• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC. Mahenge akagua miradi ya ujenzi nyumba za wakuu wa Wilaya na Watumishi, atoa siku 15 kuanza kutumika.

Posted on: January 31st, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge amewapongeza wakandarasi wanaosimamia miradi ya  ujenzi wa nyumba za  watumishi na  ofisi za wakuu wa Wilaya ikiwemo Ikungi, Singida DC  na Mkalama kwa hatua majengo hayo yalipofikia na kuwataka kukamilisha ndani ya kipindi kisichozindi siku 15 kazi hizo zilizobaki ziwe zimekamilika na ofisi kuanza  kutumika.

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 31 Januari 2022 wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa ofisi hizo ikiwa ni pamoja na kuona changamoto zilizokabili ujenzi  na kuzitafutia suluhisho kwa kipindi kifupi.

Akiwa katika mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wilayani Mkalama Dkt Mahenge akawataka wakuu wa Idara ambao wanatakiwa kuzitumia nyumba hizo kuhakikisha wanaingia kabla ya tarehe 15 na endapo atakuwepo yeyote ambaye hatatekeleza agizo hilo kwa sababu zake hatalipwa posho ya nyumba kama inavyofanyika hivi sasa alibainisha RC Mahenge.

Aidha RC Mahenge ametoa siku mbili kwa wakandarasi wa nyumba za watumishi Mkalama kumalizia uwekaji wa vifaa vidogo vidogo  vilivyobaki vikiwemo soket, Koki za maji na taa, endepo kutakuwa na changamoto ya umaliziaji huo kila mtumishi anayestahiki kuingia kwenye nyumba hizo akamilishe Mwenyewe.

Aidha akawakumbusha viongozi mbalimbali wa Wilaya hiyo kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa ukaribu ujenzi wa ofisi ya DC ambao umekuwa ukisuasua kwa kufanya mawasiliano na makao makuu ya Hazina kuhakikisha fedha zilizotolewa zinamfikia mkandarasi ambaye ni Wakala wa Majengo  nchini TBA.

Awali akitoa taarifa za ujenzi wa nyumba hizo  Mkurugenzi Mtendaji  Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Asia Messos  amesema ujenzi wa nyumba za watumishi umegharimu kiasi cha Tsh.milioni 401.2  

Amesema mradi huu ukikamilika utaokoa kiasi cha Tsh. milioni 3.6 zinazotumika kila mwezi kulipa stahiki za wakuu wa Idara sita  ambapo kwa sasa zitatumika kwa ajili ya kazi nyingine za maendeleo aliendelea kusema Mkurugenzi Mtendaji.

Akijibu baadhi ya changamoto zilizopo katika ujenzi huo RC Mahenge akamtaka meneja wa Shirika la umeme TANESCO kuhakikisha wanafikisha umeme katika nyumba hizo ndani ya siku tano ili majengo hayo yaanze kutumika.

Wakati huo huo Kaimu Meneja wa wakala wa majengo  TBA Mkoa wa Singida Mhandisi Hadija Abdalah amesema mradi huo unagharimu kiasi cha Tsh, Bilion 1.2 na ulianza mwaka 2018 ambapo changamoto imekuwa ni upatikanaji wa fedha za mradi kwa wakati jambo lililosababisha kazi kusuasua ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 80.

Hata hivyo Mhandisi Hadija amesema kutokana na kuchelewa fedha kwa muda mrefu  kumesababisha kupanda kwa  gharama za manunuzi ya vifaa vya ujenzi  pamoja na kuchelewa kufanyika kwa uchunguzi wa udongo (geotechnical investigation)  kwa zaidi ya miezi mitano.

Akiendelea na ziara yake Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge  akatembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya DC katika wilaya ya Singida vijijini  ambapo kwa mujibu wa mtoa taarifa Kaimu Mkurugenzi  Masomo Mbelwa amesema ujenzi umefikia asilimia 75 na linatarajiwa kukamili hivi karibuni.

Amebainisha kwamba zipo changamoto za upatikanaji wa umeme katika eneo hilo na kuadimika kwa saruji  kutoka viwandani kulikosababishwa na utekelezaji wa miradi ya shule kupitia fedha za UVIKO19 pamoja na changamoto za miundombinu ya barabara katika eneo hilo.

Akimalizia ziara yake Wilayani Ikungie RC Mahenge akaendelea kuipongeza  kampuni Tanzu ya Mzinga iliyoko chini ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa hatua nzuri waliyofikia katika ujenzi ambapo wametumia gharama za kampuni kukamilisha kazi hiyo kwa asilia 95.

Amewataka kuendelea kutumia mbinu walizozitumia awali ili kukamilisha kwa asilimia mia moja wakati Serikali ikiandaa mazingira ya kuweza kulipa fedha zote zilizotumika katika ujenzi huo.

Ziara hiyo iliwahusisha Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Makatibu Tawala wasaidizi, Wakurugenzi na wakuu wa Idara mbalimbali

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kutoka kushoto) akikagua moja kati ya nyumba 6 za wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Mkalama. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa Dorothy Mwaluko (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkalama

Ujenzi wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkalama ukiendelea

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Singida Vijijini mara baada ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika kijiji cha Mwahango 

Muonekano wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika kijiji cha Mwahango

Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza na viongozi mbalimbali wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa Mkuu wavWilaya ya Ikungi

Mkuu wa MKoa wa Singida (kushoto) akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la Mkuu wa Wilaya Ikungi

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa ziara hiyo

Muonekano wa ujenzi wa jengo la Mkuu wa Wilaya ya Ikungi unaotekelezwa na Kampuni Tanzu ya Mzinga - Morogoro

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.