• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

SINGIDA NA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI, 8, 2024

Posted on: March 7th, 2024

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, ametoa wito kwa Wafanyakazi wa Serikali, wadau wa maendeleo, taasisi na wana Singida kwa ujumla kushiriki katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mwanammke Duniani yatakayofanyika kimkoa katika viwanja vya standi ya zamani Wilayani Ikungi Machi 8, 2024 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Mama Tunu Pinda Mke wa waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda.


Aidha Dkt. Fatuma Mganga ametoa rai kwa jamii mkoani humo kuchukua hatua za makusudi kushughulikia masuala ya ubaguzi wa kijinsia, mifumo kandamizi na uonevu kwa Wanawake.Akiizungumzia siku ya Wanawake Dunia amesema kila (Tarehe 8 Machi) Dunia inaadhimisha Siku ya Wanawake. Hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa mwezi Machi na maadhimisho hayo, Mkoa wa Singida kwa kushirikiana na Taasisi za Umma, Asasi za Kiraia, Wadau wa Maendeleo na Mamlaka za Serikali za Mtaa wamekuwa wakifanya mijadala yenye lengo la kuongeza idadi ya wanawake wa kuchaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.


Aidha Halmashauri mkoani hapa zimefanya maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali haswa wanawake kama vile utengenezaji wa Batiki, Makongamano ya kuelimisha jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili haswa Mashuleni.Pia Serikali ya Mkoa imefanya matendo ya huruma katika kituo cha Malaika wa Matumaini kilichopo Singida Mjini kwa kuwatembelea na kuwapatia zawadi watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, imefanya maonyesho ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vilivopatiwa mikopo ya Wanawake kwa Ngazi za Halmashauri.Sambamba na hayo mkoa umehamasisha elimu kutoka kwa wanawake waliofanikiwa, pamoja na kutoa vyeti kwa vikundi vya wanawake vinavyofanya vizuri katika marejesho ya Mikopo.


Dkt. Fatuma Mganga, amemalizia kwa kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuwatia moyo na kuwapa kipaumbele Wanawake kwa nafasi mbalimbali za Uongozi wa juu kwa Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla, mikopo nafuu kwa Wanawake vijana na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kiuchumi kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kuleta maendeleo binafsi na nchi kwa ujumla.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho kwa huu wa 2024 ni:

 ‘Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii’

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.