• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC Mahenge Aliapisha Baraza la Ardhi Mkalama

Posted on: March 10th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge leo ameliapisha Baraza jipya la ardhi la wilaya ya Mkalama baada ya viongozi hao kuteuliwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili kushughulikia migogoro mbalimbali ya ardhi wilayani hapo.

Akiongea baada ya kuwaapisha, RC Mahenge akawataka wajumbe hao kuanza kazi kwa kusoma mihutasari yote ya mabaraza ya nyuma ili waweze kupata uzoefu kabla ya kuanza kutatua kesi zinazowakabili wananchi wa Mkalama.

Aidha amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa  weledi mkubwa katika kuendesha kesi za ardhi na kufanya maamuzi ya busara pamoja na kuepuka vitendo vya rushwa, zawadi na takrima kwa kuwa vinaweza kuathiri maamuzi sahihi ya baraza.

Hata hivo RC Mahenge akatoa malekezo kwa baraza hilo kuhakikisha wanapunguza au kuondoa kabisa kero na migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha wanasikiliza pande zote na kuyatembelea maeneo yenye changamoto badala ya maelezo peke yake huku wakikumbushwa kutofautisha kesi za mashamba au ardhi na kesi za wizi wa aina yeyote ile.

“Mfanye maamuzi baada ya kujiridhisha kwa sababu kesi za ardhi nyingi zimekuwa ni za kifamilia lakini pia kuna tofauti kubwa kati ya kesi za mashamba au ardhi na kesi za wizi wa kuku, ninaomba mjifunze kwa wenzenu mshirikiane na vyombo mbalimbali mtakavyoona vinaweza kusaidia lakini mhakikishe haki inatamalaki Mkalama”. Alisema RC Mahenge.

Akimalizia hotuba yake Mkuu wa Mkoa akalitaka Baraza hilo kutafuta namna ya kutatua changamoto ya ardhi kwa vijana kwa sababu familia zinapoingia katika migogoro ya hiyo wanaoteseka na kuingia hasara ni Vijana .

“Nyuso zenu zinaonesha nyie ni watu waaminifu na wenye weledi mkubwa hivyo katika kutekeleza majukumu yenu mapya mfikirie njia nzuri ya kuwasaidia vijana ambao wamekuwa wakiathirika sana na migogoro ya aridhi hasa ile ya kifamilia”. Alisema RC Mahenge.

Mwisho wa Hotuba yake RC Mahenge akabainisha kwamba ardhi ni sehemu nyeti  kwa wanadamu na wanyama hivyo kazi hiyo inaweza kusaidia  ustawi wa jamii au kuharibu kabisa ambapo alielekeza kwamba utatuzi wa migogoro ufanyike kwa weledi mkubwa .

Naye DC wa Mkalama Sophia Kizigo akilipongeza baraza hilo kwa kupata uteuzi huku akieleza umuhimu wake katika kutatua matatizo ya wananchi wa Mkalama ambao wengi wao wamekuwa wakipoteza haki zao kwa kushindwa kusafiri umbali mrefu kusikiliza kesi zinazohusu ardhi zao.

Amesema wananchi wa Mkalama walikuwa wanalazimika kwenda mpaka Wilaya ya Iramba Mkoani hapo kusikiliza mashauri yao kwa kuwa huko ndipo baraza la ardhi lilipokuwa likipatikana na kulitaka kurejesha Imani za wananchi hao ambao haki zao zilipotea.

Aidha DC Kizigo akaeleza kwamba kiapo walichopata ni ulinzi kwao ambapo wanatakiwa kuepuka kupokea rushwa na kuhakikisha hawachonganishi wananchi .

Hata hivyo DC huyo akamalizia hotuba yake kwa kuahidi ushirikiano mkubwa kwa baraza hilo huku akikumbusha kwamba  litapimwa utendaji wake kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kuona kama linawasaidia wananchi kutatua migororo au inaongezeka.

Awali akitoa salamu zake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkalama  James Mkwega pamoja na pongezi kwa baraza hilo akawataka kumtanguliza Mwenyezimungu katika shughuli zao ili aweze kuwangoza katika kutatua matatizo ya ardhi ambayo yamekuwa mengi wilayani humo.

Mwenyekiti Mkwega akaendelea kueleza kwamba kazi kubwa imefanyika ya kupata baraza hilo ambapo kilikuwa ni kilio cha Madiwani wote kutokana na malalamiko ya wananchi kupoteza haki zao .

Kupata baraza ni jambo moja na huduma za baraza ni jambo la pili, ni matumaini yetu sisi wanamkalama kwamba huduma yenu itatusaidia kupata haki zetu, James Mkwega.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo Baraka Shuma kwa niaba ya wajumbe akatoa shukrani kwa kuteuliwa katika nafasi hiyo huku akiahidi kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa wilaya hiyo.

Shughuli hiyo ya uapisho ilihudhuriwa na Mkuu wa mkoa Singida, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba na Mweyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo Wajumbe walioapishwa ni Charles Jilangi, Kitundu Emanuel Kitundu, Hamisi Igimbi Salum na Zulfa Suphian Mvungi.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.