• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

CHANGAMOTO ZA KIFEDHA KUTAFUTIWA UTATUZI SINGIDA*

Posted on: December 2nd, 2024

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema asilimia 10 tu ya watu wazima mkoani Singida ndio wanaotumia huduma za benki kiwango ambacho kipo chini ukilinganisha na kiwango cha kitaifa ambacho ni asilimia 22.

Kaimu Meneja msaidizi sera na chambuzi za huduma za kifedha kutoka BoT, Edmund Mbokosi alisena hayo Leo katika kikao cha kujadili changamoto za kifedha na utatuzi wake Mkoa wa Singida ambacho kimewashirikisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na mameneja wa benki zinazotoa huduma za kifedha mkoani hapa.

Amesema katika huduma za kifedha Mkoa wa Singida wanatumia asilimia 50 wakati wastani wa kitaifa ni asilimia 72,bima ni asilimia 5,huduma za vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) Singida ni asilimia 7 wakati lengo la kitaifa ni asilimia 12.

Mbokosi amesema kutokana na changamoto hiyo BoT imemua kuja kutoa elimu ili kuangalia namna ya kuweza kupandisha kiwango cha matumizi ya huduma za kifedha katika mkoa wa Singida kwa lengo la kuufanya mkoa kupanda kiuchumi na kuondoka katika nafasi ya tatu kutoka mwisho.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, amesema mkoa utajitathimini kwenye sensa kwa kupita kwenye maeneo mbalimbali kama kwa wanafunzi mashuleni na vyuo vilivyopo mkoani hapa ili kupandisha kiwango cha huduma za benki.

"Tuna vyuo vingi na taasisi nyingi na karibia kila mtu anatakiwa kulipwa pesa kupitia benki na hivi sasa kuna huduma mpya mfano ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa hiyo nina imani kiwango acha asilimia 72 cha huduma za kifedha tutakifikia," alisema. Ok Google

Awali Mchambuzi Maswala ya fedha kutoka BoT, Michael Mwaituka, alisema BoT imejipanga kuwasaidia wajasiriamali nchini kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (ECGS) pamoja Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (SME-CGS).

Amesema lengo la kuwezesha sekta binafsi wenye miradi mizuri kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha zilizosajiliwa chini na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha 2006, pale wanapokuwa na upungufu wa dhamana.

Mwaituka amesema  kuwa BoT wanasimamia Mfuko wa Udhamini wa Mkopo kwa niaba ya serikali ili kuwasaidia watanzania kupata mitaji kuongeza uzalishaji, ajira, fedha za kigeni na pato la Taifa kwa ujumla.

Amesema  kuwa Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa kati una lengo la kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati wenye miradi mizuri lakini wana upungufu wa dhamana, kuweza kupata mitaji kutoka kwenye mabenki na taasisi za fedha zinazosimamiwa na Benki Kuu.






Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.