• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

Posted on: May 27th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga amewaasa watumishi kuweka mbele maadili ya utumishi wa umma katika kutoa huduma sambamba na kujituma kwa bidii ili kuwaimarisha katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria, uwazi na uwajibikaji ili kuongeza imani ya wananchi kwa taasisi za serikali.

Daktari  Mganga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo juu ya Rushwa kwa Watumishi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo Mei 27,2025 ambapo Mafunzo hayo yametolewa na Afisa wa TAKUKURU Mkoa wa Singida na yaliyohudhuriwa na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida.

Awali  Dkt. Fatuma Mganga amewasistiza Watumishi wote kuwa na mwenendo mzuri ambao utawanufaisha wananchi bila kudhulumu haki zao na wafanyakazi wenzake.Kadhakika ameongeza kuwa Watumishi wa Umma wote wanatakiwa kujikumbusha Kila mara kuhusu maadili ya kazi na maelekezo ya namna ya kufanya kazi walizoajiwa nazo huku akiwataka  Watumishi wa Umma wote kujitathmini na kubadilika baada ya kupata mafunzo hayo kwa manufaa ya nchi na wananchi wote.

"Rushwa si suala la kutoa ama kupokea fedha ama kitu bali hata uchelewaji na kutokufanya kazi kama ipaswavyo au Serikali ivyokutuma kufanya, Wengine huenda wakawa wanafanya vitendo vya Rushwa bila kujua hivyo tunapaswa kuwasikiliza wataalamu hawa ili tuweze kujitafakari vizuri katika maadili ya kazi zetu kadhalika yapasa tuwe na tabia ya kuripoti matendo hayo ya Rushwa bila woga, na kutoa Ushirikiano wa dhati na ushahidi unaohitajika katika kitengo cha TAKUKURU".amesema Daktari Mganga.

Naye Afisa wa TAKUKURU mkoa wa Singida,Bw.Onesmo Mdegela akitoa mafunzo haya,amesistiza kuwa Watumishi wazingatie maadili na kuwa na Staha katika kazi pamoja na kuzingatia haki za wafanyakazi  na wananchi kadhalika na kuepukana na mitego mbalimbali wanazoweza kuingia bila kufahamu ikiwemo kupokea zawadi

 "Tuepuke kupokea zawadi kutoka kwa watu tunaowahudumia,zawadi sio Rushwa lakini inakuweka kwenye mgongano au ukinzani wa nafasi na maslahi  ambayo husababisha upendeleo na pia kwenda kinyume na sheria za nchi na hatimaye kuingia kwenye mkondo wa Rushwa. Serikali imeweka mfumo kuwa ukipokea zawadi usiitumie, iwasilishe kwa kiongozi, wako ndipo apange matumizi"

Bw. Mdegela,amefundisha pia nadharia za maadili ikiwemo nadharia ya maadili ya matokeo ambayo hupimwa kutokana na utendaji kazi na matokeo ya utendaji ya mtumishi husika ambayo hupimwa kwa uzalendo bila kuangalia masilahi binafsi kwa kuzingatia manufaa ya wengi pamoja na nadharia ya maadili ya uwajibikaji kwa watumishi kufanya kazi kwa namna ambayo wengine watajifunza kutoka kwako kwa kuwa mfano wa kuigwa ikiwemo suala la kuzingatia muda.

Kadhalika amewaasa watumishi kutokuwa na hofu ya kuripoti vitendo mbalimbali vya kuombwa rushwa ikiwemo Rushwa ya ngono ambayo wengi wanapata uoga wa kuiripoti,sambamba na kufanya kazi kwa uaminifu na kujituma na ufanisi bila kusukumwa,kufanya kazi kwa taaluma husika,kusimamia fedha za umma vizuri,kujali mipaka ya kazi kwa kuwa na maisha binafsi yenye heshima mambo ambayo yatawaepusha na kujiingiza katika vitendo vya kuomba au kupokea rushwa.


Bw.Fredrick Ndahani,Afisa Vijana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida akizungumza baada ya mafunzo hayo,amesema kuwa amejifunza kuwa muwajibikaji kwa kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili kujiweka mbali na mambo yanayotoa mwanya wa rushwa,kadhalika kutoa huduma bora na za kuridhisha kwa jamii ili kuwapa huduma bora wanazostahili.

Mafunzo hayo yanalenga na kuwakumbusha Watumishi wa Umma watumie mamlaka yao vizuri na wasipende kutumiwa ama kutumika vibaya,kadhalika kuwa na utambulisho mzuri katika jamii zao kwa kuhakikisha wanakua na staha,utu na matendo mema ili kuijengea heshima kazi,Taasisi na jina la mtumishi binafsi.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.