2
|
0
|
0
|
31
|
4
|
2
|
0
|
0
|
0
|
41
|
Mkalama
|
1
|
1
|
0
|
3
|
1
|
0
|
28
|
6
|
0
|
0
|
0
|
0
|
40
|
Singida DC
|
1
|
1
|
0
|
3
|
0
|
0
|
32
|
3
|
0
|
0
|
0
|
0
|
40
|
Singida MC
|
1
|
0
|
0
|
1
|
0
|
1
|
13
|
2
|
2
|
0
|
1
|
2
|
23
|
Jumla
|
5
|
6
|
0
|
18
|
1
|
1
|
189
|
25
|
7
|
0
|
1
|
3
|
256
|
Ikama ya Watumishi wa kada mbalimbali za Afya katika Mkoa haitoshelezi mahitaji yaliyopo katika Vituo vya kutolea huduma za Afya katika ngazi zote. Katika Mkoa kuna jumla ya Watumishi 1848 wa kada mbalimbali za Afya walioajiriwa na Serikali ambapo kada ya Uuguzi ni kada yenye watumishi wengi katika Sekta ya afya Mkoani kwani idadi kubwa ya watumishi wakiwa 749 sawa na 40% ya Watumishi wote na hivyo kuwa ndio kada mhimili katika utoaji wa huduma za Afya katika ngazi ya Msingi. Aidha, kuna Madaktari Bingwa 8, Madakatari (MD) 75, Madaktari wa Meno 1,Madaktari Wasaidizi 15, Wafamasia 5, Wateknolojia dawa 10 katika Mkoa, Hali halisi ya mtawanyo wa baadhi ya Watumishi wa kada za Afya katika vituo vya kutolea huduma ni kama ifuatavyo. Rejea Kiambatisho Na 2(a) hadi 2(h)
Pamoja na kuwepo kwa upungufu wa watumishi huduma za afya zimeendelea kutolewa vizuri ni watumishi waliopo ikiwa pamoja na Mkoa na Halmashauri kuendelea kufanya msawazo wa Watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya kulingana na uzito wa kazi na majukumu katika kuhudumia Wateja kwenye kituo cha kutolea huduma za afya.
3.1 Miundombinu ya Utoaji wa Huduma za Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa inatoa huduma za rufaa kutoka kwenye hospitali za Wilaya na vituo vya kutolea huduma za Afya. Kwa sasa hospitali hii inatoa huduma za Kibingwa zifuatazo: Huduma za uzazi, Watoto, Upasuaji, Kinywa na Meno, huduma za uchunguzi (Radiolojia) na Upasuaji wa Mifupa. Katika kuiwezesha hospitali ya Rufaa ya Mkoa kutoa huduma zilizojitosheleza inatakiwa kuwa na miundombinu ifuatayo:- Jengo la wagonjwa wa nje, Wodi za Magonjwa ya Wanawake, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wodi za Watoto, Jengo la Magonjwa ya dharura, Jengo la huduma za upimaji na uchunguzi, Jengo la Maabara, Jengo la mazoezi ya Viungo, Jengo la Bohari ya Dawa na Vifaa tiba, Jengo la huduma ya kinywa na meno, Jengo la huduma za afya ya macho, Jengo la upasuaji, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa
Jengo kwa ajili ya kufulia, Jengo la kuhifadhia maiti, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Mfumo wa maji safi na maji taka na Jengo la Huduma ya Tiba na Maangalizi (CTC).
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za rufaa ngazi ya Mkoa, miundombinu ifuatayo inakosekana: Wodi za magonjwa ya wanaume, wodi za watoto, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la Bohari ya Dawa na Vifaa tiba, Jengo la huduma ya kinywa na meno, Jengo la huduma za afya ya macho, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko na Jengo la Huduma ya Tiba na Maangalizi (CTC).
Miundombinu inayojengwa kwa sasa ni pamoja: Jengo la wagonjwa Mahututi, jengo la Magonjwa ya Dharura, Bohari ya Dawa na vifaa tiba, Jengo la Maabara, Upasuaji, Wodi za magonjwa ya wanaume na wodi za watoto. Rejea Kiambatisho Na 3: (i)
3.2 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali za Wilaya
Hospitali za Wilaya pamoja na huduma zingine zinazotoa hutumika kama Hospitali za rufaa ngazi ya Wilaya. Kulingana na miongozo hospital ya ngazi ya Wilaya inatakiwa kuwa na Miundombinu ifuatayo:- Jengo la wagonjwa wa nje, Wodi za Magonjwa ya Wanawake, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wodi za Watoto, Jengo la Magonjwa ya dharura, Jengo la huduma za upimaji na uchunguzi, Jengo la Maabara, Jengo la mazoezi ya Viungo, Jengo la Bohari ya Dawa na Vifaa tiba, Jengo la huduma ya kinywa na meno, Jengo la huduma za afya ya macho, Jengo la upasuaji, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa, Jengo kwa ajili ya kufulia, Jengo la kuhifadhia maiti, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Mfumo wa maji safi na maji taka na Jengo la Huduma ya Tiba na Maangalizi (CTC). (Rejea Kiambatisho Na 3: (ii) hadi 3(vii) na kiambatisho 3b (i hadi vii)
3.2.1 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa Hospitali ya Wilaya, miundombinu ifuatayo inakosekana: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la wagonjwa mahututi (ICU), Kiteketeza taka (Incinerator) na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Aidha miundombinu inayojengwa kwa sasa ni pamoja ni Jengo la Mgonjwa ya Dharura.
3.2.3 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Wilaya ya Iramba
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa Hospitali ya Wilaya, miundombinu ifuatayo inakosekana: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la huduma za Kinywa na Meno na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Aidha miundombinu inayojengwa kwa sasa ni pamoja ni Jengo la Mgonjwa ya Dharura, Jengo la wagonjwa mahututi na Maabara.
3.2.3 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Wilaya Ikungi
Hadi kufikia April, 2022 ujenzi wa miundombinu kwa hospitali ya Wilaya ilikuwa haijakamilika. Miundombinu inayoendelea kujengwa kwa sasa ni: Jengo la Utawala, Jengo la wagonjwa wa nje, Jengo la huduma za upimaji na uchunguzi, Jengo la Maabara, Bohari ya Dawa na vifaa tiba, Jengo la huduma za Afya ya Macho, Jengo la kufulia na Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto.
3.2.4 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Wilaya Mkalama
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa Hospitali ya Wilaya, miundombinu ifuatayo inakosekana: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la wagonjwa mahututi (ICU), Jengo la huduma za Kinywa na Meno, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wanawake na Watoto, Jengo la upasuaji, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Miundombinu inayojengwa kwa sasa ni pamoja ni Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la huduma za Afya ya Macho, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wanawake na Watoto.
3.2.5 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Singida
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa Hospitali ya Wilaya, miundombinu ifuatayo inakosekana: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la wagonjwa mahututi, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la wagonjwa mahututi (ICU), Jengo la huduma za Kinywa na Meno, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wanawake na Watoto, Jengo la upasuaji, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Miundombinu inayojengwa kwa sasa ni pamoja ni Jengo la Mgonjwa ya Dharura, na Jengo la huduma za Afya ya Macho, Wodi za Magonjwa ya Wanaume, Wanawake na Watoto.
3.2.6 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika hospitali ya Manispaa ya Singida
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya kwa Hospitali ya Wilaya, miundombinu ifuatayo inakosekana: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la wagonjwa mahututi (ICU), Jengo la Magonjwa ya Mlipuko, jengo la utawala na Kiteketeza taka (High Tech Incinerator).
3.3 Miundombinu ya Kutolea huduma kwenye Vituo vya Afya
Kulingana na mwongozo wa utoaji wa huduma za Afya, Kituo cha Afya kinatakiwa kuwa na Miundombinu ifuatayo: Jengo la wagonjwa wa nje, Jengo la huduma za Uzazi na Mtoto, Jengo la Maabara, Jengo la kufulia, Wodi za Magonjwa ya Wanawake, Wanaume na Watoto, Jengo la upasuaji, Jengo la mionzi, Jengo la kuhifadhia maiti, Kiteketeza taka na Miundombinu ya Maji safi na Maji taka. Rejea Kiambatisho Na 3: (viii hadi 3 xxv) na kiambatisho 3b (i hadi vii)
3.3.1 Miundombinu ya Kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Manispaa ya Singida
Katika miundombinu inayohitajika ili kuwezesha utoaji wa huduma za Afya ngazi ya Kituo, kituo cha Afya Sokoine kina upungufu wa miundombinu ifuatayo: - Wodi za magonjwa ya wanaume na watoto, Jengo la huduma za uchunguzi na Jiko la kupikia wagonjwa. Aidha Miundombinu ya jengo la huduma za uchunguzi linaendelea kujengwa.
Kituo cha Afya Mtisi kina jengo la wagonjwa wa nje ambalo linatumika kutolea huduma zote za Afya kwa wagonjwa wa nje.
3.3.2 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Singida
Kituo cha Afya Mgori kina miundombinu yote inayohitajika kulingana na mwongozo isipokuwa: Jengo la huduma za uchunguzi (X-ray na Ultrasound), Jengo la kutunzia Dawa na vifaa tiba, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula.
Kituo cha Afya Msange kina upungufu wa miundombinu ifuatayo; Wodi za magonjwa ya wanaume na watoto, jengo la huduma za Kiuchunguzi (X-ray na Ultrasound), Kiteketeza taka, Jengo la kutunzia Dawa na Vifaa tiba na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Kituo cha Afya Ilongero kina upungufu wa miundombinu ifuatayo; Jengo la huduma za Kiuchunguzi (X-ray na Ultrasound), Kiteketeza taka, Jengo la kutunzia Dawa na Vifaa tiba, Jengo la Upasuaji, Jengo la kufulia, Jengo la kuhifadhia maiti na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
3.3.3 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
Kituo cha Afya Kinyambuli, miundombinu inayokosekana kwa ajili ya utoaji huduma za Afya ngazi ya kituo ni; Wodi za magonjwa ya wanaume na watoto, Jengo la huduma za uchunguzi (X-ray na Ultrasound), Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Kituo cha Afya Kinyangiri kati ya majengo yote yanayohitajika kwa ngazi ya kituo cha Afya kina majengo yafuatayo: Jengo la wagonjwa wa nje, Wodi ya magonjwa ya wanawake na Kiteketeza taka.
Kituo cha Afya Mkalama kati ya majengo yote yanayohitajika kwa ngazi ya kituo cha Afya kina majengo yafuatayo: Jengo la wagonjwa wa nje, Wodi ya magonjwa ya wanawake na Kiteketeza taka.
3.3.4 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni
Kituo cha Afya Nkonko kina upungufu wa miundombinu ifuatayo: Jengo huduma za uchunguzi, Jengo la kutunzia Dawa na Vifaa tiba, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Aidha kituo cha Afya Kintinku kina upungufu wa miundombinu ifuatayo: Jengo huduma za uchunguzi, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
3.3.5 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.
Kwa kituo cha Afya Itigi, miundombinu inayokosekana kulingana na mahitaji ni: Jengo la huduma za uchunguzi, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Kituo cha Afya Mitundu kina Jengo la wagonjwa wa nje linalotumika kutoa huduma zote, Hata hivyo Miundombinu ifuatayo inaendelea kujengwa; Jengo la Maabara, Jengo la huduma ya Magonjwa ya wanawake na upasuaji, Jengo la kufulia na Jengo la kuhifadhia maiti.
3.3.6 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Kituo cha Afya Ndago, miundombinu inayokosekana kulingana na mahitaji ni: Jengo la huduma za uchunguzi (X-ray na Ultrasound), Kiteketeza taka, Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa. Chumba cha kuhifadhia maiti kinaendelea kujengwa.
Kituo cha Afya Kinampanda kinakosa miundombinu ifuatayo kulingana na mahitaji: Jengo la wagonjwa wa nje, Wodi za magonjwa ya wanaume na watoto, Jengo la huduma za uchunguzi na jiko la kupikia chakula cha wagonjwa.
Kituo cha Afya Kyengege kina Jengo la wagonjwa wa nje linalotumika kutolea huduma zote kwa wagonjwa wa nje, Kiteketeza taka na Mfumo ya Maji taka na maji safi.
Aidha Kituo cha Afya Mgongo, miundombinu inayokosekana kati ya inayohitajika ni: Jengo la uchunguzi, Jengo la Maabara, Jengo la kutunzia Dawa na Vifaa tiba, Jengo la kuhifadhia maiti, Jengo la kufulia na Kiteketeza taka.
3.3.7 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya Vituo vya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Kituo cha Afya Ikungi, miundombinu inayokosekana kulingana na mahitaji ni: Jengo la huduma za uchunguzi (X-ray na Ultrasound), Kiteketeza taka chenye sifa ngazi ya kituo, Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa, Jengo la kuhifadhia Dawa na vifaa tiba, Jengo la kufulia, Jengo la kuhifadhia.
Kituo cha Afya Ihanja, miundombinu inayokosekana kulingana na mahitaji ni: Jengo la kutunzia Dawa na vifaa tiba na Jiko la kupikia chakula cha wagonjwa. Aidha Jengo la huduma za uchunguzi (X-ray na Ultrasound) linaendelea kujengwa.
Kituo cha Afya Sepuka miundombinu inayokosekana kulingana na mahitaji ni: Jengo la huduma za Kiuchunguzi, Kiteketeza taka na Jiko la kupikia chakula cha Wagonjwa. Chumba cha upasuaji kipo lakini hakitumiki kutokana na kutokuwa na vifaa.
3.4 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya Zahanati
Huduma zinazotolewa ngazi ya zahanati kulingana na mwongozo ni: Huduma za wagonjwa wa nje, Afya ya uzazi na mtoto, chanjo na Maabara. Miundombinu inayotakiwa ili kuwezesha utoaji wa huduma hizo ni: Jengo la wagonjwa wa nje, Stoo ya kutunzia Dawa na vifaa tiba, Maabara na Jengo kwa ajili ya Afya ya Uzazi na Mtoto.
Kwa sasa huduma kwenye zahanati nyingi bado zinatolewa ndani ya Jengo moja ambalo linakuwa na huduma zote zinazotakiwa kutolewa ngazi ya zahanati. Aidha kuna baadhi ya zahanati ambazo zimeanza kujengewa miundombinu itakayowezesha kuwepo kwa mazingira mazuri ya utoaji wa huduma. Miundombinu inayoongezwa kwenye zahanati hizo ikiwa na majengo yanayojitegemea ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Jengo la Maabara, Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto, na Kiteketeza taka (De Montfort Incinerator). Baada ya miundombinu inayoongezwa kukamilika zahanati hizi zitakuwa na uwezo wa kutoa huduma kama zinazotolewa na vituo vya Afya, hivyo zitatakiwa kuhuishwa usajili wake kufikia ngazi ya kituo cha Afya. Rejea kiambatisho (3b i hadi vii)
3.4.1 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Manispaa ya Singida
Kwa Manispaa ya Singida, zahanati zote zinatoa huduma za Afya ndani ya Jengo moja. Zahanati hizo pia vina vichomea taka ambavyo havina sifa. Aidha mfumo wa maji safi na maji taka una jengwa kwenye zahanati ya Unyambwa.
3.4.2 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Singida
Halmashauri ya Wilaya ya Singida, huduma za Afya ngazi ya zahanati zinatolewa ndani ya jengo moja. Miundombinu mingine inayopatikana kwenye zahanati ni pamoja na: Vyoo vya watoa huduma, vyoo vya wagonjwa, Kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.
3.4.3 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Mkalama
Zahanati za Ilunda na Gumanga zinajengewa miundombinu itakayowezesha kutoa huduma kamili za dharura na upasuaji. Kwa sasa miundombinu inayojengwa kwenye zahanati ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Maabara, Kiteketeza taka (De Montfort Incinerator), na Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto.
3.4.4 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Manyoni.
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, huduma za Afya ngazi ya zahanati zinatolewa ndani ya jengo moja. Miundombinu mingine inayopatikana kwenye zahanati ni pamoja na: Vyoo vya watoa huduma, vyoo vya wagonjwa, Kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.
Zahanati za Chibumagwa na Sanza zinajengewa miundombinu itakayowezesha kutoa huduma kamili za dharura na upasuaji. Kwa sasa miundombinu inayojengwa kwenye zahanati ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Maabara, Kiteketeza taka (De Montfort Incinerator), na Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto. Aidha kwa zahanati ya Chibumagwa majengo yako kwenye hatua ya umaliziaji.
3.4.5 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Itigi.
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, huduma za Afya ngazi ya zahanati zinatolewa ndani ya jengo moja. Miundombinu mingine inayopatikana kwenye zahanati ni pamoja na: Vyoo vya watoa huduma, vyoo vya wagonjwa, Kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.
Zahanati za Rungwa inajengewa miundombinu itakayowezesha kutoa huduma kamili za dharura na upasuaji. Kwa sasa miundombinu inayojengwa kwenye zahanati hiyo ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Maabara, Jengo la upasuaji na Jengo la Afya ya Uzazi na Mtoto.
3.4.6 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Iramba.
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, huduma za Afya ngazi ya zahanati zinatolewa ndani ya jengo moja. Miundombinu mingine inayopatikana kwenye zahanati ni pamoja na: Vyoo vya watoa huduma, vyoo vya wagonjwa, Kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.
Zahanati za Mwanduigembe, Mtekente, Mtoa, Tyegelo, Shelui na Kisiriri zinajengewa miundombinu itakayowezesha kutoa huduma kamili za dharura na upasuaji. Kwa sasa miundombinu inayojengwa kwenye zahanati hizo ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Maabara, Kiteketeza taka (De Montfort Incinerator), na Jengo la Afya ya Uzazi na Upasuaji.
3.4.7 Miundombinu ya kutolea huduma za Afya ngazi ya zahanati Halmashauri ya Ikungi.
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, huduma za Afya ngazi ya zahanati zinatolewa ndani ya jengo moja. Miundombinu mingine inayopatikana kwenye zahanati ni pamoja na: Vyoo vya watoa huduma, vyoo vya wagonjwa, Kichomea taka na shimo la kutupia kondo la nyuma.
Zahanati za Iyumbu, Ntuntu, Misughaa na Iglansoni zinajengewa miundombinu itakayowezesha kutoa huduma kamili za dharura na upasuaji. Kwa sasa miundombinu inayojengwa kwenye zahanati hizo ni pamoja na: Jengo la wagonjwa wa nje, Maabara, Kiteketeza taka (De Montfort Incinerator), na Jengo la Afya ya Uzazi na Upasuaji
4.0 UPATIKANAJI WA DAWA, VIFAA TIBA, NA VITENDANISHI
Upatikanaji wa Dawa, vifaa tiba na vitendanishi vyenye ubora, kwa kiasi sahihi, kwenye kituo sahihi, kwa wakati sahihi na kwa gharama sahihi ni moja ya kiashiria cha ubora wa huduma zinazotolewa kwenye ngazi zote za vituo vya kutolea huduma za Afya. Katika kuhakikisha huduma za Bidhaa za Afya zinaboreshwa kwenye vituo, Serikali imeendelea kuwekeza kwenye eneo hili kwa kuweka mikakati mbalimbali ikiwa ni Pamoja kuongeza fedha za ruzuku kwa ajili ya kununulia bidhaa za Afya, kusimika mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya usimamizi wa bidhaa za Afya, kutoa mafunzo ya usimamizi wa bidhaa za Afya kwa watoa huduma za Afya lengo ni kuhakikisha bidhaa za Afya zinapatikana kwa wakati wote kulingana na huduma zinazotolewa kwenye ngazi husika.
4.1 Hali halisi ya upatikanaji wa Dawa, Vifaa tiba, na vitendanishi hadi kufikia April, 2022
Hadi kufikia April, 2022 wastani wa upatikanaji wa Bidhaa za Afya Muhimu (Dawa, vifaa tiba na vitendanishi) kwa Mkoa ni 87.7%. Aidha upatikanaji wa Dawa, vifaa tiba na vitendanishi ulikuwa wa juu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Singida 90.7% na ulikuwa chini kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba 85.7% kwa taarifa iliyotolewa April, 2022. (Rejea Kiambatisho Na 4A hadi 4H)
5.0 HALI YA HUDUMA ZA TIBA
Huduma za Tiba katika Mkoa zinatolewa na Vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyopo ngazi ya Mkoa kuanzia ngazi ya Kliniki, Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Rejea Kiambatisho Na: 5A
5.1 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huduma za Tiba za Kibingwa zinatolewa isipokuwa huduma za Kibingwa za Magonjwa ya ndani, Macho, Masikio, Koo na Pua, Upasuaji wa Watoto, mfumo wa Mkojo, huduma za Wagonjwa mahututi na dharura, upimaji wa CT Scan, MRI, ECHO.
Hali halisi ya utoaji wa huduma za tiba ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Huduma ya upimaji na uchunguzi
Huduma za dawa
Huduma ya mazoezi ya Viungo (Phyisiotherapy)
Huduma ya Uuguzi na Ukunga
Huduma za Afya ya uzazi Salama
Huduma za Kliniki za Kibingwa katika Hospitali za Halmashauri
Huduma za Kliniki mbalimbali za Afya (Afya ya Macho, Kisukari, Kifua Kikuu, UKUMWI)
Huduma za kupokea na kutoa rufaa za Wagonjwa
5.2 Hospitali za Halmashauri
Katika Hospitali za halmashauri za Iramba na Manyoni huduma muhimu za Tiba zinapatikana isipokuwa huduma za Kibingwa, huduma za Wagonjwa mahututi na dharura. Hali halisi ya utoaji wa huduma Tiba katika Hospiatli za Iramba na Manyoni ni kama ifuatavyo
Huduma ya upimaji na uchunguzi
Huduma ya Uuguzi na Ukunga
Huduma za dawa
Huduma za Kliniki mbalimbali za Afya (RCH, Kisukari, Kifua Kikuu, UKUMWI)
Huduma za kupokea na kutoa rufaa za Wagonjwa
Huduma za Kliniki mbalimbali za Afya (Afya ya Macho, Kisukari, Kifua Kikuu, UKUMWI)
Huduma za kupokea na kutoa rufaa za Wagonjwa
Aidha, katika Hospitali mpya za Halmashauri huduma za Tiba zinazotolewa ni kwa Wagonjwa wa Nje na Kliniki za RCH kwa sababu miondombinu inaendelea kujengwa na ununuzi wa vifaa tiba.
5.3 Huduma za Tiba ngazi ya Vituo vya Afya
Hali halisi ya utoaji wa huduma Tiba katika Vituo vya Afya ni kama ifuatavyo
Huduma ya upimaji na uchunguzi
Huduma za dawa
Huduma za afya ya Uzazi na Mtoto (RCH)
Huduma shirikishi za Mkoba
Huduma za kupokea na kutoa rufaa za Wagonjwa
5.4 Huduma za Tiba ngazi ya Zahanati
Hali halisi ya utoaji wa huduma Tiba katika Zahanati ni kama ifuatavyo
Huduma ya upimaji
Huduma za dawa
Huduma za afya ya Uzazi na Mtoto (RCH)
Huduma shirikishi za Mkoba
Huduma ya Uuguzi na Ukunga
Huduma rufaa za Wagonjwa
Aidha pamoja na utoaji wa huduma za tiba kuna mambo mbalimbali yanayoathiri huduma hizo kama vile;
5.5 Hali halisi huduma za tiba kinywa na meno katika halmashauri.
Muongozo wa afya ya kinywa na meno wa 2020 wa utoaji wa huduma za afya ya kinywa na meno kuwa jumuishi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima. Lengo kuu likiwa ni huduma za afya ya kinywa na meno inatolewa kuanzia ngazi ya hospitali za mikoa, halmashauri na baadhi ya vituo vya afya vya kimkakati.
Kwa mkoa wa Singida utekelezaji wa muongozo huu bado hata robo hatujaweza kuutekeleza kwa kuwa katika ngazi ya halmashauri, huduma zinatolewa katika halmashauri tatu (3) sawa na 57% kati ya halmashauri saba (7) zinazounda mkoa wa Singida. Sababu kubwa inayosababisha baadhi ya wilaya kutokutoa huduma hizi ni kutokuwepo kwa miundombinu, wataalam wa eneo husika na vifaa vya matibabu.
Huduma zinazotolewa katika vituo hivi ni matibabu ya dharura ya maumivu (64 %), uzibaji wa meno (11.4%), huduma za kuondoa maumivu bila kung’oa (0%) upasuaji mdogo (0.2%) na utengenezaji wa meno ya bandia (0%). Huduma nyingine kama usafishaji wa meno (scalling), urekebishaji wa taya na uso, upasuaji mkubwa hazifanyiki kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu na wataalam katika maeneo hayo. Rejea Kiambatisho 5C
6.0 UDHIBITI WA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA, MLIPUKO NA YASIYOKUWA YA KUAMBUKIZWA
6.1 Hali ya maambukizi ya UKIMWI
Kiwango cha maambukizi ya UKIMWI Mkoa wa Singida ni asilimia 3.6% chini ya maambukizi ya Taifa ambayo ni 4.7%. Waviu waliogundulika na kuwepo kwenye dawa jumla yao ni 24,636 ambayo ni asilimia 0.01% ya waviu wote nchini.katika Mkoa asilimia ya waviu wanaojua hali zao ni 86%, wanaotumia dawa za ARV ni 99.5% na makali ya VVU yamefubaa kwa asilimia 97% hivyo kwenda sawa na mpango wa 95%,95%,95% wa kupambana na virusi vya UKIMWI nchini.
Mkoa una jumla ya vituo 101 vinavyotoa huduma za uangalizi na matunzo ya waviu kati ya vituo 256 vya mkoa wa Singida.Hili ni ongezeko la vituo 7 vya kutolea huduma ukilinganisha na vituo 94 kwa mwaka 2020.huduma mkoba kwa waviu nje ya vituo hivi imeendelea kutolewa kuwafikia waviu wote kwenye maeneo yao. Kati ya vituo vyote 101 ni vituo 94 tu ndivyo vinasaidiwa na Mdau (USAID-AFYA YANGU) katika shughuli mbali mbali za kliniki ya VVU.
Katika Kipindi cha Januari 2022 hadi June 2022 jumla ya Watu 46,021 walipimwa na watu 1,369 kukutwa kuwa na maabukizi mapya. Kati ya waliokutwa na maabukizi mapya jumla ya waviu 1540 walianzishiwa huduma ya dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV) ukilinganisha na waviu 778 walioanzishiwa huduma katika robo ya mwisho wa mwaka 2021. Waviu waliogundulika na kuwepo kwenye dawa jumla yao ni 24,636 ukilinganisha na waviu 24,021 mwaka 2021.
Hali ya Maabukizi ya Virusi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto yameendelea kupungua kila mwaka. Mwaka 2020 ilikuwa 0.75% na 2021 ikashuka kufikia 0.73% huku mwaka huu ikitegemewa kushuka Zaidi.
6.2 Kifua Kikua na Ukoma
6.2.1 Hali halisi ya utoaji wa huduma za Kifua Kikuu
Mkoa Singida kupitia Idara ya Afya, umeendelea kutoa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma ikiwa ni pamoja na uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu wakiwemo wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu na watoto chini ya miaka 15.
Huduma za Kifua Kikuu zimeendelea kutolewa katika vituo vya kutolea huduma na kwa njia ya Mkoba na Kliniki Tembezi kwenye Maeneo ambayo hakuna vituo vya kutolea huduma. Hali kadhalika, chanjo ya kuzuia Kifua Kikuu kwa watoto (BCG) inaendlea kutolewa kwa watoto wote.
6.3 UKOMA
6.4 MALARIA
Hali halisi ya utoaji wa huduma za Malaria
Katika kutekeleza mpango Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti ugonjwa wa Malaria wa mwaka 2021-2025 unaolenga kuondoa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria. Kwa sasa kiwango cha Maambukizi ya Malaria Mkoa wa Singida 2.3%, Kiwango hiki ni kidogo ukilinganisha na wastani wa kitaifa (asilimia 7.3) wa maambukizi ya malaria. Kwa Mkoa kiwango kikubwa cha malaria kipo Halmashauri ya wilaya ya Itigi (asilimia 7.7) na kiwango kidogo cha malaria kipo katika Halmashauri ya wilaya ya Singida (asilimia 0.3). Kwa sasa huduma za upimaji wa malaria zinapatikana bila malipo kwenye vituo vyote vya umma kwa kutumia kipimo cha haraka cha Malaria (mRDT). Wastani wa upatikanaji wa dawa na vitendanishi vya Malaria ni wa kuridhisha kwa asilimia 93.5 katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya hadi kufikia 30 Aprili 2022 Kwa kipindi cha Januari hadi Aprili, 2022 jumla ya wagonjwa wateja 92,751 walipimwa malaria ambapo kati yao 6,826 Waligundulika kuwa na vimelea vya malaria na walipatiwa matibabu. Rejea Kiambatisho Na. 6 (iii)
Huduma ya chandarua Kliniki inapatikana kwenye vituo vyote vya Umma na Binafsi vinavyotoa huduma za RCH vinatoa Vyandarua vyenye Viuatilifu vya muda mrefu kwa akina mama wajawazito hudhurio la kwanza na kwa watoto wenye umri wa kupata chanjo ya kwanza ya Surua. Kipindi cha Aprili, 2022 vyandarua vyenye viuatilifu 23,916 (95%) Viligawiwa kwa wajawazito na vyandarua 18,421 (94%) kwa watoto chini ya mwaka 1. Rejea Kiambatisho Na. 6 (iv)
Halmashauri za Iramba, Itigi, Manyoni na Manispaa ya Singida zimeweza kuwagawia kina mama wajawazito wote walihudhuria Kliniki hudhurio la kwanza na Halmashauri za Ikungi na Manispaa ya Singida zimeweza kuwagawia watoto wote waliopata chanjo ya Surua Rubella ya kwanza (MR1) kwa kuwa Halmashauri nyingine hazijaweza kugawa vyandarua kwa walengwa wote imepelekea Mkoa kugawa vyandarua kwa akina mama wajawazito kwa 96% na watoto 98%
6.5 UDHIBITI WA MAGONJWA YA MLIPUKO
Mkoa unaendelea ya kutekeleza Afua mbalimbali za udhibiti wa magonjwa ya mlipuko na kuambukizwa ambapo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 Mkoa umepata mlipuko wa ugonjwa mmoja (UVIKO-19) kati ya magonjwa 35 yanayotolewa taarifa kwa siku au wiki kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonja ya mlipuko (IDSR)
6.6 UGONJWA WA VIRUSI VYA KORONA (UVIKO-19)
Mkoa unaendelea kutoa elimu na tahadhari za kuchukua dhidi ya Maambukizi ya UVIKO-19 ikiwa pamoja na kuzihimiza mamlaka za Halmashauri kufanya ufuatiliaji wa karibu kwenye jamii juu ya ugonjwa huu pamoja kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19. Kwa kipindi cha kuanzia 1 Mei hadi 31 Mei, 2022 kuna idadi ya wagonjwa 10 waliothibitika na kati yao mmoja (1) ni mtumishi wa Afya. Hakuna kisa cha kifo kilichoripotiwa na hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyelazwa.
6.7 MAGONJWA YASIO YA AMBUKIZA (MYA)
Hali halisi ya utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa MYA
Mkoa una jumla ya vituo 31 vinavyotoa huduma za dharura na kliniki za magonjwa yasio ya ambukiza. Mkoa unategemea kuanzisha huduma za kupima na kutibu MYA kutumia mionzi CT- SCAN, MRI, Miyonzi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa. Vifaa hivi vitaongeza wigo wa kufanya uchunguzi wa kina kwa wagonjwa wa MYA. Hali kadhalika Hospitali za wilaya zote zinategemea kuanzisha kliniki za ugonjwa wa selimundo. Hatua hizi ni katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa kukinga na kupunguza MYA nchini wa mwaka 2021 – 2026 unaoelekeza kuelimisha jamii, kuibua, kuwatibu, na kuwafuatilia wagonjwa wa magonjwa yasio ya kuambukiza.
Kuanzia Januari hadi Desemba 2021 Jumla ya wagonjwa wa MYA 107,239 waliibuliwa na kuanzishiwa tiba katika idara ya wagonjwa wa nje. Kati yao wagonjwa wa shinikizo la damu ni 19,729, kisukari 9,138, magonjwa mengine 78,372. Wagonjwa wa ndani walikuwa 46,960(Shinikizo la damu 205, ugonjwa wa moyo 762, kisukari 750, magonjwa mengine 45243) walihudumiwa. Jumla ya vifo 1696 vilitokana na MYA. Halikadhalika kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2022 jumla ya wagonjwa 12,758 wa MYA walipewa huduma katika vituo vya afya, 4725 wakiwa wagonjwa wa kisukari. Rejea Kiambatisho Na 6 (v)
6.8 UDHIBITI WA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
Mkoa unaenendelea kutakaleza program ya utoaji wa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa Hayapewi kipaumbele kwa watoto wenye umri wa kuwa shule za Msingi ambayo inahusisha dawa za Kichocho na dawa ya Minyoo ya Tumbo. Kwa mwaka 2021 Jumla ya watoto 417642 (94.8%) kati ya watoto 440434 walipatiwa dawa za kingatiba ya minyoo ya tumbo na kichocho. Rejea Kiambatisho Na 6 (vi)
7.0 HALI HALISI YA UTEKELEZAJI AFYA YA UZAZI, MTOTO NA VIJANA
Mkoa wa Singida unalenga kuboresha huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto kupitia idara zake za RCH. Uwekezaji katika eneo hili na mikakati mbalimbali inawekwa na Mkoa katika kupunguza magonjwa na vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto chini ya miaka mitano na vijana. Kwa kuzingatia "Malengo ya Maendeleo Endelevu" yanayohusiana na afya lengo namba 3, namba 5, kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na lengo namba 17, kuhusu ushirikiano; Mkoa umeweka mkazo katika utoaji wa huduma bora za Afya ya Uzazi kwa usawa na wakunga wenye ujuzi katika mazingira wezeshi na kwa kuiunganisha jamii na kituo cha huduma.
7.1 Huduma Rafiki za Kijamii na Afya ya Uzazi kwa Vijana:
Vituo vya huduma rafiki kwa Vijana vimeongezeka kutoka vituo 97 (42%) mwaka 2020 hadi kufikia vituo 221 (88.4%) mwaka 2021. Aidha, kuna ongezeko la huduma ya mkoba ya Elimu ya Afya ya uzazi, Ushauri, Stadi za Maisha na Habari katika Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo, Kwenye Jamii na kupitia vyombo vya habari kutoka asilimia 43 hadi kufikia asilimia 84. Huduma hii imesaidia kupunguza kiwango cha mimba na uzazi kwa Vijana kutoka asilimia 12.2(2020) hadi 11.4(2021). Rejea Kiambatisho Na 7 (i)
6.2 Huduma za Uzazi wa Mpango:
Kati ya vituo 256, ni vituo 233 sawa na asilimia 91 vinatoa huduma ya uzazi wa mpango ambapo kiwango cha wateja wapya kimeongezeka kutoka 34% (2020) hadi 35% (2021) na wateja wa njia za muda mrefu pia kimeongezeka kutoka 37.3% (2020) hadi 56.4 % (2021). Aidha, Uzazi wa Mpango baada ya mama kujifungua (Postpartum Family Planning) unatolewa na watoa huduma 32 tu kutoka katika vituo 24 tu (10.3%) kati ya vituo 233 vinavyotoa huduma ya Uzazi wa Mpango. Huduma inajumuisha elimu ya uzazi salama ndani ya kituo na huduma za mkoba kwa kushirikiana na wadau. Rejea Kiambatisho Na: 7 (ii)
6.3 Afya ya Mama
6.4 Afya ya Mtoto na huduma ya Watoto wachanga:
Kiwango cha vifo vya watoto wachanga vimepungua kutoka 12.8 (2020) hadi 10.8 (2021) kati ya watoto 1000 waliozaliwa hai na vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kufikia 7(2020) kutoka 9.2(2021) kati ya vizazi hai 1000 (Rejea Kiambatisho Na 7(iv) na 7 (v)). (ripoti ya RCH). Aidha, kiwango cha vituo vinavyotoa huduma kwa watoto wachanga sana (NICU) kimefikia asilimia 36.3. Rejea Kiambatisho Na 7 (vi)
6.5 Saratani ya Mlango wa Kizazi:
Kipindi cha Jan-Mac, 2022 kiwango kimefikia asilimia 86 kutoka 28.9 ya wanawake walengwa wenye miaka 30-50 na wanawake 30 walidhaniwa kuwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo walipewa rufaa kwenda Ocean Road na Bugando kwa matibabu zaidi. Huduma za uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi hufanyika katika vituo 33(13.2%) kati ya vituo vyote 250 vinavyotoa Afya ya Uzazi na Mtoto. (Rejea Kimbatisho Na )
Masuala mtambuka katika huduma za Afya ya Uzazi
Kiwango cha vijiji vyenye watumishi 2 wa afya ya jamii wanaotoa huduma ya uzazi na mtoto na lishe katika ngazi ya jamii kimeongezeka kutoka 75% hadi 89%. Ushiriki mdogo wa jamii katika afya ya uzazi na mtoto kupitia “Jiongeze Tuwavusha Salama”.
8.0 HUDUMA ZA CHANJO
Kwa mwaka 2021 Mkoa ulitoa huduma ya chanjo kwa watoto 69,782 sawa na 111.5% ya watoto 62,605 lengwa. Aidha, Hali ya utoaji wa huduma za chanjo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2022 ni watoto 16,999 sawa 105.9% ya watoto 16,048 waliotakiwa kupatiwa chanjo Kimkoa. Lengo kuu la Mkoa ni kuwakinga watoto dhidi ya Magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kama Kifua Kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Surua, Rubella, Polio, Pepopunda, Homa ya Ini, Homa ya Uti wa Mgongo, Kuhara, Kichomi na Saratani ya Mlango wa kizazi.
Aidha, upatikanaji wa chanjo ya Surua kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 ni 79%, kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2022 chanjo ya Surua ni 80% kutokana na kutokupatikana kwa chanjo za kutosha ngazi ya Taifa, na upatikanaji wa chanjo dhidi ya Kifua Kikuu kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 ni 155% ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2022 watoto waliopatiwa chanjo ya BCG ni 71% kutokana na ukosefu mkubwa wa Mabomba ya Sindano ya BCG (Rejea Kiambatisho Na 8 (i) . Muitikio wa chanjo ya wasichana dhidi ya Kansa la mlango ya mlango wa kizazi (HPV) wenye umri wa miaka 14 kwa chanjo ya Pili kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 ni 82% na kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2022 kwa chanjo ya HPV ya dozi ya Pili ni 52%.
Kwa mwaka 2020 hadi 2021 huduma za chanjo zimetolewa katika vituo 218 sawa na 88% ya vituo 246, ambapo kwa mwaka 2022 Mkoa wa Singida umefanikiwa kusajili vituo vipya 12 kwa ajili ya utoaji wa huduma za chanjo kwa wananchi. Kati ya vituo 256 kwasasa vinavyotoa huduma mbalimbali za Afya ni vituo 230 sawa na 90% ya vituo vinavyotoa huduma za chanjo kwa watoto na watu wazima.
8.1 HALI HALISI YA UTOAJI WA HUDUMA YA MKOBA
Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021, Hali ya Utoaji wa huduma za Mkoba ni 57% na kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2022,hali halisi ya utoaji wa Huduma ya mkoba ni 77%. Aidha, kwa kipindi cha Mwaka Jana ukilinganisha na sasa hivi Mkoa umeongezeka kwa 20% ya utoaji wa huduma ya Mkoba. Rejea Kiambatisho Na 8 (ii)
8.2 CHANJO YA UVIKO-19
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa 31 nchini ambao ulianza kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 tarehe 4 Agosti, 2021 katika vituo 232. Mkoa ushatoa chanjo kwa watu 116,497 (Wanawake 66,819 na Wanaume 49,678) sawa na 13% ya watu 892,060 wenye umri wa miaka 18+ na kuendelea. Aidha, kufikia 31 Mei, 2022 watu 73,289 sawa 8% ya watu 892,060 waliokamilisha kinga kamili dhidi ya UVIKO-19 kimkoa. (Rejea Kiambatisho Na 8 (iii)
9.0 HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA LISHE KATIKA MKOA.
Lishe bora huimarisha kinga ya mwili na huongeza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi ya magonjwa mbalimbali. Utafiti wa Kitaifa wa masuala ya Lishe (TNNS 2018) ulionyesha kuwa; Asilimia 45.6 ya watoto chini ya miaka 5 katika Mkoa wa Singida wana hali nzuri ya lishe, asilimia 29 wana udumavu, asilimia 5.2 wana ukondefu, asilimia 18 wana uzito pungufu na asilimia 2.2 wana uzito mkubwa. Aidha kwa upande wa wanawake walio katika umri wa kuzaa; asilimia 68.1 wana hali nzuri ya lishe, asilimia 10.8 wana ukondefu na asilimia 21.1 wana uzito mkubwa. (Rejea Kiambatisho Na: 9
Aidha,vituo vyote vya kutolea huduma za Afya vinafanya tathmini ya hali ya lishe kwa watoto. Vituo 164 kati ya 256 sawa na asilimia 64 vinatoa huduma na matibabu ya utapiamlo, mfumo wa rufaa hutumika pindi Kituo kisichotoa huduma hiyo kinapopata mgonjwa wa utapiamlo. Mkoa una kituo maalum cha Kuhudumia watoto wenye utapiamlo, kwa kipindi cha Oktoba 2020 hadi Juni 2022 jumla ya watoto 204 wenye utapiamlo wamehudumiwa kwenye kituo hicho. Ili kuimarisha uhakika wa chakula katika ngazi ya kaya, uhamasishaji wa upandaji na matumizi wa mazao yaliyoongezwa virutubishi (mahindi lishe, viazi lishe na maharage Lishe) pamoja na ulimaji wa mbogamboga inatolewa katika jamii. Jumla ya Shule 55 (Ikungi-19, Iramba-7, Itigi -4, Singida DC 19 na Mkalama 6) zimepata mbegu za maharage Lishe.
Elimu ya lishe inatolewa kupitia majukwaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia redio standard, kufikisha jumbe tofauti tofauti za lishe; kufanya mapishi darasa kwenye ngazi ya kituo na jamii ili kufikisha ujumbe kwa makundi mbalimbali yaliopo kwenye jamii juu ya ya umuhimu wa lishe bora. Aidha vijiji pia huadhimisha siku ya afya na lishe kila robo na kwa kipindi cha Januari-Machi 2022, vijiji/ mitaa 383 (74.8%) kati ya 512 viliadhimisha siku ya afya na Lishe ya kijiji.
10.0 HALI YA UJENZI NA MATUMIZI YA VYOO KATIKA KAYA KUFIKIA MACHI 2022
Mkoa kupitia Halmashauri unaendelea na uhamasishaji wa ujenzi na matumizi ya vyoo bora kwa kila kaya na taasisi katika jamii ikiwa ni Pamoja na kuhamasisha jamii kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni ili kupunguza Magonjwa ya kuambukiza ambayo yanaweza kuathiri jamii kama Kipindupindu, Kuhara, Kuhara damu, Homa ya Matumbo, Minyoo na Trakoma. Hadi kufikia Machi, 2022, kaya zenye vyoo katika Mkoa ni 329,818 (99.2%) na kaya ambazo hazina vyoo ni 2,656 (0.8%) na kaya zenye vifaa vya kunawia mikono nje ya choo ni 70,630 (21.2%). Hali ya uwepo wa vyoo kwa kila Halmashauri inaonekana kwenye kiambatisho Na: 10 (i). Aidha kiwango cha kaya zenye vyoo kimeongezeka kutoka asilimia 79.9 (2015) hadi asilimia 99.2 (2022) na kaya zenye vyoo bora zimeongezeka kutoka asilimia 27.6 (2015) hadi asilimia 62.1 (2022).
Aidha, Hali ya Upatikanaji miundombinu ya udhibiti wa taka na maji safi katika vituo vya kutolea huduma za Afya ni; vichomea taka vinavyokubalika katika Mkoa ni asilimia 4, mashimo ya kutupia kondo la nyuma ni asilimia 63 na upatikanaji wa vifaa vya kudumu vya kunawia mikono katika vituo ni asilimia 32 na vituo vilivyounganishwa katika mtandao wa maji ya bomba ni asilimia 33. Halmashauri za Wilaya zinaendelea kutekeleza mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji na usafi wa mazingira katika vituo 37 kwa mwaka 2021/2022. Rejea Kiambatisho Na 10( iii)
Hali ya Uwepo wa Vyoo katika Shule si ya kuridhisha, Mahitaji ya matundu ya vyoo kwa wanafunzi katika Shule 659 ni 19,198 na hali halisi ya idadi ya matundu ya vyoo vilivyopo ni 8,275 (43%). Aidha kwa upande wa vyoo vya walimu, mahitaji ni 1212 na uhalisia ni vyoo 658 (54%) kama inavyoonekana kwenye Kiambatisho Na 10 (ii). Mkoa unaendelea kusimamia mradi wa uboreshaji wa miundo mbinu ya maji na Vyoo kwenye Shule za Msingi, ambapo kwa mwaka 2021/2022, jumla ya shule 4 kutoka Halmashauri za Manyoni zimepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo na miundombinu ya maji na kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shule 73 zinatarajiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo na miundo mbinu ya maji. Aidha kwa upande wa maji safi na salama, shule 315 kati ya 658 zina vyanzo vya maji safi na salama na shule 169 (26%) zinatoa chakula cha mchana mashuleni. Rejea Kiambatisho Na 10 ( iv)
11.0 HALI YA UTEKELEZAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII, BIMA YA AFYA NA MAKUSANYO YA PAPO KWA PAPO
Mkoa wa Singida ni miongoni mwa Mikoa ambayo Wananchi wake wanaendelea kuitikia vizuri kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) kwa kiwango cha uchangijaji wa wanachama kwa kiasi cha (shilling 30,000 kwa kila kaya) na kupata huduma za Afya kwenye vituo vya serikali na binafsi kwa wanachama waliojiunga bila sharti la kituo waliposajiliwa.
Kwa kipindi cha Januari hadi Mei 2022 jumla ya kaya 2,341 kati kaya 6476 sawa na asilimia 6% wamejiunga na mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa katika halmashauri zote saba (07). Hali ya utoaji huduma za ichf/NHIF katika katika Mkoa unaendelea vizuri kwani wananchi waliojiunga na mifuko hii ya Bima wanapofika katika vituo vya kutolea huduma za afya wanapata huduma za afya kwa kulingana na huduma zinazopatikana katika kituo husika, kuanzishwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa malipo ya wanachama wa iCHF kwa njia ya kielekloniki (GePG). Mkoa wafanikiwa kutoa mafunzo kwa maafisa uandikishaji wapatao 296 kati ya maafisa uandikishaji 528 wanaohitajika katika mkoa sawa na asilimia 56% na kuwepo na upungufu wa maafisa uandikishaji wapatao 232 sawa na asilimia 44%
Hali ya ukusanyaji wa mapato kutokana na uchangiaji wa huduma za Afya sio wa kuridhisha katika Mkoa wa Singida kama inavyoonekana katika Kiambatisho Na: 11.
12.0 HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII
Huduma za Ustawi wa Jamii hutolewa kwa wananchi hususani kwa makundi maalumu zenye uwiano, haki na usawa ili kufikia maendeleo ya Makundi yote kwenye jamii ambapo hutolewa kwa kuzingatia Sera, Sheria, kanuni ,miongozo na taratibu. Hali halisi ya utoaji huduma kwa makundi hayo ni kama ifuatavyo
Wazee wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea Kitaifa wanakadiriwa kuwa Jumla 2,507,568 ambapo Ke 1,307,358 na Me 1,200,210 Mkoa kwa mwaka 2020/21 umetambua Wazee 65,454 ( Ke. 30,851 na Me 34,603) kati ya hao Wazee 9,432 (Me. 5,307 na Ke 4,125) wamepatiwa vitambulisho vya matibabu sawa na 14% kama ilivyoainishwa katika Kiambatisho Na 12 (i).Aidha Mabaraza ya Wazee ya ushauri yameundwa katika ngazi zote mabaraza hayo huwasaidia Wazee kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu katika maisha yao.
Pia Mkoa una Makazi ya kulelea Wazee wasiojiweza ya Sukamahela yaliyopo Halmashauri ya Manyoni, Makazi yana jumla ya Wazee 16 Me 12 na Ke 04 ambao hupatiwa mahitaji ya Chakula, Malazi, Afya na msaada wa kisaikolojia Aidha Makao ya Wazee yaliyopo Chaberereko katika Halmashauri ya Mkalama yana Wazee 18 ( Me 11 na Ke 07) ambayo yalianzishwa na Kanisa la KKKT, kwa sasa Wazee hao wanahudumiwa Chakula na Matibabu na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kushirikiana na Masista wa Kanisa Katoliki wa Mwanga. Idadi ya Wazee na Makazi ya Wazee imeambatishwa kwenye Kiambatisho Na 12 (ii)
12.2 Hali halisi ya watu wenye ulemavu
Mkoa kwa Mwaka 2020/21 umetambua Watu wenye Ulemavu wapatao 12,804 kati ya hao walemavu wa viungo ni 5,814(45.% ) walemavu wa akili 2,599 (20.2%) viziwi 1799( 14%) na Watu wenye ualbino 442 (3.4%) huduma zitolewazo kwa Wenye Ulemavu ni Vifaa vya kujimudu, Afya, Elimu na uwezeshwaji kiuchumi kupitia 2% ya mapatao ya ndani ya Halmashauri pamoja na Elimu ya Ufundi Stadi Kamati za Kuhudumia Watu wenye Ulemavu zimeundwa Ngazi ya Mkoa 1(100%) Ngazi ya Wilaya 7 ( 100%), Ngazi ya Vijiji/Mitaa 494( ) Kamati hizi husaidia kujadili changamoto za Watu wenye ulemavu katika ngazi husika na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkoa una Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi kinachowezesha Watu wenye ulemavu kupata elimu ya ufundi stadi na Jumla ya walemavu 89 (Me 37, Ke 52 ) wasio na ulemavu 7 ( Me 6 Ke 1) .Rejea Kiambatisho Na 12 (iii, iv&vi)
12.3 Hali halisi ya watoto walio katika mazingira hatarishi
Kwa mwaka 2020/21 jumla ya Watoto 15,859 (Me 7,454 na Ke 8,405) walio katika mazingira hatarishi wametambuliwa kati ya hao Watoto 8,231 sawa 52% walipatiwa huduma za Afya, kuunganishwa na Familia zao, Ushauri nasaha, Msaada wa kisheria, Elimu. Aidha sababu kubwa ya kuongezeka kwa watoto walio katika mazingira hatarishi kimkoa ni pamoja na Umasikini, Malezi yasio chana kutoka kwa Wazazi au Walezi pamoja na maambukizi ya VVU na UKIMWI.
Aidha Jumla ya Watoto 186 ( Me 82 na Ke 104) wanalelewa katika Makao ambapo Watoto hao hupatiwa mahitaji yote ya msingi .Rejea Kiambatisho Na 12 (v& vi)
13.0 SEKTA BINAFSI
Ili kuwezesha utoaji wa huduma bora za afya, Ustawi wa jamii na Lishe na zinazofikika kirahisi kwa watu wote, Serikali inaendelea kutoa huduma kwa ubia na Sekta Binafsi. Katika kufanikisha Mashirikiano hayo, Serikali imeingia Mikataba ya utoaji wa huduma na Mashirika ya Dini. Kupitia ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi huduma zifuatazo zinatolewa bila malipo; Afya ya Uzazi na Mtoto, VVU/UKIMWI, Kifua Kikuu na Ukoma, Malaria. Kati ya vituo 44 vya Sekta Binafsi vituo tisa (9) tu ndiyo vyenye mikataba na Halmashauri.
Kwa ngazi ya Mkoa,Wizara ya Afya imeingia Mkataba na Hospitali ya Mt. Gaspar kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa na rufaa ngazi ya Mkoa. Kwa ngazi ya Wilaya Serikali imeingia Mikataba na Hospitali ya Mt. Carolus Mtinko kwa ajili ya kutoa huduma za Afya ngazi ya Wilaya kwa Halmashauri ya Singida, na Hospitali ya Makiungu kwa ajili ya kutoa huduma kama Hospitali teule ya Wilaya kwa Halmashauri ya Ikungi.
Serikali inalipa mishahara kwa baadhi ya watumishi kwenye hospitali za Mt Gaspar, Mt Carolus Mtinko, Makiungu, Iambi na Kilimatinde.
Aidha huduma za Afya zinazotolewa na Hospitali za Malikia wa Ulimwengu, IAMBI na Kilimatinde ni za kusuasua, kunakosababishwa kwa kiasi kikubwa na kushindwa kulipa Mishahara ya watumishi, hii inapelekea watumishi wenye sifa na ujuzi kuhama katika hospitali hizo.
Huduma zinazotolewa na Hospitali ya Mt. Gaspar ni pamoja na: Huduma za Kibingwa
Magonjwa ya kina mama, Upasuaji na magonjwa ya watoto. Hospitali ya Makiungu inaendelea kufanya maboresho ya miundo mbinu itakayowezesha utoaji wa huduma za rufaa ngazi ya Mkoa, miundombinu inayojengwa ni: Jengo la Magonjwa ya Dharura, Jengo la mazoezi ya viungo, Jengo la magonjwa ya mlipuko, Karakana ya matengenezo ya Vifaa tiba, Jengo la wagonjwa mahututi (ICU) na huduma za uchunguzi za mionzi (CT-Scan).
Pia Sekta binafsi imekuwa ikitoa huduma katika jamii kwa kuendesha Kliniki za magonjwa mbalimbali, Famasi, Maduka ya Dawa Muhimu na Maabara.
15.0 USHAURI NA MAPENDEKEZO
16.0 HITIMISHO
SINGIDA
Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA
Telephone: 2502170, 2502089
Mobile: 2502170, 2502089
Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.