• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

ILI KUPUNGUZA AJALI BARABARANI; MADEREVA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU HURIA SINGIDA.

Posted on: December 4th, 2017

  Madereva wa vyomo vya moto hasa bajaji na bodaboda wamewahimizwa kujiunga na chuo kikuu huria ili waweze kujiendeleza kielimu na kuboresha huduma zao, ambapo kwa kufanya hivyo watasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi cha Mjini Singida.

Amesema masomo ya chuo kikuu huria humwezesha mtu kujiendelea kwa kupata elimu bora bila kuathiri shughuli zake za kila siku hasa za kujipatia kipato.

“Dereva wa bodaboda, bajaji au mkazi yeyote mkoani kwetu, tusiridhike na elimu tuliyonayo, kumbukeni elimu haina mwisho. Hivyo tutumie chuo chetu hiki cha huria kujiendeleza kielimu. Tukiwa na wasomi wengi mkoa wetu kwa vyovyote   lengo la kuwa na uchumi wa kati na chini ya viwanda utalifikia kwa haraka”, amesema.

Dkt Nchimbi amwataka madereva wa vyombo vya moto kutii na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali na sio tu kuendeshwa na kamera za barabarani.

“Baadhi  ya madereva wa vyombo vya moto, hawaheshimu kabisa sheria za usalama barabarani, wanaendeshwa na  kamera. Siku moja yupo dereva mmoja wa bodaboda alikuwa mbele yangu, huku akiandika ujumbe kwenye simu yake. Utamaduni huu haufai kwa sababu ni chanzo cha ajali”,amesema Dkt.Nchimbi.

Aidha amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba kusimamia zoezi la madereva wa bajaji na bodaboda kujiunga na Chuo kikuu Huria.

“Hebu angalia uwezekano wa kuanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya madereva hawa kujiendeleza kielimu. Tunataka ifike siku tuwe na madereva hawa wana diploma au digrii, kwa hili nina imani na wewe utaweza kuwasaidia vizuri”, amesema.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amesema atagharamia safari ya viongozi wa madhehebu ya dini kwa kutoa kiasi cha shilingi laki tano, kwenda kufanya sala maalum kwenye maeneo yaliyokidhiri  kwa vitendo vya ajali.

“Karibu kila wilaya ina eneo ambalo ajali haziishi kutokea mara kwa mara. Nina imani Mungu hajanipa mkoa wenye maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajali. Nimekubaliana na viongozi  wangu wa madhehebu ya dini wataenda katika maeneo hayo, na kuomba Mungu atuondolee balaa la ajali za barabarani kwenye maeneo hayo”, amesema.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amewaagiza viongozi wa madereva wa bodaboda na bajaji, kusimamia vema madereva hao ili wapunguze ajali za barabarani.

Mmoja kati ya wakazi wa Manispaa ya Singida, Njolo Kidimanda, amesema kuwa kuna haja  serikali kuongeza kiwango cha faini kwa madai kiwango kilichopo, hakiwaogopeshi kabisa  baadhi ya madereva.

Aidha, Kidimanda ameshauri madereva kuwa mstari wa mbele katika kuchangia damu salama, ili kusaidia majeruhi wa ajali barabarani wenye hitaji la damu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, jumla ya watu 68 wamefariki kutokana na ajali za barabarani kati ya Januari hadi Oktoba mwaka huu. Idadi hiyo imeonyesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na ajali za  barabarani kwa kuwa katika kipindi hicho hicho mwaka jana, watu 152 walifariki.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.