• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

"WAUMINI TUTUNZE AMANI NA UTULIVU TULIO NAO":RC DENDEGO

Posted on: June 7th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amesisitiza umuhimu wa kutunza amani na utulivu katika Taifa letu,akisisitiza waumini kuendelea kutunza umoja na ushirikiano walio nao kama nyanja muhimu ya kuwaweka pamoja na kufanya shughuli za maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo Juni 7,2025 katika kanisa la Unyankindi Mkoani Singida wakati alipoalikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee ya ujenzi wa kanisa hilo  ambapo pia amewahimiza wananchi kutumia jukwaa la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu vema kwa ajili ya kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo na kuitunza amani iliyopo hapa nchini.

“Tunaenda kwenye uchaguzi mwaka huu. Tuendelee kuomba amani. Suala hilo litufikie na liishe salama. Tuwe wamoja – iwe Waislamu, Wakristo, KKKT au dhehebu lolote – tuwe wamoja katika kulinda amani,” amesema Mhe. Dendego

Aidha, Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa kusaidia kwenye ujenzi wa nyumba za ibada ni sehemu ya maandalizi ya safari ya kiroho ya kila mwanadamu hivyo ni vema kila mmoja kushiriki ili kuwezesha kazi ya Mungu kusonga mbele kadhalika na kumpa kila mmoja baraka.

“Msafiri bora ni yule aliyefunga mizigo yake sawasawa.. na mizigo hiyo ni kama hii ya ujenzi wa kanisa, kusaidia maskini, kuwajali yatima. Haya yote yanatuandalia safari njema ya kesho,” 

Naye Mchungaji Livingstone kutoka nchini Kenya,akizungumza qakati wa harambee hiyo,amewaasa Watanzania kuilinda na kuitunza vizuri amani waliyonayo kwqni ni hazina kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na utulivu uliopo nchini Tanzania ambao unawapa wananchi nafasi ya kushiriki vema katika shughuli za uzalishaji ambazo  zimekua kichocheo kikubwa cha maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Nimesafiri nchi nyingi sana, lakini amani ya Tanzania ni ya kipekee. Tanzania mna amani sana chini ya uongozi huu. Ithaminini hiyo amani yenu,” amesema.

Kwa upande wake, Mchungaji Dr. David, Askofu Mkuu wa Kanda ya Kati wa Kanisa la Waadventista Wasabato, amemshukuru Mgeni rasmi wa Shughuli hiyo- Mkuu wa Mkoa na waumini wote wa ujumla kwa kukubali kushiriki katika harambee hiyo iliyogusa mioyo yao na kufanikiwa kufikia lengo lililotarajiwa.

Katika harambee hiyo iliyokua na lengo la kukusanya jumla ya Shilingi Milioni mia moja,imefanikisha kupata zaidi ya shilingi milioni mia moja na kuvuka lengo lililopangwa hapo awali huku Mkuu wa Mkoa akichangia kiasi cha Milioni 15.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • MAAFISA MAENDELEO KIKAANGONI,WAASWA KUJIPIMA KWA MATOKEO NA SIO IDADI YA VIKAO.

    June 30, 2025
  • HAPO AWALI NA SASA KATIKA MIUNDOMBINU YA ELIMU SINGIDA

    June 27, 2025
  • MIRADI MBALI MBALI YA UJENZI INAYOENDELEA MKOANI SINGIDA

    June 27, 2025
  • WENYE MAHITAJI MAALUM SINGIDA WASHIKWA MKONO

    June 25, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.