• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Zoezi la upandaji miti laendelea kwa kasi Manyoni na Ikungi.

Posted on: January 21st, 2023

WAKATI Mkoa wa Singida ukijiandaa na maadhimisho ya Siku yake ambapo unatimiza Miaka 60 imeanzishwa kampeni ya upandaji miti ambapo jumla ya miti 254,880 imepandwa tokea zoezi hilo lilipoanza tarehe 07 January 2023.

Zoezi hilo linatekelezwa kila siku ya Jumamosi ambapo kwa wiki hii Wilaya mbili za Ikungi na Manyoni zilipanda idadi hiyo ya miti mbapo Ikungi imepandwa miti 54,000 na Manyoni miti 200,880 toka kuanza kwa kampeni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewapongeza wananchi wa Wilaya hizo na kuwataka kuzilinda na kuitunza miti hiyo ili iweze kukua.

Akiongea na wananchi wa Wilaya hizo leo wakati wa zoezi la upandaji miti lililoanzia katika mpaka wa Manispaa ya Singida na Ikungi mpaka  Kintiku mpakani mwa Dodoma na Singida ambapo RC Serukamba amesema lengo la Mkoa ni kupanda miti Milioni tatu kwa Mkoa mzima (3,000,000) kwa mwaka 2023.

RC Serukamba ameeleza kwamba miti hiyo inapandwa katika maeneo ya kingo za Barabara kufuata bikoni zake, mashuleni Hospitalini, vyanzo vya maji, majumbani na kwenye nyumba za ibada.

Aidha Serukamba ameagiza Wakuu wa shule kupitia Maafisa Tarafa na kata kuhakikisha miche inapatikana mashuleni ambapo kila Mwanafunzi atapatiwa miti minne wakapande nyumbani kwao.

Hata hivyo RC ametoa maagizo kwa wenyeviti wa Halmashauri na Madiwani kuhakikisha wanatunga Sheria kali zitakazo wafanya wafugaji kuwa makini na mifugo yao sambamba na kuweka faini kubwa kwa atakaye sababisha mfugo kula miti hiyo.

Serukamba ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Ikungi kuhakikisha wananchi wa Ikungi wanapunguza tabia ya ukataji miti hovyo na uchomaji wa mkaa kwakuwa imeonekana eneo hilo ndilo athirika zaidi.

Akimalizia hotuba yake Mkuu wa Mkoa huo ameahidi kuwakutanisha Wakuu wa Wilaya wote na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayojishughulisha na uboreshaji wa Miche ili waweze kuisaidia halmashauri ambazo zina changamoto hiyo.

Kwa upande wake DC wa Ikungi Jerry Muro amesema wameshaweka mkakati kupitia Maafisa Tarafa na kata kuhakikisha kuwa wanapanda miti Milioni moja na laki tano kwa Wilaya nzima.

Amesema Mpango huo utakamilika kwa kuanzisha vitalu vya miti kila kata ambapo itakuwa rahisi kuisambaza kwa wananchi na kuzisimamia kikamilifu.

Jerry Muro ameeleza changamoto ambayo inaweza kutokea ni upungufu wa miche ambapo amemuomba Mkuu wa Mkoa huo kuharakishwa kuwakutanisha na wadau wanaozalisha miti ili zoezi lisikwame.

Naye DC wa Manyoni Rahabu Mwagisa amesema wameweza kupanda miti  200,880 kwa kushirikiana na Taasisi ya Wakala wa misitu Nchini (TFS) na muitikio mzuri wa wananchi.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko akishiriki zoezi la upandaji miti

Mwisho.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.