• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

WAZAZI WASISITIZWA KUWALINDA WATOTO KIPINDI CHA SIKUKUU

Posted on: March 31st, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanafuatilia vema mienendo ya watoto wao hasa katika sikukuu ya leo ya Eid AL Fitr ambazo watoto huwa na uhuru mwingi wa kutembea peke yao maeneo mbali mbali.

Ameyasema hayo  leo katika sala ya asubuhi ya kusherehekea siku kuu ya Eid Al Fitr baada ya  kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mhe.Dendego Amesema kuwa katika kipindi cha siku kuu zinazojumuisha watu wengi wa kila rika ni vema watoto wakapatiwa uangalizi maalum kwa lengo la kuwaweka katika mazingira rafiki ikiwemo kutembea pamoja nao badala ya kuwaacha pekee yao,kuwa makini katika vyakula na vinywaji wanavyotumia kwa kuhakikisha ni Salama kiafya pia kulingana na umri wao.

Pia amesisitiza kuwaweka katika mazingira rafiki ili kuepusha kufanyiwa kitendo visivyo vya kimaadili na watu wasiofahamika na kuharibu utu wao kwa lengo la kuwaweka salama na kukua vema kiafya,kimwili, na kiakili.

Sambamba na hilo Mheshimiwa Dendego amewasilisha salamu za Rais Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa waumini wa dini ya kiislamu kwa kuwataka kusherehekea kwa amani na kuyaishi yale yote yaliyofanyika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa kudumisha upendo,amani,kusaidiana na kutembeleana.

"Tusherehekee sikukuu ya leo kwa amani,tutaishi yake yote mema tuliyoyatenda mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kusaidiana,kutembeleana, na kuwajali wenye mahitaji muhimu,Pia tuwape watoto uangalizi mzuri katika siku kuu kwa kuwapa uangalizi kuhakikisha wapo salama muda wote wa sikukuu na baada ya sikukuu za Eid."amesema Mhe.Dendego.

Awali Sheikh wa Mkoa wa Singida,Sheikh Issa Nassoro,amewashauri waumini wa dini ya kiislamu kuhakikisha wanawapa ushirikiano wa kutosha Viongozi wa Serikali  kwa kuwasikilza ,kutii na kufuata maagizo yanayotolewa na Serikali kwa  manufaa ya wote.

Amesisitiza kuwa kutowapa ushirikiano Viongozi hao ni chanzo cha mtafaruku na changamoto mbali mbali katika jamii kwani maendeleo hayatakuwapo endapo kukiwa na matabaka kati ya wananchi na viongozi wao mfano kuwepo kwa milipuko ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza katika jamii kwa sababu ya kushindwa kusikiliza maelekezo ya namna ya kujilinda,kujikinga na magonjwa mbalimbali.Pia katika uzalishaji italeta athari nyingi kwa jamii ikiwemo kukosa mazao ya kutosha kutokana na kutosikiliza na kufuata taratibu zinazotolewa na serikali kupitia kwa viongozi.

Kadhalika,Sheikh Isihaka Hassan Salum akitoa mawaidha,aliwasisitizia waumini wa dini ya kiislamu kuishi katika sifa za waumini wa dini hiyo ili kudumisha uhusiano mwema katika jamii ikiwemo Kujichunga na maasi  ya kuwaudhi watu na mwenyezi Mungu kwa kuwaudhi watu wengine,kutukana,na kuwanyanyasa.

Pia amesisitiza kuwa muumini bora hapaswi  kuwafitinisha watu bali anapaswa kuwaunganisha watu pamoja,wawe na tabia ya kutoweka vitu katika mioyo,bali wawe wepesi wa kusema yanayowaudhi mioyoni mwao na kusamehe ili wakatende mema yale wanayopenda kufanyiwa na wengine.

Akizungumza baada ya swala ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Rashidi Hakimu,muumini na mkazi wa Mkoa wa Singida amesema leo ni siku njema hivyo ni vema tuisherehekee kwa amani na utulivu na kudumisha tabia njema hasa kimavazi kwa vijana kuendelea kujisitiri kwa vijana hata baada ya mwezi Mtukufu.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.