• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

WAFANYABIASHARA WATOA CHANGAMOTO NA KERO ZAO, SULUHU KUPATIKANA

Posted on: January 22nd, 2025

Viongozi na wajumbe kutoka Tume ya Rais ya maboresho ya Kodi wamefika Mkoani Singida kwa lengo la kuzungumza na Wafanyabiashara,wajasiriamali wadogo na wakubwa  Mkoani Singida pamoja na kusikiliza kero, changamoto,na kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwao kwa lengo la kuhakikisha wanakuwa kibiashara na kuongeza wigo wa kulipa kodi.

    Wafanyabiashara hao wametoa maoni  yao ikiwa ni pamoja na kuiomba  Mamlaka ya mapato nchini TRA kuanzisha maduka darasa ili wafanyabiashara wajifunze kupitia maduka darasa hayo kama ambavyo sekta zingine zinafanya,Lakini pia wameshauri ajira za TRA ziwape kipaumbele vijana waliosomea mambo ya kodi ili kuongeza ufanisi katika kusimamia kodi.

    

  Pia wameomba kupunguzwa kwa vizuizi barabarani ambavyo vimekuwa ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara wanaposafirisha mizigo yao  hivyo Tume hiyo iangalie katika eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi mbadala.

Aidha,wafanyabiashara hao wameiomba tume hiyo  kurejesha vitambulisho vya wafanyabiashara wajasiriamali vilivyokuwa vikilipiwa Shilingi Elfu ishirini ili kuongeza idadi ya walipakodi nchini  na kuchochea  maendeleo.

Katibu Tawala  Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga akizungumza baada ya kusikiliza kero mbali mbali za Wafanyabiashara amewaagiza TRA kuhakikisha wanafanyia kazi malalamiko yote yaliyotolewa pamoja na kuboresha huduma zao ili ziwe rafiki kwa wateja wao kwa lengo la kuhakikisha ongezeko la mapato katika Mkoa bila kuathiri Wafanyabiashara.

Pia aliwasilisha changamoto ya kukosekana ya uandaaji wa mahesabu ya biashara inayosababisha kufungwa kwa biashara  baada ya ukaguzi kwa wafanyabiashara ambao hulalamika kukosekana kwa uwiano wa tozo wanazodaiwa na faida inayopatikana.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida akiwapokea wajumbe hao ofisini kwake amesema ni wakati sahihi kwa wao kufika Singida ili kusikiliza maoni na changamoto Wafanyabiashara wanazopitia katika kazi zao.

Amesema kuwa ,makusanyo ya kodi  Mkoani Singida yapo vizuri kwani wananchi wanajitambua na wanalipa kodi licha ya changamoto zilizopo ikiwemo elimu ndogo ya ulipaji kodi hususani vijijini,matumizi madogo ya mashine za EFD,na mrundikano wa tozo katika Halmashauri.

Amesema kuwa kama Mkoa wameandaa mikakati ya kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa kushirikiana na TRA pamoja na kusisitiza matumizi ya mashine za EFD kwa wafanyabiashara.Pia kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo miundombinu ya barabar na masoko,pia, kutumia rasilimali na vyanzo mbadala kuongeza mapato.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya maboresho ya Kodi,Balozi Ombeni Sefue amewahakikisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida kuwa  wataziwasilisha kero zao zote  kwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na wataendelea kupokea kero zao kupitia njia  mbalimbali ikiwemo barua pepe.

Mkutano huo umewakutanisha viongozi na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, wakuu wa Sehemu na vitengo, Wakurugenzi wa Halmasahauri, Wakuu wa Taasisi za umma na binafsi, wawakilishi wa Wafanyabiashara, wanawake wajasiriamali na Chama cha watu wenye ulemavu.


@USIKOSE KUFUATILIA MITANDAO YETU YA KIJAMII

INSTAGRAM:SINGIDA RS

FACEBOOK:SINGIDA RS

YOUTUBE:RAS SINGIDA 


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.