• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

"SINGIDA TUJILINDE NA MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU NA UKIMWI":DC GONDWE

Posted on: December 1st, 2024

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Leo hii katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani Disemba Mosi,2024 amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego yakiyoadhimishwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida katika chuo Cha uhasibu kampasi ya Singida.

Akizungumza katika maadhimisho hayo,ametoa wito Kwa vijana kupima afya zao ili kuweza kuziishi ndoto zao nyingi huku akiwasisitiza wanandoa kuwa waaminifu ili kuepuka ongezeko la maambukizi huku akisisitiza tohara Kwa wanaume kama njia mojawapo ya kuzuia magonjwa Kwa wanaume


"Wanandoa wawe waaminifu Kwa wenza wao,pia ni vema kuwapenda,kuwajali na kuwahudumia waathirika WA VVU.Pia ni vema vijana wakaacha tamaa za maisha mazuri ili kuepuka vishawishi ambavyo vinasababisha kujiingizia katika vitendo vinavyoweza kupelekea kupata VVU,kuepuka hilo ni vema kuishi katika uhalisia WA maisha Yao na kupambania ndoto zao za baadae".amesema Gondwe.

Said Mgeleka ambaye ni Meneja wa Mradi kutoka USAID amesema kwasasa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI zinapatikana Kwa urahisi na Kwa wingi tofauti na miaka ya nyuma ambapo iliwalazimu watu wa makundi maalum pekee kama wamama wajawazito wakati WA kujifungia pekee na wagonjwa wale ambao CD4 zao zilianza kushuka na kusumbuliwa na magonjwa nyemelezi ndio waliokua wakipata dawa hizo kutokana na uchache wa dawa uliosababishwa na ufinyu WA bajeti

"Kwasasa dawa za ARV zinapatikana katika ngazi zote sio tu katika hospitali za mikoa na Taifa Bali mpaka katika zahanati zote vijijini kwani tangu 2016 juhudi za Serikali na wadau zimewezesha utoaji wa dawa hizo Kwa yeyote yule atakayegundulika na maambukizi bila Kujali wingi wa CD4 au dalili yeyote ya magonjwa nyemelezi"amesema Dkt.Mgeleka

Amesema kwasasa huduma za kinga dhidi ya VVU zimeongezwa Kwa kuleta dawa kinga Kwa watu wote walio katika hatari ya kuambukiza au kupata VVU,Pia kwasasa ni rahisi kupima wakati wowote na mahali popote na Kwa usiri kwani vifaa vya kujipima maambukizi vinapatikana kwa wingi na sio katika vituo vya afya pekee kama wakati wa nyuma.

Amini Nyaungo ni mmoja wa vijana ambao wamejitokeza katika maadhimisho haya amesema kuwaa ameitumia siku hii vema Kwa kupima afya yake pia kupata elimu juu ya VVU NA UKIMWI ambayo ataiwasilisha pia Kwa vijana wengine ambao hawana uthubutu katika kupima na kupata elimu ya VVU na UKIMWI.

"Nitaitumia fursa hii Kwa kuwapa vijana wenzangu elimu juu ya VVU,pia ntawaekimiaha kuhusu matumizi ya dawa kinga Kwa lengo la wao kufahamu Nini wafanye pale ambapo wanaona kuwa wapo katika hatari ya kupata VVU na matumizi Sahihi ya ARV Kwa wale ambao wamegundulika kuathirika na ugonjwa huu ila wana hofu ya kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi"alisema Nyaungo.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na maandamano mapema asubuhi,ikifuatiwa na huduma ya kupima afya(VVU NA UKIMWI) na mjadala kuhusu UKIMWI na vijana jinsi gani watajilinda na maambukizi au jinsi gani ya kuepuka kuambukiza wengine VVU.Kaulimbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni "CHAGUA NJIA SAHIHI,TOKOMEZA UKIMWI"








Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.