• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Dkt. Mahenge Afanya Ziara Kwenye Masoko Kubaini Changamoto Na Kero Za Wamachinga.

Posted on: September 20th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge leo amefanya ziara katika masoko na mitaa ya  manispaa ya Singida ili kubaini hali halisi  ya maeneo hayo na changamoto zinazowakabili  wafanya biashara wadogo  maarufu kama wamachinga.

Ziara hiyo iliyoshirikisha Kamati ya Usalama ya mkoa na viongozi mbalimbali wa manispaa hiyo ililenga kubaini maeneo yenye changamoto kwa wafanya biashara wenye maduka na wanaopanga bidhaa barabarani.

Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa amewataka  wakurungezi na wakuu wa wilaya kuhakikisha zoezi la kuwahamisha wafanyabiashara hao linafanyika kwa njia ya majadiliano badala ya kutumia nguvu.

Aidha Dkt. Mahenge amemshauri Mkurungezi wa Manispaa ya Singida mjini ashirikiane na vyombo vingine ikiwemo TARURA  ili walete mapendekezo ya maeneo tarajiwa pamoja na mipango ya namna ya utekelezaji.

Hata hivyo amebainisha kwamba maeneo tarajiwa lazima yaandaliwe vizuri ikiwemo ujenzi wa vyoo, uwepo wa umeme na maji ili maeneo hayo yawavutie wafanyabiashara.

Aidha amesema mchakato wa kubaini maeneo mapya ya kufanyia biashara na mipango ya kufunga baadhi ya Barabara  kwa nyakati tofauti  inafanyika ili kuhakikisha kila mfanya biashara anaendelea na shughuli zake bila kubughuziwa.

“Nashauri wafanyabiashara wa mjini ambao watatakiwa kupisha maeneo waliopo watafutiwe mengine upande wa huko mjini na wafanyabiashara wa mitaani watafutiwe maeneo  karibu na mitaa yao.” alisema Dkt. Mahenge

 Hata hivyo amewataka wataalamu mbalimbali waliofuatana nao kutumia fursa hiyo kufanya mipango miji wakati wa kufungua maeneo mapya kwa ajili ya biashara.

Ametoa wito kwa wakurugenzi na wakuu wa wilaya kushirikiana ili kuhakikisha zoezi la kuwapanga wafanyabiashara hao halichukui muda mrefu iwe wameshapatiwa maeneo mapya ya bishara kwa njia ya majadiliano.

Ziara hiyo ilifanyika katika kata ya Ipembe barabara Nyerere, Lumumba, sokoni na Posta ambapo kata ya majengo   ilifanyika ziara barabara ya usafirishaji, Ukombozi na Kituo cha mabasi cha zamani.

 Wakati kata ya mandewa ilifanyika maeneo ya Ginnery kuelekea hospitali ya manispaa.

MATUKIO KATIKA PICHA

Dkt. Binilithi Mahenge akiwa katika ziara kwenye soko la Kariakoo  manispaa ya Singida mjini kuangalia changamoto na kero  za wamachinga

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Dorothy Mwaluko (aliyeshika kitambaa) akitoa ufafanuzi kwenye baadhi ya mambo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Bi Sophia Kizigo (kulia ) akijadili jambo na Mkurugenzi mtendajia Halmashauri hiyo  Bi  Asia Juma Messos wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa iliyofanyika katika Kata tatu za manispaa ya Singida mjijni

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.