• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

KUWAFANYA WATOTO WETU KUWA SALAMA NI WAJIBU WETU

Posted on: October 25th, 2024

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida,Daktari Fatuma Mganga amewaasa wadau Kuendelea kuwajibika katika kuhakikisha usalama wa  watoto,vijana na familia zinazoguswa na mradi wa  USAID-Kizazi hodari kwa kupatiwa huduma stahiki kwa mafanikio chanya kwa mnufaika mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

      Ameyasema hayo aliposhiriki katika kikao cha mrejesho wa mradi wa USAID,Kizazi hodari kanda ya kaskazini Mashariki chenye lengo la kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mradi kwa mwaka 2024 katika Halmashauri nne,  kujadili na  kuweka mikakat ya utekelezaji wa shughuli za mradi kwa mwaka mpya 2025 na kutambulisha Halmashauri ya Itigi iliyoongezwa kwenye utekelezaji wa Mradi huo kwa mwaka wa fedha 2025.

"Tuna wajibu wa kuwafanya watoto wetu wawe salama, wenye furaha wakati wote kwa kuwapenda,kuwajali na kuhakikisha wanafikia ndoto zao wakiwa na uzalendo na kujivunia kuwa Watanzania.Tukatekeleze mradi huu kwa tija na ushirikiano katika kuhakikisha matokeo makubwa kwenye kuibua Watoto wote wanaohitaji huduma na kuhakikisha wote wanapatiwa huduma muhimu" alisema Daktari Fatuma Mganga.

Lengo la mradi huu ni  kuboresha na kuimarisha Afya na Ustawi wa Watoto, Vijana na Kaya zao walioathiriwa /kuathirika na Virusi vya Ukimwi. Lengo likitegemea kufikiwa kwa huduma mbalimbali zinazotolewa na mradi huo ikiwemo afya, lishe, msaada wa kisaikolojia, ulinzi na usalama wa mtoto, uimarishaji uchumi wa kaya na elimu kupitia mfumo jumuishi wa kitaifa wa usimamizi wa Mashauri ya watoto.

Pia amepongeza uongozi wa makao makuu ya KKKT  kwa kuendelea na utekelezaji wa mradi huo ambao Mkoa wa Singida ni sehemu ya wanufaika wa mradi huo katika wilaya za Ikungi, Manyoni, Iramba na Manispaa ya Singida .

 Kwa mwaka wa fedha 2024  jumla ya walengwa 8,185 walifikiwa na kupewa huduma sawa na asilimia 119 ya 6,890 waliopangwa kufikiwa na kupewa huduma huku mwaka 2025 mradi ukipanga kuwafikia Jumla ya walengwa10,389  katika Halmashauri tano za mradi wenye kaulimbiu isemayo," Kizazi Hodari - Taifa Endelevu’"


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.