• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

SINGIDA KUNG'ARA MWENYEJI WA MEI MOSI 2025!

Posted on: March 11th, 2025

Kuelekea katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (maarufu kama Mei Mosi),Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo nchini Tanzania yatakayofanyika Tarehe Mosi mwezi Mei 2025.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 11, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego wakati akizungumza na wadau wa kamati  ya maandalizi ya maadhimisho hayo kimkoa na Kitaifa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mhe.Dendego amesema kuwa shughuli hiyo itafanyika katika uwanja wa Liti uliopo Manispaa ya Singida, ambayo itatanguliwa na   Shughuli mbalimbali ikiwemo v michezo mbalimbali,huku  jumla ya watu elfu mbili na miatano (2,500)wakitarajiwa kushiriki kwenye michezo hiyo itakayohusisha watumishi kutoka katika wizara tofauti,taasisi binafsi na za umma,

Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa katika kuendelea kusherehesha shughuli hiyo kutafanyika pia utalii wa ndani ya Mkoa wa Singida,lengo likiwa kuwaonyesha wageni waliofika Mkoani Singida mambo mbalimbali yanayopatikana katika Mkoa huu,ikiwemo fursa zilizopo za kiuchumi na uwekezaji.

Maadhimisho hayo yatapambwa na mambo mbalimbali kabla ya kilele ambapo kutakuwa na Usiku wa Kuku ( kuku festival) Mashindano ya magari, Mashindano na ngumi, maonyesho mbalimbali ya shughuli ambazo wanaSingida wanazifanya, Burudani mbalimbali ikiwemo Ngoma za asili na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakubwa hapa nchini.

Kwa upande wake rais wa Shirikisho la Wafanyakazi,( TUCTA) Tumaini Nyamhokya amesema kuwa kupitia mikakati mbalimbali iliyowekwa kwa kushirikiana na Uongozi wa Ofisi ya  Mkuu wa Mkoa wa Singida wanategemea  sherehe hiyo itafanyika vizuri na itakuwa ni ya kipekee sana kutokana na maandalizi makubwa yaliyoandaliwa.

"Singida ipo tayari kuwapokea wageni wote,wataishi vizuri..wenye hofu na malazi watalala vizuri,kwani maandalizi yamewekwa vizuri sana hivyo karibuni sana Singida kusherehekea Mei Mosi itakayofanya sana"amesema Bw.Nyamhokya.

Siku wa Wafanyakazi duniani maarufu kama Mei Mosi hufanyika kila mwaka lengo likiwa ni kuangalia na kufanya tathimini juu ya haki na usawa kwa wafanyakazi, kuzifahamu na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi pamoja na usalama wao mahala pakazi.


https://youtu.be/3fuA8Uth0vs?si=hKn_fxe1ESWoh2Cd

Mei Mosi singida 2025


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.