• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC SINGIDA AWAOMBA VIONGOZI KUHAMASISHA WATU KWENDA KUJIANDIKISHA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Posted on: September 17th, 2021

MKUU wa Mkoa Singida Dkt.Binilith Mahenge amewaomba viongozi mbalimbali mkoani hapa kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kushiriki zoezi la majaribio la Sensa ya Watu na Makazi.

Dkt.Mahenge ametoa ombi hilo katika kitongoji cha Gajaroda kilichopo Kijiji cha Dominiki  wilayani Mkalama alipofika kukagua zoezi hilo ambalo limeonesha kupata mafanikio makubwa kutokana na uhamasishaji uliofanyika.

" Kama uhamasishaji uliofanyika katika eneo ili na hakukuwa na changamoto yoyote kama walivyosema wataalamu wetu wanaofanya kazi hii Mkoa wa Singida utakuwa na nafasi kubwa ya kufanikisha sensa itakayofanyika mwakani ". alisema Mahenge.

Alisema kama katika eneo hilo la kijijini limefanikiwa kwa kiasi hicho anaamini kwa maeneo ya mjini itakuwa ni nafuu zaidi.

Alisema lengo kubwa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

Alisema taarifa za idadi ya watu zitakazopatikana katika sensa hiyo husaidia mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Alisema Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum. Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. 

Alisema takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

"Jambo ili la sensa ni la muhimu sana hivyo  nawaomba wananchi ninao waongoza walipokee kwani ndio msingi wa maendeleo " alisema Mahenge. 

Kalani wa Sensa katika eneo hilo Elifrida Yunde alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni umbali wa kutoka kaya moja na nyingine hivyo hutumia muda mwingi wa kuzifikia na kuwa wananchi wamekuwa wakiwapa ushirikiano mkubwa licha ya kushindwa kujibu maswali mengine kwa ufasaha hasa yanayohusu umiliki wa mali kama mifugo na mashamba.

Mkuu wa wilaya hiyo Sophia Kizigo alisema changamoto kubwa inayowakabili wataalamu hao ni wingi wa kaya ambazo wanazipitia kwani awali zilidhaniwa ni chache lakini baada ya kufika eneo la tukio wamezikuta ni nyingi akitolea mfano wa kitongoji hicho ambacho walikisia kitakuwa na kaya 150 kumbe kina kaya 273 ambazo ni zaidi ya kijiji ambapo aliomba  ifanyiwe kazi.

Meneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing'oya Kipuyo alisema zoezi hilo linakwenda vizuri licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.

Msimamizi wa Sensa Mkoa wa Singida Profesa Mourice Mbago alisema changamoto kubwa ilikuwa ni usafiri wa kutoka eneo moja kwenda jingine ambayo imetatuliwa kwa msaada wa viongozi wa eneo hilo kwa kuwashirikisha wananchi wenye pikipiki ambao wamekuwa wakijitolea kuwapeleka wataalamu hao katika kaya mbalimbali kuendelea na kazi.

Mkazi wa Kitongoji hicho Lusia Samsoni alisema sensa hiyo ni nzuri kwani itasaidia kupanga mipango ya maendeleo kama ujenzi wa shule, zahanati, barabara na mambo mengine mengi

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.