• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Ujenzi vyumba vya madarasa Singida washika kasi, RAS Mwaluko atoa wito

Posted on: November 29th, 2021

WATENDAJI wa Serikali katika ngazi ya Kata, Tarafa na vijiji mkoani Singida wametakiwa kutumia muda wao mwingi katika kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa ili kufanikisha ujenzi huo kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.

Mkoa wa Singida umepokea fedha za UVIKO-19 kiasi cha Shilingi Bilioni 13.24 kwa upande wa elimu ili kujenga vyumba vya madarasa 632 ambapo vyumba 330 ni kwa ajili ya shule za sekondari na 330 shule za msingi pamoja na mabweni mawili kwa ajili wenye mahitaji maalum ikiwa ni matarajio ya Serikali kwamba fedha hizo zitasimamiwa na kukamilisha ujenzi huo.

Kauli hiyo imetolewa Novemba 29,2021 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko wakati akikagua miradi mbalimbali ya ujenzi wa vyumba hivyo katika Wilaya ya Mkalama ambapo amebainisha kwamba hali ya ujenzi inaendela vizuri na vyumba vingi vikiwa vimefikia katika hatua ya lenta na vingine vikisubiri kupauliwa.

RAS amewataka viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo watendaji wa vijiji, Kata na Tarafa kuhakikisha haipiti siku bila kujua kinachoendelea katika miradi hiyo ambayo inatakiwa kukamilika kabla ya Desemba 15, mwaka huu.

Ziara hiyo ya RAS imehusisha viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Mkalama ambapo walitembelea miradi katika shule ya Ibaga Kata ya Ibaga ambapo kunajengwa vyumba vitano vya madarasa, Shule ya Sekondari Nduguti kunakojengwa vyumba viwili, Shule ya Sekondari Gunda Kata ya Ilunda kunakojengwa chumba kimoja, Shule ya Sekondari Grace Mesaki kunakojengwa chumba kimoja, Kikhonda Sekondari kwenye ujenzi wa vyumba vitatu (3) na Shule ya Sekondari Iguguno kunakojengwa vyumba vinne vya madarasa .

Akiwa katika miradi hiyo, Dorothy Mwaluko ametuma ujumbe kwa wakuu wa shule zote mkoani Singida zenye miradi inayotumia fedha za UVIKO-19 kuhakikisha wanajenga kwa kufuata michoro iliyokubalika na kuhakikisha kwamba wanafanya mawasiliano ya karibu na wahandisi wa halmashauri za wilaya zao endapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kulinda ubora na viwango vilivyotajwa na wataalamu hao.

Aidha, RAS akawataka viongozi kuhakikisha wanazishirikisha kamati za ujenzi wa madarasa na kamati za mapokezi ya vifaa vya ujenzi, kiasi cha fedha zilizokuja na namna ya matumizi ya fedha hizo kama sehemu ya kuweka uwazi na kutengeneza dhana ya ushirikishwaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo amesema wilaya imepokea fedha kwa ajili ya ujezi wa vyumba vya madarasa 63 na ya shule shikizi 16 ambazo kwa jitihada wanazofanya vyote vitakamilika ndani ya wakati.

DC Sophia amebainisha kwamba, hali ya ujenzi kwa sasa inaendelea vizuri baada ya kumaliza changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi ambavyo amesema vilikuwa havipatikani kwa kuwa zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa unafanyika nchi nzima, hivyo kusababisha changamoto za upatikanaji wa vifaa hivyo.

Amesema, kwa sasa wilaya imeshanunua vifaa vyote vinavyohitajika katika ujenzi huo ambapo amebainisha kwamba asilimia 85 ya majengo yamefikia hatua ya kufungwa lenta wakati asilimia 15 vinafungwa mkanda wa katikati ili kuondoa nyufa zinazoweza kutokea.

DC amefafanua kwamba, mbao zitakazotumika kwa wilaya nzima tayari zimeshafika kilichobaki ni kuzisambaza kwenye shule mbalimbali na mpaka kufikia Novemba 30, 2021 jioni mabati nayo yatakuwa yamefika.

Wakimalizia ziara hiyo katika shule Sekondari Iguguno, DC Sophia amezitaka kamati za mapokezi na za ujenzi kujipanga kupokea vifaa hivyo ambapo watatakiwa kuongeza usimamizi ili kupata thamani ya fedha zilizotumika.

Mwisho DC Kizigo akamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo katika Wilaya ya Mkalama jambo ambalo amesema limeondoa kabisa changamoto ya uhaba wa madarasa.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Juma Mesossi akimuelezea RAS maendeleo ya ujenzi wa madarasa wilayani Mkalama.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothly Mwaluko akiwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ibaga iliyopo Kata ya Ibaga mkoani Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akiongea na viongozi mbalimbali wa mkoa na halmashauri kuhusu maendeleo ya ujenzi.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.