• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Bomba la mafuta kutoa fursa kibao Singida - Dkt. Mahenge

Posted on: September 10th, 2021

Wito umetolewa kwa wananchi mkoani Singida  kutumia fursa zitakazopatikana wakati wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) utakao anza hivi karibuni mkoani hapo  ili waweze kujiongezea kipato na kuondoa umaskini.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ametoa wito huo hivi karibuni  wakati akifungua mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano  ofisi za Mkaguzi wa Hesabu  na kuhusisha Wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida na kuwataka kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zitapatikana wakati wa ujenzi wa bomba hilo.

Amesema  ujenzi wa bomba hilo utakuwa na jumla ya  vituo 14 katika Wilaya na Mikoa mbalimbali ambapo kituo cha  11 kitakuwa mkoani Singida katika kijiji cha Ntondo kilichopo Manispaa ya Singida Mjini.

Dkt. Mahenge amesema kituo hicho kitakuwa na watumishi kuanzia 1,000 hadi 2,000 ambao watahitaji kula, kulala na kunywa  hivyo  wananchi wa Singida wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuanza kuwekeza  kwa kujenga vyumba za kupangisha, nyumba za kulala wageni pamoja na ufugaji wa kuku ili wapate kipato na watoe ajira kwa wengine.

Aidha Serikali tayari imeandaa mazingira wezeshi yanayovutia uwekezaji kwa kutengeneza barabara  na kuweka umeme ili wananchi waweze kuendelea na mapambano ya kuondoa umasikini alifafanua Mkuu wa Mkoa.

Akimalizia hotuba yake Mhe. RC ameeleza kwamba Serikali mkoani hapo imeendelea kuongea na mabenki mbalimbali wapunguze riba katika mikopo yao ili iweze kuwavutia wateja .

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Dorothy Mwaluko moja ya wadau katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amesema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 140  kwa Singida ambapo litapita katika wilaya tatu  za Iramba, Mkalama na Singida Vijijini.

Katibu Tawa huyo amebainisha kwamba jumla ya vijiji 31 na kata 17 vitapitiwa na mradi huo  hivyo kuwataka wananchi wa maeneo husika kuhakikisha wanatumia fursa kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla .

Kwa upande wake Bw. Safiel Msovu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) katika wasilisho lake mbele ya mgeni rasmi amebainisha kwamba urefu wa Bomba kutoka Uganda hadi Tanzania ni km 1,443. Urefu upande wa Uganda ni km 296 na Tanzania ni km 1,147. Uwezo wa Bomba kusafirisha mafuta ni mapipa 216,000 kwa siku.

Aidha Bw. Msovu amefafanua kwamba mradi huo ni mkubwa na unagharimu kiasi cha dola bilioni 3.5 sawa na shilingi triloni nane (8) na unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kuwa mikataba muhimu  imekamilika.

“Wanahisa katika mradi huo ni kampuni ya ufaransa inayojulikana kwa jina la Total, Uganda kupitia shirika la mafuta la  UNOC, kampuni ya kichina ya CNOOC na Shirika la Uendelezaji wa Petrol nchini (TPDC)” alisema Bwana Msovu.

Kwa mujibu wa muundo wa sasa wa mgawanyo wa hisa, kampuni ya Ufaransa Total itamiliki asilimia 62, kampuni ya China CNOOC asilimia 8, UNOC ya Uganda  itamiliki asilimia 15 na asilimia 15 iliyobaki itamilikuwa na  Tanzania kupitia kwa kampuni yake ya maendeleo ya mafuta TPDC.

 Hata hivyo alimalizia kwamba  mradi huo unategemewa kujengwa kwa kipindi cha miaka mine (4) na unategemewa kutoa huduma kwa miaka isiyopungua 25, alimalizia bwana   Safiel Msovu

Wafanyabiashara mkonia Singida kwa umoja wao wamesema kwamba wamejipanga kutumia fursa hiyo ila wameomba Serikali kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za mara kwa mara  kuhusiana na maendeleao ya mradi huo

Mwisho.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.