• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Vijana Mkoani Singida Wametakiwa Kuwekeza Katika Kilimo Cha Pamoja Ili Kupata Huduma Kwa Urahisi.

Posted on: April 13th, 2022

Vijana mkoani Singida  wametakiwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili kutumia fursa ya uwepo wa maeneo ya mashamba yaliyotengwa kila Halmashauri kwa ajili ya Kilimo cha pamoja (block farming) ili kuongeza kipato na ajira.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa  ziara yake katika Wilaya ya Mkalama na kuwataka vijana kujiunga katika vikundi ambavyo vitaweza kupewa mashamba makubwa kwa ajili ya Kilimo cha vitunguu na alizeti.

"Kila Halmashauri zimetenga maeneo ya mashamba kwa ajili ya Kilimo cha pamoja hivyo fursa kwa vijana kujiunga katika vikundi na kuvisajili ili Halmashauri zao ziweze kuwakopesha mitaji kupitia asilimia 10 na wawekeze katika kilimo cha alizeti au Vitunguu." Alisema Dk. Mahenge

Ameagiza vijana ambao wanajishughulisha na kilimo kuhakikisha kinafanywa ki Biashara ili kuongeza  tija ambapo amesema kilimo cha pamoja  kitasaidia kupata mikopo sehemu mbalimbali na urahisi wa kupata huduma za ugani kwa pamoja.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mkalama Lameck Tungi, kwa kuwekeza katika kilimo cha vitunguu

Hata hivyo RC Mahenge akatumia nafasi hiyo kwa kumpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya kwa kuwekeza katika kilimo cha vitunguu na kwa hatua aliyoichukua ya kuwasaidia Vijana wengine katika matumizi ya maji ya Umwagiliaji kwa kutumia miundombinu aliyoitengeneza kwa gharama ya zaidi ya Milioni 40.

Aidha Rc Mahenge ameendelea kumpongeza Mwenyekiti huyo kwa kutoa ajira kwa vijana zaidi 90 ambao wanasimamia miradi ya shamba la vitunguu na mabwawa ya samaki huku akihamasisha vijana kujiunga katika shughuli za kilimo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kata ya Bumagwa wilayani Mkalama wakati wa ziara hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo amesema wamejipanga  kuimarisha vikundi vya vijana kwa kutoa mikopo  mikubwa  kwa vikundi vichache ili waweze kuwekeza kwa kiasi kikubwa

Hata hivyo DC Kizigo amesema Wilaya hiyo  imejipanga  katika mwaka huu wa fedha kuvikopesha vikundi kupitia asilimia kumi ambayo kuna mgawanyiko wa asilimia nne kwa vijana, nne kwa wanawake na mbili kwa watu wenye ulemavu lengo likiwa ni kuhakikisha vikundi hivyo vinatoa ajira kwa  watu wengine.

Akitolea mfano wa kikundi kilichopo Iguguno  DC Kizigo amesema Halmashauri ya Mkalama ilitoa mkopo wa Milioni 25 na kuwapatia Mradi wa kufyatua tofali 6000 kwa ajili ya Ujenzi wa shule jambo ambalo liliwasaidia kutoa ajira kwa watu wengi.

Akizungumza kuhusu vikundi vya vijana kuwekeza katika kilimo DC Kizigo amesema ili vijana waweze kupata faida kupitia kwenye kilimo ni lazima wawe tayari kulima  ekari  kuanzia tano na kuendelea.

Kwa upande wake Lameck Tungi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkalama ambaye ni mkulima wa vitunguu katika shamba lenye ukubwa wa ekari 14 amesema kwa utaalamu uliotumika katika shamba hilo anategemea kuvuna  magunia 1200 kwa sababu limekuwa na mchanganyiko wa mvua na umwagiliaji.

Amesema uwekezaji wake katika eneo hilo kumeleta hamasa kwa wakulima wengine ambapo zaidi ya ekari 18 zimelimwa kuzungukia bwawa alilolichimba  kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkalama Lameck Tungi (kulia) ambaye ni mkulima wa vitunguu katika shamba lenye ukubwa wa ekari 14, akizungumza wakati wa ziara katika shamba hilo.

Lameck ametoa wito kwa vijana kushiriki katika kilimo cha pamoja ili kupata urahisi wa huduma za ugani na masoko ambavyo vitaondoa changamoto ya ukosefu wa ajira.

Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa ililenga kukagua  hali ya Kilimo katika eneo hilo, ukaguzi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Bumagwa Ujenzi  wa shule ya Nyeri na kuangalia maendeleo ya Ujenzi wa miradi ya maji katika Wilaya hiyo ya Mkalama.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati alipotembelea shamba hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akishiriki uchimbaji wa msingi kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Bumagwa wilaya Mkalama leo Aprili 13, 2022


www.singida.blogspot.go.tz

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.