Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilianzishwa rasmi Februari 5, 1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar, kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amaan Abeid Karume.
CCM imeendelea kushinda chaguzi zote sita (6) za Urais tangu kuanzishwa kwa vyama vingi mwaka 1992. Huku kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Viongozi walioshinda Urais kwa tiketi ya CCM kwenye chaguzi hizo ni Benjamin Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na Dk. John Joseph Pombe Magufuli
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi kwa sasa ni Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu Mwenyekiti Zanzibar akiwa Nje.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Ndugu Stephen Masato Wasira akiwa Makamu mwenyekiti Tanzania Bara.Katibu Mkuu wa CCM ni Dkt.Emanuel John Nchimbi.
CCM inazo Jumuiya tatu ambazo zinafanya kazi kwa kuyaunganisha makundi ya Vijana (Umoja wa Vijana wa CCM), Wanawake (Umoja wa Wanawake Tanzania- UWT) na Jumuiya ya Wazazi Tanzania. Jumuiya hizi kila moja ina viongozi ambao muundo wake unafanana na ule wa CCM yenyewe kuanzia ngazi ya Mwenyekiti Taifa hadi ngazi za matawi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Chama kikubwa zaidi, kikongwe, chenye nguvu na mvuto barani Afrika, kinachoongoza kwa kuwa na Wanachama zaidi ya millioni 12.
SINGIDA
Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA
Telephone: 2502170, 2502089
Mobile: 2502170, 2502089
Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.