• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Shirika la Umeme Tanesco latakiwa kuimarisha ulinzi Katika miundombinu Yao

Posted on: May 17th, 2022

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoani Singida wametakiwa kuimarisha ulinzi katika vituo vyao  vya kupoozea Umeme kikiwemo cha mkoani hapo kama tahadhari ya kupambana na waharibifu wa miundombinu hiyo.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 17.05.2022 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge alipotembelea Kituo hicho na  kujionea walinzi wakiwa wachache ndio akabaini kwamba usalama  wa eneo hilo la uwekezaji pamoja na wafanyakazi wake haujitoshelezi.

Akiwa katika ziara hiyo iliyowashirikisha vyombo vyote vya usalama vya Mkoa huo RC Mahenge  akasema uwekezaji huo ni mkubwa  hivyo unahitaji ulinzi wa kutosha huku akiwataka Tanesco kushirikiana na Jeshi la Polisi kabla ya kupata walinzi wao ili kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo.

Aidha amemtaka Meneja wa Tanesco Singida kutembelea Wilaya ya Mkalama Manyoni na Itigi kwa kuwa eneo hilo  inasemekana  Umeme unakatika Mara kwa Mara na kuleta kero kwa wafanyabiashara.

Akipokea maelekezo hayo Afisa usalama wa Shirika la Umeme Tanesco Devisi Mkuche amesema tayari wameandaa mkakati wa kukabiliana na hali ya kuimarisha usalama katika Mradi huo ambao tayari kulishaanza kuwa na wezi wa vitu vidogovidogo.

Amesema wameendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na Jeshi la Polisi ili kusaidia kukabiliana na hali hiyo wakati Shirika likiendelea kuandaa Mkakati wa kupata walinzi wake kupitia mashirika mbalimbali ya ulinzi.

Hata hivyo Mkuche ameeleza kwamba bado Mkandarasi wa mitambo hiyo  hajakabidhi  kwa Shirika jambo ambalo ililazimu swala la ulinzi kubaki mikononi mwa Mkandarasi huyo.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi huo Deogratius Nyantumbaga amesema Mradi huo umeshakamilika kwa upande wa Singida na tayari wameshawasha Umeme hivyo wanategemea kukabidhi kwa Tanesco mwishoni mwa mwezi ujao.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.