• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Mkurugenzi Mtendaji wa Cambridge Education amefurahishwa na utekelezwaji wa programu ya Shule Bora

Posted on: May 25th, 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Cambridge Education duniani Bw. Nicholas Santcross hivi karibuni  ametembea Mradi wa Shule Bora Mkoani Singida ili kujionea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita wa 2021/2022.

Akiongozana na Mshauri Kiongozi wa programu Bi Laura Mclnerney, amekutana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa (RAS) huo Ndg Stanlous Choaji pamoja na Afisa Elimu Mkoa Dkt. Baganda Elpidius na kujadili namna ya utekelezaji wa programu  unavyofanyika na bàadhi ya maboresho ili kuongeza tija katika eneo la elimu.Aidha, ugeni huo umetembelea shule za Msingi  za Somoku na Nyerere ambapo walijionea madarasa yaliyojengwa kupitia Miradi ya EQUIP Tanzania na EPforR-I,utekelezaji wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) pamoja na Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWaWa). Vilevile, ugeni huo ulishiriki katika upandaji wa miti kama ishara ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira shuleni kwa ajili ya upatikanaji wa kivuli na matunda.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo kutoka   nchini Uingereza amepongeza jitihada za Serikali kwa kushirikiana na programu ya Shule Bora kwa namna walivyofanikiwa kuunda Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWaWa) na usimamizi wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) hali iliyosababisha kuwepo kwa  matokeo chanya kama vile kuongezeka kwa umahiri wa walimu katika ufundishaji,  upatikanaji wa chakula shuleni,  usimamizi wa elimu jumuishi, usalama wa mtoto na ushiriki wa jamii katika masuala mbalimbali ya elimu. “Nimefurahishwa na jinsi programu hii inavyotekelezwa. Ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo Serikali,unaleta ufanisi katika utekelezaji wa programu hii na ni mfano wa kuigwa. Cambridge tuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha elimu bora inapatikana”, alisema Bw. Nicholas.

Aidha, kwa upande wake RAS ameeleza kwamba programu hii imesaidia kutoa mafunzo kwa walimu yaliyokuwa na lengo la kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji ambapo tayari mafanikio yameanza kuonekana huku akieleza kufanikiwa kuongeza uhusiano baina ya Walimu na Wazazi kupitia umoja wao wa UWaWa ambapo umesaidia kuongeza idadi ya madawati, upatikanaji wa chakula shuleni na kupunguza utoro wa wanafunzi na walimu.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt. Banganda wakati akishukuru ugeni huo ameeleza bàadhi ya mafanikio ya programu ya Shule Bora. Dr Baganda amesema kwamba programu ya Shule Bora imekuwa na tija kwani bàadhi ya mbinu za ufundishaji na usimamizi wa shule zinazotumika katika mradi wa shule Bora katika shule za msingi na Awali zimeanza pia kuigwa katika shule za Sekondari kwa kuwa zimeonekana kusaidia kuondoa mdondoko na utoro wa wanafunzi shuleni.

Hata hivyo, Dr Baganda ametaja kuwepo kwa baadhi ya changamoto  ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mashine zenye uwezo mkubwa wa kuchapisha mitihani ya ndani na upungufu wa  miundombinu ya shule.

Naye Samwel Daniel ambaye ni Mratibu wa Shule Bora Mkoa wa Singida alieleza kwamba ujio wa wageni hao umeongeza morali na chachu ya utendaji kazi kwa wote wanaoguswa na programu  jambo ambalo amesema litaleta matokeo chanya katika utekelezaji .Aidha, Ndg Samwel ametoa wito kwa wasimamizi wa elimu katika ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Shule kuweza kusimamia na kutekeleza kwa ufanisi shughuli zote zinazotekelezwa na Serikali kupitia Mradi wa Shule Bora ili kuboresha ujifunzaji,ufundishaji,ujumuishi na uimarishaji wa mifumo ya usimamizi wa elimu.

Shule Bora ni programu ya Serikali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia UK aid. Programu hii inatekelezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara kwa  ushauri wa kitalamu kutoka Cambridge Education ikishirikiana na ADD International,International Resque Committee na Plan International.

Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt. Banganda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Cambridge Education duniani pamoja na baadhi ya wajumbe ambao ni waratibu wa shule bora mkoani Singida wakati alipotembelewa ofisini kwake.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Cambridge Education duniani Bw. Nicholas Santcross akishiriki upandaji miti wakati wa ziara yake mkoani Singida.

 Mratibu wa Shule Bora Mkoa wa Singida Samwel Daniel ambaye akishiriki upandaji miti wakati wa ziara yake mkoani Singida.



Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.