• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

SINGIDA YAADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI – VIJANA WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA

Posted on: August 12th, 2025

Mkoa wa Singida leo umeadhimisha Siku ya Vijana Duniani katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Ikungi, ambapo vijana wametakiwa  kutumia fursa zinazotolewa na Serikali katika kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa vijana wa Mkoa wa Singida Ndg.Fredrick Ndahani amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa maendeleo ya vijana kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo mikopo ya Asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia Halmashauri,Programu za mafunzo ya stadi za maisha kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Mafunzo ya kilimo cha kisasa na ufugaji kupitia mpango wa BBT kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Kwa upande wa Mkoa wa Singida, Ndahani amesema katika mwaka wa fedha uliopita, jumla ya Shilingi 1,361,894,654.66 zimetolewa kwa vikundi 147 vya vijana kutoka Halmashauri zote za mkoa huo. Aidha, katika sekta ya elimu, Serikali imetoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari, mikopo ya elimu ya juu, na ufadhili wa "Samia Scholarship".

Ameongeza kuwa Serikali imetumia Shilingi Bilioni 41.9 kujenga madarasa 422, vyoo 905, mabweni 28 na maabara 43, pamoja na ujenzi wa shule za amali katika kila wilaya na shule moja ya amali ya mkoa.

Katika wito wake, Ndahani amewataka vijana kutumia ipasavyo mikopo na fursa zilizopo, kuimarisha mshikamano wa vikundi, kushirikiana na viongozi wa serikali na wadau, kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, na kwa wanafunzi, kusoma kwa bidii.

Amehitimisha kwa kuwasihi wazazi na jamii kuendelea kuwalea na kuwaunga mkono vijana, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano wa taifa.

Maadhimisho ya mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu "Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu", ikisisitiza umuhimu wa vijana kama rasilimali muhimu ya taifa katika kuchochea maendeleo.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO SINGIDA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIDIJITALI.

    September 06, 2025
  • ELIMU YA WATU WAZIMA -NGUZO YA MAENDELEO ENDELEVU

    September 01, 2025
  • SINGIDA YAAZIMIA KUBORESHA HALI YA LISHE KWA WATOTO NA WATU WAZIMA.

    August 22, 2025
  • SINGIDA YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA USAFI WA MAZINGIRA

    August 15, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.