• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

*BAKWATA SINGIDA BEGA KWA BEGA NA MHE.DENDEGO

Posted on: January 25th, 2025

Baraza la Waislamu Tanzania(BAKWATA )Mkoani Singida wameandaa Kongamano la kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego kwa kazi kubwa na ushirikiano aliyouonyesha kwa Taasisi za dini, madhehebu yote ambayo yamekua ni kiungo muhimu katika kuwaunganisha Wanasingida pamoja na kuwa daraja la maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,biashara ,ulinzi na usalama wa mali za wananchi na maadili kwa ujumla.

Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwenge leo Jumamosi Januari 25,2025 likihudhuriwa na viongozi mbalimbali kama vile Mkuu wa wilaya ya Singida Mhe.Godwin Gondwe,Meya wa Manispaa ya Singida na wengineo.

Sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Nassoro akizungumza wakati wa gafla hiyo ameainisha sababu mbali mbali za kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ikiwemo usimamizi wa uchaguzi Serikali za mitaa,kuongezeka kwa Mapato ya ndani kutokana na usimamizi bora,Pongezi kisekta katika sekta za Elimu katika Uandikishaji ,ufaulu wa Kidato cha sita,Kidato cha nne,Kidato cha pili na darasa la nne.

Sheikh Issa Nassoro amewaasa wanajamii  kuwa na umoja kwa kushirikiana mambo mbalimbali ikiwa ni moja ya nyanja kuu ya kudumisha uhusiano mwema baina ya wanajamii kwa lengo la kudumisha ushirikiano na kuchochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.

"Maendeleo lazima kuzingatia Umoja, Huwezi pata Maendeleo bila umoja,wito wa Baraza Kuu la kislamu BAKWATA  kwa wote ni kudumisha umoja ambao utatutoa hapa tulipo kwenda kwenye Maendeleo ,Umoja hauwezi patikana bila Mshikamano ili kuweza kufanikiwa"amesema Sheikh Issa.

Pia ametoa ombi kwa serikal kuwashirikisha viongozi wa dini katika kulinda na kujenga maadili kwa  kushirikiana na Polisi Kata na watendaji pamoja na kuomba marekebisho ya Katiba ya mwaka 1999 huku akiwaonya watumishi kukosa ushirikiano, mshikamano na nidhamu kwa kutosikiliza maelekezo ya viongozi.

Naye Yohana Msita, Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Martha Mlata ,ametoa Pongezi kwa Viongozi wa Bakwata  kwa kuendelea kuwa moja ya Taasisi za dini zinazoimarisha amani ya Mkoani Singida kwa kukemea vitendo viovu kwa jamii kupitia mafunzo mbalimbali.

Akitoa shukurani zake katika hafla hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amewashukuru Viongozi wa dini zote Mkoani Singida akisema kuwa tangu kufika kwake Singida wamekuwa walezi na washauri kwake na kusema kuwa pongezi hizo zimemtia moyo na kumpa hamasa ya kufanya kazi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  suala la mmomonyoko wa maadili katika Mkoa wa Singida amebainisha moja ya sababu kubwa ya kuwa katikati ya nchi  na kukutanisha watu wa jamii mbalimbali wenye tabia za tofauti, akisema kuwa  mikakati mbali mbali imeandaliwa ikiwemo kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mbalimbali za kimaadili.Pia kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali kuanzisha darasa la malezi kwa wazazi majumbani pia kutoa elimu ya dini na maadili kwa wanafunzi mashuleni.

Akizungumzia suala la uchaguzi Mkuu mwaka huu, ameomba wananchi kushiriki katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025 kwa amani na utulivu kama walivyoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.