• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Mfumo wa M-Mama wazindulia rasmi Mkoani Singida, Serukamba aagiza kutumika kupunguza vifo vya Mama wajawazito na mtoto.

Posted on: November 22nd, 2022

Halmashauri za Mkoa wa Singida zimetakiwa kutenga fedha katika mipango na bajeti zake kwa ajili ya gharama za usafiri wa dharura kwa Mama wajawazito na watoto wachanga.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo Novemba 22, 2022 wakati akifungua kikao cha Uzinduzi wa Mpango wa Usafirishaji wa dharura kwa akina Mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (M-Mama) kwa Mkoa wa Singida.

Rc Serukamba ameelekeza kwamba mfumo huo utakuwa ni msaada mkubwa kwa  wananchi wa Singida kwakuwa utasaidia kupunguza vifo vya  Mama wajawazito, wanaojifungua na watoto kwa kuweza kufikishwa Hospitali au vituo vya afya kwa wakati.

Amesema mpango wa huduma hiyo utaboresha zoezi la rufaa kati ya vituo vya kutolea huduma za Afya, hasa upatikanaji wa usafiri wa dharura kutoka kituo kimoja hadi kituo kinachoweza kutoa huduma ya viwango vya juu ambapo ameeleza kwamba utasaidia kupunguza changamoto ya upungufu kusubiria foleni ya magari ya wagonjwa.

“Kama tunavyofahamu huduma za Afya ya Mama na Mtoto hutolewa bila malipo, kwa hiyo hatua mbalimbali za kuhakikisha huduma bora zinapatikana katika Mkoa wetu wa Singida, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyotoa huduma kamili za dharura na Upasuaji kutoka vituo vya huduma sita (6) mwaka 2020 hadi saba (7) mwaka 2022” amesema Serukamba

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma hotuba yake mbele ya washiriki wa zoezi la uzinduzi rasmi wa  Mfumo wa M-Mama uliyofanyika kimkoa katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wake Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Mkoa wa Singida Christoweru Barnaba wakati akitoa wasilisho lake amesema mradi huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Aidha ameleeza kwamba  uwepo wa changamoto ya Upungufu mkubwa wa magari (Ambulance) za kubebea wazazi na wagonjwa wanaohitaji rufaa hasa Halmashauri ya Itigi, Mkalama, Singida, Ikungi kwa uwepo wa mradi huo utasaida kwa kuwa magari binafsi yatasajiliwa kwa ajili ya kupeleka wagonjwa.

Akimalizia wasilisho lake Christoweru ametoa wito kwa  mama wajawazito kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani au njiani na badala yake wahakikishe wanafika hospitalini ili waweze kukutana na wataalamu.

Mratibu wa Afya ya uzazi na mtoto Mkoa wa Singida Christoweru Barnaba, akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi huo.

Aidha Mkurungenzi  wa mfumo wa M-Mama Dolorosa Duncan kutoka Kampuni ya Vodafone  foundation amesema Serikali kwa kushirikiana na Vodacom inatekeleza mfumo wa rufaa na usafiri wa dharura – M-Mama ambao umefanyiwa majaribio katika Wilaya za mkoa wa Mwanza na Shinyanga na kuona unafanya kazi kwa ufasaha.

Hata hivyo Dolorosa ameendelea kueleza kwamba mfumo huo kwa sasa umeanza kutekelezwa katika mikoa ya Shinyanga Lindi Mororgoro Dodoma Tanga  na sasa Singida na Manyara ambapo utaendelea kutekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.

Mkurungenzi  wa mfumo wa M-Mama Dolorosa Duncan,akiwasilishamadawakati wa uzinduzi huo


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.