• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

KILA KIJIJI KUCHIMBIWA KISIMA CHA MAJI SAFI MKOANI SINGIDA

Posted on: March 6th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, leo tarehe 6 Machi, 2024 amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa Miradi ya Maji inayotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika Wilaya ya Mkalama na Iramba mkoani humo.

Akizungumza katika nyakati tofauti Serukamba amemuagia Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said, kuhakikisha kila kijiji mkoani humo ambacho kinachangamoto ya upatikanaji wa maji kinachimbiwa kisima pamoja na kujengewa miundombinu imara ili wananchi waweze kupata maji kwa ukaribu kwa kuwa gari la kuchimba lipo.

 "Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshatuletea gari la kuchimbia visima, sasa siona sababu ya wananchi kukosa huduma ya maji, natoa wiki mbili kila halmashauri iniletee mpango kazi wake kuhusu utekelezaji wa huduma ya maji vijijini" RC Serukamba

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo ametoa rai kwa wananchi hususani jumuiya ya watumia maji kutunza miundombinu ya maji iliyojengwa na inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kutokata mabombo, kulinda vyanzo kwa kupanda miti pamoja na kutumia maji vizuri.

"Serikali imetuletea huduma ya maji safi na salama, hizi ni juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi wake, ninawaomba tumuunge mkono kwa kuitunza miradi hii ili itutunze" RC Serukamba

Naye Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said, amemhakikisha Mkuu wa Mkoa huo kwamba kuanzia mwezi huu Machi, gari hilo litakuwa na ratiba ya kuchimba visama vya maji kwenye maeneo ambayo yanachangamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Mkalama Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Omary Matembo, amesema kwa sasa ni asilimia 68.23 sawa na wananchi 174,346 wanaopata huduma hiyo kati ya wananchi wote 255,514.

Mhandisi Matembo, amefafanua kuwa huduma ya maji katika Halmashauri ya Wilaya hiyo hutokana na vyanzo vya maji chini ya ardhi ambavyo ni visima virefu, vifupi na vya kati ambapo katika miundombinu ya maji iliyopo vituo vya kuchotea maji (water points) ikiwa ni jumla ya 885.

Naye Meneja wa RUWASA Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhandisi Ezra J. M, amesema ujenzi wa mradi wa maji kwa vijiji vya Galangala na Kisharita vilivyopo kata ya Kinampanda umeanza tarehe 2 Oktoba, 2023 na unatarajiwa kukamilika tarehe 2 Aprili, 2024 ambapo gharama ya mradi ni Shilingi 976,636,255.04 na utekelezaji kwa sasa umefikia asilimia 85 na ukikamilika utawanufaisha zaidi ya watu 8,782.

Kwaupande wao wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwasogezea huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa vijijini na kueleza kuwa huduma hiyo imeongeza hali ya kiuchumi, kifamilia kwakuwa imepunguza muda mwingi uliokuwa ukitumika kwaajili ya utafutaji maji sambamba na kuepushwa na magonjwa yatokanayo na maji machafu.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.