• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Watoa huduma za afya kutembelea nyumba kwa nyumba kuondoa tatizo la vifo vya mama na mtoto wakati wa uzazi

Posted on: August 31st, 2021

Watoa huduma za afya katika ngazi za kata na vijiji wametakiwa kutembelea nyumba kwa nyumba ili kuwatambua mama wajawazito na watoto walioko maeneo hayo ili kuwapatia ushauri wa kiafya kwa kuwa hao ndio wateja wao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith  Satano Mahenge ametoa kauli hiyo leo tarehe 31.08.2021 alipokuwa akifungua kikao kazi cha Wataalam wa afya wa Mkoa wa Singida kilichokuwa kinajadili tathmini na vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika ukumbi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni  mkoani Singida.

Akifungua kikako hicho Dkt. Mahenge amesema kwamba bado kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza au kuondoa vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi pamoja na watoto wachanga endapo wataalamu wa afya ngazi ya kata na vijiji watatembelea nyumba kwa nyumba kuangalia uwepo wa watu hao na kuwapatia ushauri wa kwenda hospitali kwa wakati na kutumia lishe bora kwa afya ya mama na mtoto.

 

“Kutembelea  nyumba kwa nyumba kutasaidia kujua  idadi ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya afya na ushauri katika eno husika, hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wengi huchelewa kuanza kiliniki pindi wanapokuwa wajawazito na kusababisha matatizo wakati wa kujifungua” alikaririwa Dkt. Mahenge.

Amesema Serikali  ya awamu ya sita chini Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kujenga miundombinu wezeshi kwa sekta ya afya  ikiwa ni pamoja na kuongeza bajeti na idadi ya watumishi katika sekta hiyo ili kusogeza huduma na elimu ya afya  kwa wanachi.

Amesema ujenzi na uboreshwaji wa vituo vya afya ni mkakati wa Serikali wa kuondoa changamoto ya vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga.

Hata hivyo Dkt. Mahenge amebainisha kwamba  jumla ya vituo vya afya 15 na hospitali tatu (3) zimejengwa mkoani hapo ili kusaidia utoaji wa  huduma za dharura  kwa wazazi na watoto.

Aidha Mhe. Mahenge amezitaka Halmashauri mkoani hapo kuhakikisha kwamba vituo vyote vya kutolea huduma ya afya vinakuwa na mikakati ya kupunguza au kuondoa  vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na changamoto ya vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika.

Pia amezitaka Halmashauri kuimarisha upatikanaji wa bidhaa afya kutoka MSD na kwa mshitiri  hasa kwa bidhaa za mama na mtoto kama vile vifaa tiba vya kupimia wingi wa damu, kuhakikisha uwepo wa dawa za kuongeza damu katika vituo vyote pamoja na dawa  muhimu za kuzuia damu kutoka baada ya kujifungua na matibabu mengine muhimu katika kundi hili.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Victorina Ludovick amesema lengo la kikao kazi hicho ni kujadili na kutathmini vifo vya kinamama vilivyosababishwa na uzazi vilivyotokea kwa muda wa miezi mitatu ya April hadi Juni 2021 ambapo kikao hicho kitatoa  suluhisho la namna ya kuzuia hali hiyo isiweze kujirudia.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kinategemewa kutoa mrejesho wa matukio kadhaa ya vifo vilivyojitokeza na kujadili mipango kazi ya Halmashuari  hizi kwa kipindi cha miezi mitatu na kuchukua hatua stahiki za kuboresha maeneo yenye changamoto, alisema Dkt.Victorina

Aidha alibainisha kwamba bado kuna changamoto ya jamii yetu kwenye kupanga uzazi na pia vijana kupata  mimba wakiwa katika umri mdogo ambapo wengi wao hupoteza  maisha kwa kutokwa na damu vyingi wakati wa kujifungua.

 “Bado tuna changamoto ya ukusanyaji wa damu salama ambayo hutumika kuwasaidia kinamama na watoto wanapokuwa na uhitaji”. Alisema Mganga Mkuu wa Mkoa

Dkt. Victorina amewaomba wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchangia damu ili iweze kuwasaidia wenye uhitaji.

Hata hivyo Mganga Mkuu amewataka wahudumu wa afya kuendelea kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi kwa kuwa itawezesha kuwa na uzazi salama na pia ina mchango mkubwa katika kuzuia vifo vya kinamama vinavyosababishwa na uzazi.

Naye Emanueli Mlalange  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Itigi na Mwenyekiti wa Waganga wakuu wa mkoa huo kwa niaba ya waganga  hao ameishukuru serikali kwa jitihada zake za kuongeza watumishi mkoani hapo na kuimarisha utoaji wa dawa katika vituo vya afya.

Aidha amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba madaktari watajitahidi kuhakikisha kwamba vifo vya kinamama na watoto wachangavinapungua.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.