• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RAS Singida awatembelea wakufunzi wa Sensa ahimiza umakini katika kazi.

Posted on: July 18th, 2022

Makarani wa Sensa Mkoani Singida wametakiwa kuongeza umakini wakati wa kufanyika kazi  madodoso kwa kuzingatia mila na desturi za jamii husika  ili kuepuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza wakati wa kuendesha zoezi hilo.

Akiongea na wakufunzi hao leo wakati wa mafunzo hayo  ya Sensa  katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani hapa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Mwl. Doroth Mwaluko amesema pamoja na kujua namna ya kuuliza maswali lakini lazima saikolojia itumike kwa sababu bado jamii za watu wa Mkoa huo zinaishi kutokana na mila na desturi.

"Wapo watu ambao hawapendi kutoa taarifa zao za ndoa mfano swala la ndoa mara nyingi ni siri za familia hivyo unaweza kukosa majibu yaliyotarajiwa, ni lazima kutumia saikolojia na kuangalia mambo ya mila na desturi za maeneo husika katika kuuliza maswali" Alisema

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Mwl. Doroth Mwaluko akiongea na wakufunzi wakati wa mafunzo ya Sensa  katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Singida.

Hata hivyo Mwaluko amewataka wakufunzi hao kuwa na uvumivu mkubwa na kutumia vizuri nafasi waliyopata  kwa kuwa taifa limewaamini kwamba wana uwezo wa kukamilisha zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Awali mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Neing'oya Kipuyo amesema mafunzo hayo ni ngazi ya pili ya Mkoa ambayo yalianza tarehe 6 Julai na yatahitimishwa Julia 26 watakuwa tayari kwenda  kuwafundisha Makarani ngazi ya Kata na Tarafa.

Mratibu huyo ameeleza kwamba Mkoa wa Singida utakuwa na jumla ya Makarani na wasimamizi 542 ambao ndio watakaoshughulika na zoezi lote la Sensa.

Alisema  Sensa ya watu na makazi ina madodoso manne ambayo ni dodoso la makundi maalum, ambalo linahusu ukusanyaji wa taarifa za makundi ambayo hayawezi kuhesabiwa na madodoso ya kawaida.

Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Neing'oya Kipuyo akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mafunzo ya Sensa yanayofanyika katika ukumbi wa Veta  mkoani Singida.

Kipuyo aliendelea kueleza kwamba lipo dodoso la jamii ambalo linajazwa ndani ya siku mbili kabla ya siku ya Sensa wakati Karani akiwa analitambua eneo lake la kuhesabiwa watu ambapo anakusanya taarifa zinazohusu mambo ya kijamii kama mashule  zahanati masoko na huduma za kifedha.

Dodoso jingine  ni la majengo ambalo taarifa hukusanywa  kuhusu majengo yote ya makazi na yasiyo ya makazi,  na dodoso la anwani za makazi ambalo linalenga kukusanya taarifa mbalimbali za anwani za makazi kama majengo nyumba na viwanja.

Amesema tayari wameshakamilisha madodoso matatu kati ya manne na kundi hilo linatakiwa kuanza mafunzo ya vitendo siku ya tarehe 19 Julai 2022.


Mafunzo yakiendelea

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.